Jaji aliyetoa hukumu ya Lema ni nani haswa?

vyovyote vile majaj wote wanafanya kazi ya CCM kuanzia 45% mpka 100%! watanzania wote wenye akili tunajua hilo
 
Jamani mwenye uthibitisho na hili tetesi tunaomba afunguke zaidi kwani kwani kila unaeongea nae anakwambia ndio ni kweli,sasa mwenye uhakika na detail za kutosha tunaomba amwage hapa jamvini.

Let's assume kwamba ni kweli huyu jaji ndiye aliyemhukumu yule mbakaji mnayemwita Babu Seya, then what? Bila kujali huyu bwana amefunga watu wangapi au ametengua ubunge wa watu wangapi, bottomline hapa ni kwamba yeye aliridhika (rightly or wrongly) kwamba Lema alistahili kuvuliwa ubunge na recourse aliyonayo Lema au chama chake ni kukata rufaa.

Hizo habari za kuunga unga hazitasaidia kitu.
 
Uteuzi wa huyu mkuu wetu wa kaya usiutumie kama kigezo cha usmart wa mtu kimaadili na kiutendaji. Mara nyingi kama siyo mara zote huwa ni kinyume kabisa kabisa na hivyo unavyofikiria! Vigezo vyake vya uteuzi huwa anavifahamu na kuvibuni mwenyewe.
uteuzi wake mara nyingi hutegemea wanamtandao walio mwingiza madarakani.
 
Tatizo la Majajde wa Bongo wanajipendekeza kwa JK, ili awape fadhila wakistaafu. Unaona Agustino Ramadhani, Lubuva, Msumi, Mihayo. Angalia wale majudge ambao mitizamo yao ni maadili ya kazi zao tu hakuna siasa wapo wapi baada ya kustaafu?
 
Jopo
la majaji watatu hao ilikua ni mahakama ya rufaa,nafikiri mleta mada
alimaanisha hukumumu ya mahakama kuu,japo nako aliyetoa hukumu si huyu
jaji aliyemkomoa Lema,alikua ni jaji Thomas Mihayo

hukumu ya babu seya ilianzia mahakama ya kisutu. majaji wote hao hata jaji mihayo walisikiliza rufaa na kuzikataa
 
Ikithibitika kweli basi ntaamini kikwete na ikulu imeshinikiza uamuzi kesi ya lema
 
Tuanze kwanza Mujulizi ambaye ndiyo aliyeanza hii kesi alikuwa firm moja na Masha,na soon baada ya mkuu wa kaya kuingia magogoni alimteua Masha kuwa Naibu Waziri then akafuata Mujulizi kuteuliwa kuwa jaji.Uteuzi wa hawa watu wawili ilileta malalamiko mengi sana ikichukuliwa kuwa malipo ya deep green yalifanyika chini ya hii firm na wakati huo huo Riz alikuwa yupo kwenye hii firm.....connect the dot unaweza pata picha.


mujulizi ni mkuu wa chuo cha uongozi wa mahakama lushoto.Alafu jamaa ni kichwa sana ana msimamo thabiti.
 
Tusipoteze muda kutetea makosa yaliyotendeka...ukweli siku zote utabaki hivo kama ulivo...na nyeupe haiwezi kuwa nyeusi hata siku moja....mshaurini Lema kuwa siasa si ugomvi wala matusi, aache jazba ya kupayuka hovyo...amekua na tabia ya kupayuka hovyo na maneno yake hayana ukweli ila ya kijiweni zaidi na ndio haya yalio sababisha kuvuliwa ubunge...haya yaliandikwa na kurikodiwa wakati wa wa kampeni alikua kampeni zake zilitawaliwa na udhalilishaji na wanawake na mgombea wa CCM , ni kweli alimdhalilisha kwa sababu ya jinsia yake na dini yake...huu ni ukweli...kulaumu hukumu na hakimu haisaidii kitu jadili jee lugha ya lema wakati wa kampeni ilikuwa inavunja masharti ya sheria za uchaguzi ama la? hili ndio la kujadili ...
lugha yake na maneno yake hata baada ya kuwa mbunge yamekua tata chadema wanahitaji kumweka chini....wamfuze siasa za ustaarab na kuropoka hovyo sio sifa ya kiongozi bora na makini..kuchaguliwa na kuwa na sapport katika jimbo sio hoja...hata Hitler alikuwa na supoort ya karibu 90% ya Wa Germans...na maneno yake ya hovyo na msimamo ya kibabe iliitumbikiza dunia katika vita vikuu vya pili...na wajerumani kukumutwa na dunia nzima...na ndipo walipokuja kujua kujua ubaya wa Hitler na hotuba zake za hovyo...Uchochezi kuasi au kuchukia mtu kwa jinsia yake ama dini yake ndio iliyokua dhambi ya Hitler lakini pia ndio ngazi aliyotumia kujipandisha mpaka akawa Kiongozi wa Germany....
Jaji amefanya kazi yake kwa ushahidi na facts zilizo wazi.....wasifu wake hausaidii kitu...
We unautaka ili iweje si umuulize mwenyewe acha kusumbua watu
 
Kwanza, Alishamhukumu Ya Akina Lamwai akawafungia u advocacy akiwa bado magistrate kitu ambacho hakuwa na jurisdiction nacho, Pili ashatukanana na mtikila mahakamani kuwa mtikila aende milembe, ila most of it..kamfungia Lema kutocontest kuwa mbunge kitu amabcho hakuna act inayompa hiyo jurisdiction...he's BOLD..
 
Ni historia nzuri, ungeweka kwenye mtiririko unaofaa with full details nadhani ingevuta hisia za wengi wakachangia Mkuu.
 
Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi ya Uchaguzi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema amerejea katika kituo chake cha kazi.Kituo cha kazi cha Jaji Rwakibalila ni Sumbawanga.Alikuwepo Arusha kwa ajili ya kusikiliza kesi ya Lema tu.Hivi sasa yuko njiani kuelekea Mbeya na baadaye Sumbawanga.Jaji Kiongozi,Mh Fakil Jundu anatarajia kufanya ziara katika Mahakama Kuu-Sumbawanga juma hili.

Wakati huohuo,nimeelezwa kuwa hukumu ya kesi ya Lema imemalizwa kuchapwa jana na hivyo kutoa nafasi kwa upande wa Lema kuchukua nakala yao na kuendelea na taratibu nyinginezo zikiwemo za kukata rufaa.Stay tuned...
 
Lamwai alikuwa mwanasheria aliyebobea kipindi hicho na mwalimu wa sheria chuo kikuu (UDSM) alishindwaje kwa kesi ya kusingiziwa?
 
Kwanza, Alishamhukumu Ya Akina Lamwai akawafungia u advocacy akiwa bado magistrate kitu ambacho hakuwa na jurisdiction nacho, Pili ashatukanana na mtikila mahakamani kuwa mtikila aende milembe, ila most of it..kamfungia Lema kutocontest kuwa mbunge kitu amabcho hakuna act inayompa hiyo jurisdiction...he's BOLD..

ungefanya kautafiti kadogo kuongeza nyama kwenye kazi yako ingebeba maana lakini hapa ni kama unapingana na sheria iliyozaa hukumu kwamba Jaji hakupaswa kuwahukumu uliowataja bila kuanisha vipengere vya sheria vilivyokiukwa.
 
Back
Top Bottom