Jack Pemba matatani

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imemkamata mfanyabiashara Jack Pemba kutokana na madai ya kujipatia pesa kwa udanganyifu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Jack anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilwa Road tangu Jumapili (Juzi) na alifunguliwa jalada namba CD/IR/3657/2009.

Habari za kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo zilitawala katika maeneo mbalimbali jijini kutokana na umaarufu wake hasa katika kumbi za starehe kutokana na tabia yake ya ‘kumwaga fedha’ kwa wanamuziki na wapambe wake.

358uesg.jpg

...Jack Pemba

Jana (Jumatatu) gazeti hili liliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova ambaye alikiri kukamatwa kwa Pemba.

Alisema amekamatwa kutokana na kutuhumiwa kujipatia zaidi ya shilingi milioni 344 kwa njia ya udanganyifu kupitia Benki ya Exim ya Uingereza.

“Pemba alifunguliwa kesi na kampuni moja ya Uingereza mwaka jana na alikuwa akitafutwa na polisi yeye na wenzake ambao bado wanasakwa,” alisema Kova.
 
huh! Kwa hiyo kakamatwa kwa mashitaka aliyofunguliwa na exim Uingereza au?
 
Kama kova amemkamata huyu bwana kwa sababu kaiingiza mkenge Exim bank ya huko Uk basi yatakuwa ni mambo ya interpol ambayo ni mambo ya kawaida. Pia Kova angefanya uchunguzi kabla ya kumkamata.

Kuna walakini kama huo uhusiano wa kuwakamata watuhumiwa kutokana na uhusiano wa kipolisi wa nchi na nchi basi nao polisi ya UK iwakamate waliokula hela za rada na kuwarudisha watuhumiwa wetu ili tuwashulikie.

Isije kuwa tuu ni ushabiki wa kisiasa alionao Kova kwani nani asiye mjua kova kwa kufanya kazi kama kibaraka wa siasa?
 
Jamaa ni mcharuko mbaya, longtime alikuwa na tabi ya kitapeli ila sisi wabongo hupenda kuwakumbatia wenye hela hata kama ni hela chafu, lazima anyee debe na hao wanamuziki waendelee kumuimba tu.Safi sana interpol.
 
Kuna walakini kama huo uhusiano wa kuwakamata watuhumiwa kutokana na uhusiano wa kipolisi wa nchi na nchi basi nao polisi ya UK iwakamate waliokula hela za rada na kuwarudisha watuhumiwa wetu ili tuwashulikie. Isije kuwa tuu ni ushabiki wa kisiasa alionao Kova kwani nani asiye mjua kova kwa kufanya kazi kama kibaraka wa siasa?

Huenda Pemba hajawahi kukichangia chama chetu kitukufu..

NB: Ktk mafioso system hii inaitwa 'protection funds'..

Close call.
 
Huenda Pemba hajawahi kukichangia chama chetu kitukufu..

NB: Ktk mafioso system hii inaitwa 'protection funds'..

Close call.

Hajawahi - I gather kwamba walimu-approach kuchangia akatoa nje na matokeo yake ni hayo
 
Hawa jamaa athee kweli puppets on the strings JP katoka UK kama hiyo benki ilikua na ushahidi what stopped them from prosecuting whilst he was in UK. Hii ndio wazungu wanaita africans are bu*t skin, wenyewe kwa wenyewe tuna umana. Leave the dude alone ajaibia Tz, so whats the fuc*en problem. Umaskini wa mawazo bana.

Kuna mijambazi inaua kila siku mnashindwa kuikamata embu hawa masiwa waache roho za kimaskini. Kuna mijizi kedekede ya serikali ambayo inaitia taifa hasara na bado ipo loose.
 
he he,kova anaona wivu jamaa anawatip waimba muziki tuu,naona anamkumbusha kama na yeye kova ana njaa anataka mgao.
 
DUH..R.I.P huko KILWA ROAD..tuhuma tu hzo mzee Kiasi kikubwa hicho cha hela kwa Polisi wetu mzee lazima wale 2/3 hata kama zimeisha!.
 
kesi za Fraud ni ngumu na mara chache sana washutumiwa hufungwa, otherwise labda hakuwa mtaalamu na aliingizwa mkenge na Wapopo kwa wizi kama huo wa mamilioni ya fedha ni lazima watu wa bank washirikishwe, ni kama issue ya EPA bongo
 
Hawa jamaa athee kweli puppets on the strings JP katoka UK kama hiyo benki ilikua na ushahidi what stopped them from prosecuting whilst he was in UK. Hii ndio wazungu wanaita africans are bu*t skin, wenyewe kwa wenyewe tuna umana. Leave the dude alone ajaibia Tz, so whats the fuc*en problem. Umaskini wa mawazo bana.

Kuna mijambazi inaua kila siku mnashindwa kuikamata embu hawa masiwa waache roho za kimaskini. Kuna mijizi kedekede ya serikali ambayo inaitia taifa hasara na bado ipo loose.

Juma

Acha sheria ichukue mkondo wake..kwa sababu waizi fulani hawajakamatwa sio kwamba basi tuwasamehe wote ati. BTW hii ni chanzo tu cha mchakato wa kuhakikisha haki inatendeka.
 
hawa jamaa athee kweli puppets on the strings jp katoka uk kama hiyo benki ilikua na ushahidi what stopped them from prosecuting whilst he was in uk. Hii ndio wazungu wanaita africans are bu*t skin, wenyewe kwa wenyewe tuna umana. Leave the dude alone ajaibia tz, so whats the fuc*en problem. Umaskini wa mawazo bana.

Kuna mijambazi inaua kila siku mnashindwa kuikamata embu hawa masiwa waache roho za kimaskini. Kuna mijizi kedekede ya serikali ambayo inaitia taifa hasara na bado ipo loose.

kaka shida mtu akiona hela yake ya wizi, hata kama kaiba huko ulaya au Amerika ambako wathungu washatuibia sana utajiri wetu, ya nini akirejea nyumbani ageuke na kuanza kutanua hovyo hovyo kiasi cha kusababisha macho ya dola kumtilia wasiwasi..??. Hapa hajaelezwa ni vipi hiyo fraud imefanyika na imebainika lini kiasi cha kuweza kujua kwa nini aligongewa "Exit" kurejea Bongo tokea UK.
 
Kama kova amemkamata huyu bwana kwa sababu kaiingiza mkenge Exim bank ya huko Uk basi yatakuwa ni mambo ya interpol ambayo ni mambo ya kawaida. Pia Kova angefanya uchunguzi kabla ya kumkamata.

Kuna walakini kama huo uhusiano wa kuwakamata watuhumiwa kutokana na uhusiano wa kipolisi wa nchi na nchi basi nao polisi ya UK iwakamate waliokula hela za rada na kuwarudisha watuhumiwa wetu ili tuwashulikie.

Isije kuwa tuu ni ushabiki wa kisiasa alionao Kova kwani nani asiye mjua kova kwa kufanya kazi kama kibaraka wa siasa?

Na wewe ni mmoja wapo wa Beneficiaries nini? Mbona unaongea kinyonge na kumtetea mtu aliyekamatwa kwa kutuhumiwa! Subiri system iamue mambo, wewe kama mimi, uhitaji kulalamika kwa namna hii ya HURUMA! Nakua kama nakuona hivi
 
uyu jack pemba ni nani hasa, na mimi naomba wasifu wake kwa wale wanaomfahamu..ana campuni ipi, anafanya biashara gani vile?...
 
Ukiona watu wanamwaga fedha ovyo bila ya uchungu ujue hizo ni za wizi au za kitapeli. Zile za kuchuma kwa jasho lako mwenyewe kwa kweli huwa ni chungu sana na hutazitumia ovyo ovyo.

Kama amefanya utapeli na akamatwe tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom