Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,538
- 3,826
Kuwa na degree au kuwa na PhD haimaanishi kuwa unaweza au unafahamu kila kitu. Kila siku kuwa mtu wa kujifunza kutoka kwa watu wanaokuzunguka kila siku.
Katika maisha yako ya kila siku hasa kwa jamii inayokuzunguka kuna elimu zaidi ya iyo degree yako au PhD yako. Usipende kujiona kama muweza wa kila jambo na kuwadharau wasiokwenda shule au walio na elimu ndogo zaidi yako.
Hivi unajua kuwa bila hao watu wenye elimu ndogo au wasiokwenda shule wewe usingekuwepo? Ulishawai kufikilia kuwa katika biashara yako kila siku inawategemea hao watu wasio na elimu na wenye elimu ndogo kama wateja wako, na ata kama ufanyi biashara bado watu hao ni muhimu katika maisha yako ya kila siku.
#fikichaAkiloYako
#timizandotozako
#jifunzekutokatatamaa