Jaji aagiza Mkurugenzi Ilala ashtakiwe kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji aagiza Mkurugenzi Ilala ashtakiwe kortini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 11, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  Jaji aagiza Mkurugenzi Ilala ashtakiwe kortini
  Friday, 10 December 2010 20:38

  James Magai

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeagiza Msimamizi wa Uchaguzi Ilala jijini Dar es salaam ashitakiwe katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Segerea wilayani Ilala. Kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, ilifunguliwa na Mpendazoe kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala Novemba 10 mwaka huu, akipinga matokeo uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, yaliyompa ushindi mgombea wa CCM, Dk Makongoro Mahanga.

  Awali kesi hiyo, ilikuwa na walalamikiwa wawili, wa kwanza akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Dk Mahanga mwenyewe, lakini jana, mahakama hiyo iliagiza msimamizi wa uchaguzi, ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala naye aunganishwe katika kesi hiyo. Akitoa agizo hilo jana, Jaji Profesa Ibrahim Juma wa mahakama hiyo, alisema kutokana na marekebisho ya Sheria mpya ya Uchaguzi ya mwaka 2010, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo husika ni lazima naye aunganishwe kwenye kesi za uchaguzi


  Kutokana na agizo hilo, Jaji Juma aliuagiza upande wa malalamikaji kufanya marekebisho katika hati ya malalamiko na kuiwasilisha mahakamani hapo kesho.
  Pia mahakama hiyo, imepanga upande wa walalamikiwa wanapaswa kujibu hoja hizo, Desemba 20, kabla ya kesi hiyo kutajwa mahakamani hapo tena Februari 3, mwakani.

  Mpendazoe analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi katika jimbo hilo, akidai kuwa taratibu na sheria za uchaguzi zilikiukwa. Mpendazoe alisema sheria zilikiukwa katika kukusanya, kuhesabu na kutangaza matokeo ya nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

  Kutokana na kasoro hizo, Mpendazoe aliiomba mahakama hiyo, itengue matokeo ya ushindi wa Dk Mahanga.

  Alisema endapo haiwezekani kurudiwa kwa uchaguzi huo, mahakaama iamuru atangazwe kuwa mshindi na mbunge wa jimbo hilo. Katika uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alimtangaza Dk Mahanga kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo la Segerea saa 8:46 usiku wa kuamkia Novemba 3, mwaka huu kwamba alipata kura 43,555 na Mpendazoe 38,150.
   
Loading...