Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 24, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Tume ya Kufuatilia Kampuni za
  Madini Serikalini (TEITI), Jaji Marck Bomani

  MWENYEKITI wa Tume ya Kufuatilia Kampuni za Madini Serikalini (TEITI), Jaji Marck Bomani, amesema wageni wanazidi kuimaliza nchi kupitia sekta ya madini, yakiwa ni matokeo ya sheria mbovu. Jaji Bomani imeishauri Serikali kubadilisha haraka sheria zilizopo kuhusu sekta hiyo ili kuwawezesha wananchi kujua kila kinachopatikana kutokana na raslimali hiyo.

  Alisema uchimbaji wa madini utaendelea kuwanufaisha wageni kwa kuhamishia fedha na madini nchi za nje na kwamba hilo linatokana sheria zilizopo kuwapa mwanya.Jaji Bomani alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika warsha ya uelimishaji na uhamasishaji umma juu ya taarifa ya kwanza ya ulinganisho wa malipo na mapato kutoka kampuni za uchimbaji madini na gesi asili, katika mwaka wa fedha 2008/2009 iliyofanyika jijini Tanga

  Alisema ni jambo la kushangaza kuona Tanzania pekee ikitoa mwanya kwa wawekezaaji kuchimba madini na kuyasafirisha nje kwa ajili ya kuyauza.Jaji Bomani alisema mabaya zaidi makampuni hayo yametakiwa kulipa kodi baada ya kuondoa gharama zote za uendeshaji au uzalishaji. “Hakuna mfanyabiashara anayeweza kusema ukweli juu ya faida ganayoipata kutokana na kuchimba madini, haiwezekani Tanzania tuendelee kuwa masikini wakati madini yetu yanayotoka yangeweza kusukuma mbele maendeleo yetu,”alisema Bomani.

  Alisema katika taarifa ya awali imebainika kuwa uchambuzi uliofanyika kuna tofauti kubwa ya taakribani zaidi ya Sh 46 bilioni kati ya malipo yaliyodaiwa kulipwa na kampuni na fedha iliyopokelewa serikalini. Akiwasilisha mada ya mtizamo wa wadau na jamii juu ya ripoti ya kwanza ya TEITI na matarajio ya ripoti ya pili, mjumbe wa kamati hiyo, Askofu Stephen Munga alisema unahitajika uzalendo wa hali ya juu kwa viongozi waliopewa madaraka ya kuwaongoza wananchi.

  Alisema haiwezekani rasilimali ya nchi kuendelea kuvunwa na kutoroshwa nje ya nchi kijanja na kuwanufaisha wageni huku Watanzania wakiendelea kuwa masikini na kwamba ni lazima hatua za makusudi za kuinusuru nchi zichukuliwe.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #21
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Yeye akiwa mwenyekiti wa tume ya kufuatilia makampuni ya madini amechukua hatua gani badala ya kulalamika kama mimi ambaye sina bakora YA KUWACHAPA HAWA WIZI?
   
 3. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #22
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,378
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuache maneno maneno yasioisha,lets start doing,lets be practial,Bomani stop the bullshit mother****er,too much talking is harming the people.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #23
  May 27, 2017
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  The saga continues.
   
 5. BAKOI

  BAKOI JF-Expert Member

  #24
  May 27, 2017
  Joined: Jan 31, 2016
  Messages: 929
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 180
  Kwaya haya yanayotokea leo unatakiwa umuombe radhi Kama upo hai.
   
 6. BAKOI

  BAKOI JF-Expert Member

  #25
  May 27, 2017
  Joined: Jan 31, 2016
  Messages: 929
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 180
  Wewe sindounashangilia na kumsifia magufuli kuhusu haya ya mchanga halafu ulimpinga jaji bomani. We jamaa kweli n DS Sana na pia unajua kuwa waliotufikisha hapa n mkapa na Net group.
  Kweli ndo mana kuna jina wanakuita le mpumb*z
   
 7. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #26
  Mar 3, 2018
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 12,688
  Likes Received: 3,912
  Trophy Points: 280
  ......
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...