Serikali ya awamu ya sita, Imefeli Kusimamia Sekta ya Madini Chunya na Songwe

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
16,108
Reaction score
26,390
Kwa masikitiko makubwa, wananchi na wachimbaji wadogo wa Wilaya za Chunya na Songwe wameendelea kulalamikia hali mbaya ya utendaji ndani ya ofisi za Tume ya Madini, ambapo vitendo vya rushwa, upendeleo na matumizi mabaya ya madaraka vinaonekana kuwa sehemu ya kawaida ya utendaji wa kila siku.

Watumishi wengi wamekaa katika vituo hivyo kwa muda mrefu kupita kiasi, jambo lililosababisha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga mitandao ya maslahi binafsi, na kushindwa kabisa kuwatendea haki wachimbaji wadogo wanaotegemea sekta hii kwa maisha yao.

Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa huduma za utoaji wa leseni, usimamizi wa maeneo ya uchimbaji, pamoja na biashara ya dhahabu zimegeuka kuwa sehemu ya rushwa ya waziwazi.

Wachimbaji wadogo wananyanyaswa, wanacheleweshwa huduma makusudi, na wengine hulazimishwa kutoa fedha ili kupata haki zao za msingi. Serikali imeonekana kushindwa kusimamia watumishi wake wenye dhamana ya kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha sheria zinafuatwa kwa usawa.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba hata taasisi zilizopaswa kusimamia uadilifu na kupambana na rushwa zimeonekana kupoteza mwelekeo.

Wananchi wamekuwa wakitoa taarifa na malalamiko kwa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, lakini hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa.

Badala ya kulindwa, baadhi ya watoa taarifa wamekuwa wakisalitiwa siri zao na kujikuta wakitajwa kwa watuhumiwa, hali inayokatisha tamaa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola.

Aidha, yapo malalamiko makubwa kuwa baadhi ya watendaji kutoka vyombo vya usalama, wakiwemo TISS, polisi, uhamiaji pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya, wameacha majukumu yao ya msingi na badala yake kuingia moja kwa moja katika shughuli za uchimbaji na hata utoroshaji wa dhahabu.

Hali hii imegeuza maeneo ya Chunya na Songwe kuwa mazingira ambayo yanaonekana kutawaliwa na mitandao ya kifisadi inayoihujumu serikali yenyewe na kuwakandamiza wananchi wa kawaida.

Wananchi wanaomba kwa dhati Serikali ya Tume ya Madini, pamoja na mamlaka zote husika, ichukue hatua za haraka na za wazi. Watumishi wote waliokaa katika ofisi hizo kwa zaidi ya miaka mitatu wahamishwe mara moja ili kuvunja mitandao ya rushwa na mazoea mabovu ya kazi.

Pia uchunguzi huru ufanyike kuhusu vitendo vya rushwa, utoroshaji wa madini, na matumizi mabaya ya madaraka vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika Wilaya za Chunya na Songwe.

Rasilimali za madini zinapaswa kuwa baraka kwa wananchi na taifa kwa ujumla, si chanzo cha mateso, dhuluma na ufisadi unaofanywa mbele ya macho ya serikali bila hatua kuchukuliwa.
 
Rasilimali za madini zinapaswa kuwa baraka kwa wananchi na taifa kwa ujumla, si chanzo cha mateso, dhuluma na ufisadi unaofanywa mbele ya macho ya serikali bila hatua kuchu

sio kwenye madini tu bali imefeli kwenye kila sekta
 
Kwani kuna serikali Tanzania?
 
Riziwani na kampuni ya Wamala Resources, kwenye kumiliki leseni kama zote wilaya ya chunya,! Same on you!
 
Back
Top Bottom