Jaji Kiongozi aibipu Serikali.. tena.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Kiongozi aibipu Serikali.. tena.!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Naanza kumchunuku Jaji Kiongozi.. nimemfuatilia tangu alipoteuliwa na kwa namna fulani nimegundua kuwa haumi umi maneno na anasema kila anchomaanisha. Safari amenigusa kwenye jambo hili jingine la watuhumiwa kukaa rumande wakati "upelelezi unaendelea". Mara nyingi tumekuwa tukisikia haya pale watu wanakamatwa na kwa haraka wanafikishwa mahakamani halafu waendesha mashtaka wanadai kuwa mtuhumiwa asiachiliwe kwa sababu upelelezi unaendelea. Siyo hapo tu wakati mwingine mtu anaenda mahakamani kufuatilia kesi yake miaka nenda na kila ikitajwa wenye akili wetu wanatoa hoja iahirishwe kwa sababu upelelezi bado unaendelea.

  Pendekezo langu ni kuwa wakati umefika kuwa mtu akifikishwa mahakamani lazima iwe ni pale ambapo upelelezi umefikia mahali pa kukamilika ili kesi kuanza. Na zaidi ya yote kesi isiahirishwe zaidi ya mwaka kwa kusubiri "upelelezi". Mahakama lazima ianze kupima ushahidi uliopo kwenye discovery na kutoa agizo kama kesi iendelee kuliko mtindo huu wa kuwaacha prosecutors kuahirisha kesi kwa muda mrefu. Na ninaamini huu ndio msimamo wa Jaji Kiongozi.

  IPPMedia

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Fakhi Jundu ameonyesha kutoa huruma kwa watuhumiwa wanaosota muda mrefu wakiwa magezani, ambapo amewataka Mahakimu kuanza utaratibu wa kuwaachia huru washtakiwa waliokaa magerezani muda mrefu endapo upelelezi wa kesi zao unasuasua.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akiongea wakati akitoa tathimini ya ziara aliyoifanya ya kutembelea Mahakama za Mwanzo za Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Jundu alisema wakati umefika sasa kwa mahakimu wa Mahakama za ngazi zote kutumia busara kwa kuangalia uwezekano wa kuzifuta kesi zote zinzooneka mwenendo wake sio nzuri ili kupunguza mrundikano ndani ya magereza.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema, kuna watu wengi wanaendelea kukaa magerezani zaidi ya miaka mitano, ambapo ukichunguza kwa makini utabaini wanashindwa kuhukumiwa kutokana na waendesha Mashtaka kutomaliza upelelezi wa kesi zao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]"Nimetembelea ndani ya magereza nimegundua watu wengi wanaendelea kukaa magerezani kutokana na upelelezi wa kesi zao kutokamilika, huu sio utaratibu wa kutenda haki, huyu mtu atakaa gerezani kwa miaka mingapi ili upelelezi ukamilike?" alihoji Jaji Jundu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]"Kwa maana hiyo Mahakimu wanatakiwa kutokubaliana na utaratibu huu, waanze kutumia busara kwa kuwaachia huru washtakiwa hawa ili wakikamilisha upelelezi wao wawakamate tena ili wajibu kesi zao," alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akifafanua Jaji Kiongozi alisema, Mahakamu wana uwezo wa kutumia kifungu cha 225 cha makosa ya jinai, ambapo kinaeleza mtuhumiwa anaweza kuachiwa huru kama kosa lake halikuwa na ushahidi wa kutosha lakini anaweza kukamatwa tena kwa kosa hilo hilo endapo ushahidi utapatikana.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Sambamba na hilo, alisema amewaagiza Mahakimu wa ngazi za Wilaya na Mahakimu wakazi wa Mkoa kutembelea magereza mbalimbali kwa ajili ya kwenda kuzungumza na wafungwa wote ambao wameonekana kufungwa kimakosa au kupewa adhabu kubwa kulingana na kosa alilofanya.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema amechukua hatua hiyo baada ya kumkuta mwanamke mmoja katika gereza la Bukoba akiwa amefungwa kutokana na kosa la kutolipa pesa alizokopeshwa, lakini kutokana na sababu zisizoeleweka alifunguliwa kesi ya jinai na kufungwa miaka mitano na kibaya zaidi wakati huo alikuwa na hali ya ujauzito.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]"Nashukuru yule mama kajifungua akiwa ndani ya gereza, lakini hakutakiwa kufungwa kifungo kama kile kwa kuwa hakutakiwa kushtakiwa kwa kosa la jinai, alitakiwa kuwa na kesi ya madai ingawa hakimu na mwendesha mashtaka kwa namna wanavyoelewa wao walifanya hivyo," alisema jaji Jundu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika ziara yake aliyoifanya katika Wilaya za Bagamoyo, Mkuranga na Kibaha, Jaji Jundu aliweza kushuhudia Mahakama za Kimanzichana na Kibaha zikiwa katika hali mbaya na kuwaomba Halmashauri za Wilaya wakishirikiana na wananchi kusaidia kujenga upya Mahakama ili huduma ziweze kutolewa katika hali bora.[/FONT]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Too bad!

  Shida ni kwamba process nzima ya kumkamata mtuhumiwa na kumfungulia mashitaka, na hatimaye kumweka ndani imeoza!..
  Imepenyezewa rupia kubwa mno kiasi inawaumiza wengi sana...hopeful huyu mtu ataleta mabadiliko!
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tuombe Mungu yafanyike kwa vitendo
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,548
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  Huo ndio utawala wa haki na sheria. Ila wataweza kuufanikisha?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  nadhani mahakama ianze kutumia hiyo sheria na kuwafungulia watu.. ili serikakli iamke.. na kuachana na hizi dana dana.. si unaona hata walijaribu kutumia kwenye kesi ya mgombea binafsi?
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwanakiji kwenye status - Badili isomeke 'Unafurahia uongozi wa Mahakama". Nafikiri inafit in
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,548
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  Imeshaamshwa na mgombea binafsi. Hata hili la kuwaachia watu kama ushahidi hakuna nalo twaweza sikia mpaka referendum iitishwe.
  Mahakama inaanza kuonyesha uhai kama nayo ni muhimili wa tatu wa katiba ya nchi. Na nafikiri ndio maana halisi ya kuwa na mahakama. Sio kila kitu kikamilishwe na serikali tu.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160

  mimi naungana na wewe katika mtizamo huo, kuwa lazima Police na waendesha mashitaka wakamilishe upelelezi kabla hawajamkamata muhalifu, hasa hawa ambao wametenda makosa ambayo hayawafanyi polisi kuhisi moja kwa moja kuwa huyu ndo muhusika,
  chukulia kesi za wahujumu Uchumi, kesi za EPA, Kesi za wezi katika majengo Pacha.
  hainiingii akilini eti mpaka mtuhumiwa anakamatwa na kupelekwa mahakamani upelelezi unakua haujakamilika,
  waangalie hawa kina Maranda, Liyumba na wengineo, serikali ilipaswa kujilidhisha na upelelezi wake kuwa hawa ni wahusika kabla ya kuwakamata kisha kuendesha upelelezi.
  hii itapunguza watu wengi kusota ndani bila sababu.
   
 9. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  M.M sheria ipo lakini haifuatiliwi kabisa na hii inachangiwa sana na watu wa mahakama wenyewe wakiwemo baadhi ya majaji na mahakimu, kwa mfano sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act) katika kifungu cha 226(1) inaitaka mahakama kufuta mashtaka na kumwachia huru mshtakiwa iwapo mlalamikaji atashindwa kujitokeza mahakamani siku shauri hilo litakapokuwa limetajwa lakini kwa experience yangu ya mahakama za Tanzania mara nyingi unakuta upande wa Jamhuri (washtaki) kila mara wanashindwa kuleta mashahidi lakini hakimu badala ya kutumia kifungu hicho cha sheria anatoa ahirisho la kesi kila mara bila kujali jinsi watuhumiwa wanavyosota mahabusu.,kwa hiyo pamoja na kuilaumu serikali, ni lazima mahakama nayo ijikosoe kwani wao wakiamua kusimamia sheria hizi hadithi tutazisahau.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ni maoni mazuri tatizo ni political will.It seems kuna wanaofaidika ni hii system ndio maana wanaona sawa tu...
   
 11. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  yeah, kama ni hivyo hata mie namchunuku, safi sana jaji, kweli kuna watu wapo ndani muda mrefu nenda rudi nenda rudi,kila siku waendesha mashitaka wanasema uchunguzi bado unaendela.sawa kwa wiki hata mwezi kuchunguza, lakini si miaka jamani. haki itendeke sasa, JAJI NAKUPONGEZA SANA KWA KULIONA HILI
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Serikali inatakiwa kuheshimu mahakama na pia kama kuna watu wamehusika na mambo kama haya basi inapaswa kushitakiwa kama watu wengine vile Watanzania
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunampongeza Jaji lakini tutampongeza sana hayo aliyoyasema yakianza kutekelezwa tukiwaona wanaosota magerezani kwa miaka mingi wanaachiwa huru.

  Huu ni mwaka wa uchaguzi, haiyumkiniki watakaoachiwa huru kwa uamuzi huo wataishukuru Serikali ya CCM ...!
   
 14. K

  Kinnega Member

  #14
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Umeshukuru nini sasa Jaji?

  Huyu kiongozi anaweza kuwa na nia nzuri lakini kauli zake - ambazo ni kielelezo kizuri cha upeo wake - zinatia shaka. Katika nasaha hizo hizo alidai: "Adhabu zinachangia msongamano, sio kila siku kutoa vifungu, unao uhuru wa kutoa adhabu mbadala,"

  Anawaambia mahakimu na majaji wasifuate vipengele vya sheria kila siku tuuu, watumie busara-huru zao.

  Hakimu au jaji hana mamlaka ya busara-huru ambayo hajaitoa kwenye vipengele vinavyompa uhuru. Ndo maana ni lazima unukuu vipengele vinavyokubana. Aliyeua ni lazima utauawa kwa kitanzi, aliyenajisi mtoto, lazima apewe "mvua thelathini," kama alivyotamka Rais leo kwenye Siku ya Wanawake, Tabora.

  Jaji Kiongozi Jundu anawaambia mahakimu wasifate vipengele kila siku!
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Safi sana,kumbe taratibu tunaanza kuwapata wachapa kazi.Ila nashangaa wanasheria wetu,yaani hicho kifungu cha sheria hawakukiona?
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,961
  Likes Received: 9,612
  Trophy Points: 280
  When you think about it, kumuweka mtu jela kwa sababu tu "upelelezi unanendelea" hakun tofauti na the oppressive process of "indefinite detention" ambayo nayo inabidi tuiondoe, kwa sababu haifuati due process.Both "indefinite detention" na "upelelezi unaendelea" have an indefinite nature.

  Now here is a scenario, suppose someone commits a crime whose maximum sentence is 3 years, and the investigation takes 5 years (while the accused is detained). At the conclusion of the investigation, will he be jailed for more time? Ridiculous.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,227
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Hakuna uhusiano wowote kati ya uchaguzi na tamko la jaji kiongozi. Ukweli ni kuwa mahabusu ziko overcongested kwa sababu za kujitakia tu na hii inakuwa burden kwa walipa kodi. Hela za kuhudumia mahabusu zinatakiwa ziende kwenye shughuli zingine za maendeleo.

  Ona kesi ya Bangi, mtu ananyimwa dhamana na kukaa mahabusu mwaka kwa nini kisa bangi mpaka iende kwa mkemia athibitishe. Ofisi ya mkemia ilikuwa moja tanzania nzima, angalau sasa hivi wameweka branches. Kwa nini kusiwe na kiwango ambacho mtu akikutwa nacho isiwe kosa la jinai, ila akizidisha kiasi hicho ndio iwe kosa.

  Alhamisi ilioyopita Wasomali na waethiopia 73 walikuwa wanaenda zao South Africa, polisi wakawakamata wakawapeleka mahakamani, wakakubali kosa hakimu akawapeleka rumande mpaka jumatatu kwa hukumu. Adhabu ni faini na kurudishwa kwao kwa gharama ya serikali. Was it necesary to do so? Kuwashika that is. Busara ilikuwa defender iwasindikize mpaka mpakani na waishie zae.Kuwaweka mahabusu ni kutumia vibaya hela ya walipa kodi.

  Wazururaji wanakamatwa na wananyimwa dhamana wanaenda mahabusu mwezi au hata miwili dhamana wananyimwa kwa faida ya nani huyo mtu ni afadhali akae nje kuliko akikaa rumande.

  Tukija kwenye adhabu ndio vichekesho, wakati wa mkoloni adhabu zilikuwa very reasonable miaka mitano ilikuwa ni stiff kweli adhabu nyingi zilikuwa miezi michache na wale walikuwa wabaripoti kwa Dc na kufyeka barabarani kufanya usafi na wengine wanapelekwa comworks kufanya kazi za ujenzi. Sasa hivi kila kosa kifungo miaka 15, 30 au maisha oneni vichekesho.

  Halafu ustaarabu wetu ni zero kabisa, kesi za kubambika ni nyingi kwelikweli na hivyo kuongeza mrundikano mahabusu, hii inaongezwa nguvu na inefficiency ya polisi.

  Pamoja na tamko la Jaji Kiongozi kuna haja kubwa ya kubadili Penal system yetu. Inabidi Penal system iwena manufaa kwa nchi na mahabusu na hata mfungwa.
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,227
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Ukikisoma kifungu chote hata wewe hutakitumia, mtu anaachiwa sasa hivi na anakamatwa mbele ya hakimu huyohuyo aliyemuachia kwani kifungu hakikatazi kufunguliwa kesi nyingine kama hiyo.

  Jaji kiongozi afanye utaratibu ili kifungu hicho kisiruhusu kushitakiwa tena mtu akiachiwa. Kama maika mitatu hujapata ushahidi utawezaje kuupata baadaye????
   
 19. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,757
  Likes Received: 1,534
  Trophy Points: 280
  Mkuu usulize wataweza, sema hivi; tutaweza?? Hili nijukumu letu sote tumia njia yoyote ile kupambana na wanaodhulumu haki za watu.
  Nchi hii ni yetu sote na jukumu la kuipigania ni letu sote.
   
 20. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 463
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi ilifikia hatua sikujua kumbe mahakama ni mojawapo ya mihimili kama katiba inavoonyesha, make sijawahi ckia mahakama imeishauri kitu serikali zaidi ya kulisikia bunge tu, kumbe nao wamo within those three organs? jamani hivi Tanzania Judicially system ni corrupt au nini, kwa nini wasiige hata mfumo wa mahakama wa Zambia, in that place judicial is judicial kweli, hata mkuu wa polisi anafungwa tena on the spot. cku moja nilishuhudia mkuu wa polisi wa zambia akifungwa six years kwa kosa la kununua sterling ya gari kumbe ilikuwa ya wizi, lakini Tanzania ni ndoto kuona hawa watu wakubwa wakichukuliwa sheria, lazima mahakama ifanye kazi independently, bila muingiliano na serikali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...