mkuu nimekusoma ila kwa kifupi Lissu alitoautetezi uliokuwa umejitosheleza kabisa. JK inabidi aangalie kwa mapana hao wateule wakeWakuu kwa wale ambao hawafahamu kile Lissu alichosema kuhusu huyu JA, soma hapa kwa umakini
JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK
Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba: "Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano."
Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, "mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba." Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba. Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.
Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong'ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani. Aidha, monong'ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.
Jamani mimi naomba kuuliza tu, hivi kama mtu aliferi form four baadaye akatengeneza cheti cha kijanja mpaka akapata Degree kihalali, hivi huyu kesi yake ikoje? naomba jibu kabla sijalipuwa bomu.
N:B, Mkumbuke miaka ya nyuma ulikuwa unaweza kufoji cheti cha form four na kuendelea na Elimu ya juu bila kukalili darasa, kwahiyo sitalajii swali kuhusu hilo.
Mkuu nijuavyo mimi ni kunyang'anywa kila kitu cha taaluma alichonacho kwa sasa sababu ndio kimepelekea yeye awe hapo hayaJamani mimi naomba kuuliza tu, hivi kama mtu aliferi form four baadaye akatengeneza cheti cha kijanja mpaka akapata Degree kihalali, hivi huyu kesi yake ikoje? naomba jibu kabla sijalipuwa bomu.
N:B, Mkumbuke miaka ya nyuma ulikuwa unaweza kufoji cheti cha form four na kuendelea na Elimu ya juu bila kukalili darasa, kwahiyo sitalajii swali kuhusu hilo.
Watu mmejaa wivu wa kike..
kwa nini wasiwapeleke kule Chuo Uongozi wa Mahakama cha Lushoto, Tanga ambapo wangepigwa msasa mzuri tu wa wiki moja kwa kutumia wataalam wetu kama kina majaji waliobobea wastaafu na hata kumwalika Mh. Tundu Lissu, Prof. Safari n.h badala ya kwenda wiki moja huko RIPA , Uingereza CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA - LUSHOTO kwa ajili ya customised - training Strategic and operational management, organisational development and capacity building huku RIPA hawajui mahitaji yetu watanzania.
Watu mmejaa wivu wa kike..
Watu mmejaa wivu wa kike..