WAGOMBEA 17 WA CCM 1995
Mwaka 1995, walijitokeza wagombea wanaccm 17 kuomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya ccm. Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao 3 ie CC, NEC na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni CC. Mwenyekiti wa kikao alikua Mwenyekiti wa ccm A.H. Mwinyi. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alialikwa ili asaidie shughuli hii pevu.
Nyerere bila kumungunya maneno wala kupepesa macho, kama ilivyo kawaida yake kwenye masuala ya kitaifa alisema wazi kuwa MALECELA NA LOWASA HAWAFAI KABISA KUONGOZA NCHI HII. Nyerere alisema Malecela ana madhambi mengi na ameyaweka wazi katika kitabu ambacho pia alielezea udhaifu wa Kolimba. Kuhusu Lowasa, Nyerere alisema baada ya kua amepewa file confidential na watu wa usalama-"Huyu kijana wa miaka 42 tu amepata wapi utajiri wote huu?? S. Sita ambaye alikua Compaign Manager wa J. Kikwete na E. Lowasa kwa pamoja aliinuka na kumtetea sana Lowasa hadi kufikia kusema hizo ni tuhuma tu hazijathibitishwa na pia kua Lowasa ana mvuto mkubwa kwa wananchi na anakubalika sana.
Baada ya kusikia "upuuzi" huu Nyerere hakusubiri Sita amalize hadithi zake alimkatisha na kumwambia "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa, na kama ni mzuri kanywe nae chai". Wana-CC wengine wajitahidi kuwatetea Lowasa na Malecela kwa nguvu kubwa maana tayari walikua na makundi. Kutokana na hilo Nyerere alisema "Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje??". Kutokana na tishio hilo pamoja na nguvu kubwa aliyokua nayo A. Mrema wa Nccr ilibidi wana-CC hao kunywea hivyo Malecela na Lowasa wakachinjiwa baharini. Majina 5 yakapelekwa NEC na hatimaye majina ma3 yakapelekwa Mkutano Mkuu (Mkapa, Kikwete na Msuya) na mwishowe Mkapa akachaguliwa kuwa mgombea wa CCM
UCHAGUZI WA 2005
Kama ilivyokawaida kikao cha kwanza cha kuchuja wagombea kilikua ni CC. Malecela, kwa mshangao wa wengi, naye pia aligombea na wakati huo alikua M/Mwenyekiti wa CCM. Kwa kutumia wadhifa huo, toka 1995 Malecela alizunguka nchi nzima na kufajhamiana na wajumbe wote wa vikao vyote muhimu hivyo wkt wa kuchukua na kujaza na kurudisha fomu yeye alikua wa kwanza kumaliza mchakato wote huo na takriban asilimia 85 ya wajumbe wa vikao vyote 3 walikua wanamkubali na Malecela mwenyewe na wapambe wake waliamini baada ya kifo cha Nyerere kusingekua na kikwazo tena. Mkapa,Mwenyekiti wa CCM alifungua kikao na kuwaonyesha alichosema Nyerere kuhusu Malecela. Wana-CC wengi walikumjegea hoja Malecela lakini hoja za msingi zilizojengwa na Mkapa na wengine kua chama kitashindwa kuonekana kinamuenzi Nyerere na pia itakua vigumu kumnadi MALECELA ambaye tayari alikua amechafuka. Hatimaye, kwa mara nyingine, Malecela akachinjiwa baharini. J. Kikwete ndiye akapererusha bendera ya ccm.
HARAKATI ZA E. LOWASA UCHAGUZI 2015
Licha ya Nyerere kusema Lowasa hafai na kwamba ni kijana mdogo mwenye utajiri mkubwa na mwenye uchu mkubwa wa kwenda Ikulu, Lowasa baada ya kujiuzuru uPM alianza jitihada kubwa mno za kutaka kuwa Rais wa TZ 2015. Katika jitihada hizo amefanya mambo mengi miongoni mwake ikiwa ni pamoja na 1. Kuweka mtandao mkubwa wa wapambe wake wakiwamo mawaziri lukuki waliomo kwenye Barza la mawaziri la sasa 2. Kuhakikisha kundi lake linaingiza watu wengi kwenye NEC 3. Kuhakikisha waCC na Wajumbe wengi wa mkutano mkuu nao wanakua upande wake 4. kugawa vyakula, kuku, ngombe mbuzi kama hana akili nzuri kwa watu na taasiis mbali mbali 5. kugawa na kuchangisha fedha kwa dini zote mbili ili asionekane mbaguzi 6. kutumia vyombo vya habari kumsafisha 6. kutumia wabunge mbalimbali kumsafisha na ikiwezekana mjadala wa Richmonduli urudishwe upya na pia amekua akiwalipa wetu wengi na vijana wake ili kumsafisha katika mitansao mingi ya jamii.
Lowasa amedaiwa kuwa ni fisadi mkubwa na kumekua na tuhumu kibao dhidi yake kama ifuatavyo
1. Amedaiwa kua ni mla rushwa mkubwa na kamwe hana moral authority kukemea rushwa
2. Amedaiwa alipokua AICC alitumia vibaya madaraka yake
3. Amedaiwa kua ni mgonjwa hivyo hawezi mikikimikiki ya uchaguzi na ya kuongoza nchi
4. Amedaiwa kutumia hela nyingi sana kuwaweka watu wake NEC hadi hela zilikua zikigawiwa vyooni, kwenye vibanda vya simu na kwa mama ntilie na vocha za simu
5. Anadaiwa akiwa Waziri wa Ardhi alitumia vibaya madaraka na kuuza viwanja hovyo hasa open spaces kwa wahindi
6. Ingawa alikua mtumishi wa serikali ana mahoteli mengi, majumba pamoja na jumba la ubalozi wa Africa Kusini.
7. Richmonduli
8. Ana utitiri wa vitega uchumi eg Alpha
9. Ni shareholder wa Vodacom analipwa 900M KWA MWEZI
10. Amekorofishana na swahiba wake JK
Hizi ni tuhuma ambazo ameshindwa kabisa kuzikanusha
MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2)Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.
Hivyo wote mnaotumia JIKI kumsafisha Lowasa na njaa zenu mjue fika mgombea wenu hauziki. Hivi CCM ikimteua Lowasa kuwa mgombea je itakua imetoa picha gani kwa wanachama wake? Je wanachama wataweza tena kusema mbele ya watu kua CCM ni chama CHA WAFANYAKZANI NA WANYONGE??
Mtu pekee ambae angeweza kumsafisha Lowasa ni Nyerere tu vinginevyo sioni mwingine. Tukumbuke kua nchi imegundua uwepo wa Uranium, gas na oil hivyo kumpa mtu mwenye hurka na uroho wa mali kama Lowasa ni kuipeleka nchi pabaya.
Ni imani yangu watu wengi watachangia na kutoa maoni yao ili nchi ipate Rais anayefaa na sio mtu anayetumia hela kwa namna ambayo haijapata kutokea hapa nchini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!