J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by galiya, Oct 30, 2012.

 1. g

  galiya JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WAGOMBEA 17 WA CCM 1995

  Mwaka 1995, walijitokeza wagombea wanaccm 17 kuomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya ccm. Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao 3 ie CC, NEC na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni CC. Mwenyekiti wa kikao alikua Mwenyekiti wa ccm A.H. Mwinyi. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alialikwa ili asaidie shughuli hii pevu.

  Nyerere bila kumungunya maneno wala kupepesa macho, kama ilivyo kawaida yake kwenye masuala ya kitaifa alisema wazi kuwa MALECELA NA LOWASA HAWAFAI KABISA KUONGOZA NCHI HII. Nyerere alisema Malecela ana madhambi mengi na ameyaweka wazi katika kitabu ambacho pia alielezea udhaifu wa Kolimba. Kuhusu Lowasa, Nyerere alisema baada ya kua amepewa file confidential na watu wa usalama-"Huyu kijana wa miaka 42 tu amepata wapi utajiri wote huu?? S. Sita ambaye alikua Compaign Manager wa J. Kikwete na E. Lowasa kwa pamoja aliinuka na kumtetea sana Lowasa hadi kufikia kusema hizo ni tuhuma tu hazijathibitishwa na pia kua Lowasa ana mvuto mkubwa kwa wananchi na anakubalika sana.

  Baada ya kusikia "upuuzi" huu Nyerere hakusubiri Sita amalize hadithi zake alimkatisha na kumwambia "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa, na kama ni mzuri kanywe nae chai". Wana-CC wengine wajitahidi kuwatetea Lowasa na Malecela kwa nguvu kubwa maana tayari walikua na makundi. Kutokana na hilo Nyerere alisema "Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje??". Kutokana na tishio hilo pamoja na nguvu kubwa aliyokua nayo A. Mrema wa Nccr ilibidi wana-CC hao kunywea hivyo Malecela na Lowasa wakachinjiwa baharini. Majina 5 yakapelekwa NEC na hatimaye majina ma3 yakapelekwa Mkutano Mkuu (Mkapa, Kikwete na Msuya) na mwishowe Mkapa akachaguliwa kuwa mgombea wa CCM

  UCHAGUZI WA 2005

  Kama ilivyokawaida kikao cha kwanza cha kuchuja wagombea kilikua ni CC. Malecela, kwa mshangao wa wengi, naye pia aligombea na wakati huo alikua M/Mwenyekiti wa CCM. Kwa kutumia wadhifa huo, toka 1995 Malecela alizunguka nchi nzima na kufajhamiana na wajumbe wote wa vikao vyote muhimu hivyo wkt wa kuchukua na kujaza na kurudisha fomu yeye alikua wa kwanza kumaliza mchakato wote huo na takriban asilimia 85 ya wajumbe wa vikao vyote 3 walikua wanamkubali na Malecela mwenyewe na wapambe wake waliamini baada ya kifo cha Nyerere kusingekua na kikwazo tena. Mkapa,Mwenyekiti wa CCM alifungua kikao na kuwaonyesha alichosema Nyerere kuhusu Malecela. Wana-CC wengi walikumjegea hoja Malecela lakini hoja za msingi zilizojengwa na Mkapa na wengine kua chama kitashindwa kuonekana kinamuenzi Nyerere na pia itakua vigumu kumnadi MALECELA ambaye tayari alikua amechafuka. Hatimaye, kwa mara nyingine, Malecela akachinjiwa baharini. J. Kikwete ndiye akapererusha bendera ya ccm.

  HARAKATI ZA E. LOWASA UCHAGUZI 2015

  Licha ya Nyerere kusema Lowasa hafai na kwamba ni kijana mdogo mwenye utajiri mkubwa na mwenye uchu mkubwa wa kwenda Ikulu, Lowasa baada ya kujiuzuru uPM alianza jitihada kubwa mno za kutaka kuwa Rais wa TZ 2015. Katika jitihada hizo amefanya mambo mengi miongoni mwake ikiwa ni pamoja na 1. Kuweka mtandao mkubwa wa wapambe wake wakiwamo mawaziri lukuki waliomo kwenye Barza la mawaziri la sasa 2. Kuhakikisha kundi lake linaingiza watu wengi kwenye NEC 3. Kuhakikisha waCC na Wajumbe wengi wa mkutano mkuu nao wanakua upande wake 4. kugawa vyakula, kuku, ngombe mbuzi kama hana akili nzuri kwa watu na taasiis mbali mbali 5. kugawa na kuchangisha fedha kwa dini zote mbili ili asionekane mbaguzi 6. kutumia vyombo vya habari kumsafisha 6. kutumia wabunge mbalimbali kumsafisha na ikiwezekana mjadala wa Richmonduli urudishwe upya na pia amekua akiwalipa wetu wengi na vijana wake ili kumsafisha katika mitansao mingi ya jamii.

  Lowasa amedaiwa kuwa ni fisadi mkubwa na kumekua na tuhumu kibao dhidi yake kama ifuatavyo
  1. Amedaiwa kua ni mla rushwa mkubwa na kamwe hana moral authority kukemea rushwa
  2. Amedaiwa alipokua AICC alitumia vibaya madaraka yake
  3. Amedaiwa kua ni mgonjwa hivyo hawezi mikikimikiki ya uchaguzi na ya kuongoza nchi
  4. Amedaiwa kutumia hela nyingi sana kuwaweka watu wake NEC hadi hela zilikua zikigawiwa vyooni, kwenye vibanda vya simu na kwa mama ntilie na vocha za simu
  5. Anadaiwa akiwa Waziri wa Ardhi alitumia vibaya madaraka na kuuza viwanja hovyo hasa open spaces kwa wahindi
  6. Ingawa alikua mtumishi wa serikali ana mahoteli mengi, majumba pamoja na jumba la ubalozi wa Africa Kusini.
  7. Richmonduli
  8. Ana utitiri wa vitega uchumi eg Alpha
  9. Ni shareholder wa Vodacom analipwa 900M KWA MWEZI
  10. Amekorofishana na swahiba wake JK

  Hizi ni tuhuma ambazo ameshindwa kabisa kuzikanusha


  MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
  Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2)Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
  1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
  2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
  3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
  4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.

  Hivyo wote mnaotumia JIKI kumsafisha Lowasa na njaa zenu mjue fika mgombea wenu hauziki. Hivi CCM ikimteua Lowasa kuwa mgombea je itakua imetoa picha gani kwa wanachama wake? Je wanachama wataweza tena kusema mbele ya watu kua CCM ni chama CHA WAFANYAKZANI NA WANYONGE??

  Mtu pekee ambae angeweza kumsafisha Lowasa ni Nyerere tu vinginevyo sioni mwingine. Tukumbuke kua nchi imegundua uwepo wa Uranium, gas na oil hivyo kumpa mtu mwenye hurka na uroho wa mali kama Lowasa ni kuipeleka nchi pabaya.

  Ni imani yangu watu wengi watachangia na kutoa maoni yao ili nchi ipate Rais anayefaa na sio mtu anayetumia hela kwa namna ambayo haijapata kutokea hapa nchini.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu galiya

  karibu sana JF, Nimeupenda sana uchambuzi wako...maana umeandika UKWELI tupu.

  Unaonekana unaifahamu sana system yote ya Magamba, Hivi JK alipitia kwa mkakati gani 2005, kwanini Lowassa asipitie njia ya mtangulizi wake?

  Ila tafadhali andiko lako lisiwe ni baada ya kutoshwa ama kuzidiwa nguvu za rushwa UVIVUCCM,

  Naamini umesukuwa na uzalendo na si hasira juu ya Lowassa maana kuna kamanda Pasco na Ritz, hamtaelewana.
   
 3. g

  galiya JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  POMPO,

  Nashukuru mkuu. Pamoja sana. Nakuhakikishia mimi natumwa na UZALENDO. Mambo ya UVCCM hayanihusu.

  Umeuliza ni kwanini JK aliweza kupita 2005 na ni vipi EL atashindwa kupita. Kama nilivyosema katika utangulizi wangu ni kua Nyerere alimkubali JK kwani hakuna na kashfa yoyote. Nyerere alimkataa EL kwakua alikua ananuka rushwa ingawa alikua bado kijana mdogo. NASISITIZA KAMATI KUU YA CCM 2015 haitakubali kumpitishwa EL.

  Wale wote mnaoganga njaa gangeni jaa zenu lakini mjue kua at the end of the day EL atachinjiwa baharini. Habari ndio hiyo!
   
 4. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Duh Mkuu Hapo Umenena Lowassa hafai alivyonavyo vinamtosha sidhani kama ana shida zaidi tu ya kuwa anataka kutuletea shida watanzania kama tunavyoletewa na huyu mkwer3 and his inner cycle yake
   
 5. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Hivi haya uliyoandika, wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wanayajua?
  Je, wako tayari kuziachia pesa watakazopewa kumpigia kura zote ili
  apeperushe bendera ya chama kwenye uchaguzi mkuu? Au Nyerere
  atarudi kuja kutishia kukihama chama? Ukweli, hadi sasa hakuna aliyeweza
  kumzuia Lowassa, CCM ijiandae kumeguka kama Kanu ya Kenya...
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  kuna watu wanahoji kwanini EL hastahili kuongoza nchi hii nadhani watakuwa wamekusoma mkuu
   
 7. g

  galiya JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  BISHOP HILUKA

  Umeuliza "Wajumbe wa mkutano Mkuu wako tayari kuziachia pesa"

  Labda tu nikueleweshe kua process ilivyo ni kwamba lazma kwanza Kamati kuu ikae inachuja majina matano na kuyapeleka NEC . NEC inayachuja na kuyapeleka Mkutano Mkuu majina 3. Sasa hoja yangu ni kua Lowasa jina lake haliwezi hata kufika NEC wachilia mbali mkutano mkuu. Pia umedai Nyerere hatakuwepo kutishia kurudisha kadi yake. But hata 2005 Nyrere hakuwepo bali Malecela aligombea na akapigwa chini maana MAWAAZO YA NYERERE 1995 NDIO DIRA NA NI PRECEDENT!!!
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama nyerere kweli alimkubali JK leo hii mwalimu angekua bado yuko hai hivi angesemaje kuhusu hali ya nchi hii JK alivyoifanya mtu ambae alikua anamuona anafaa? wazungu wanasema dont judge a book by its cover
   
 9. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Nafikiri wafuasi wako na kundi lako watakuelewa na kukupongeza kwa uliyoandika bila kuwa na ushahidi wowote. Nashangaa mbona hakufunguliwa kesi ya rushwa, kutumia vibaya madaraka, na huyo J. K. wako ambaye Mwalimu alimkubali kwamba hana doa mboa katuleta kwenye matatizo kiasi hiki. Mimi ni vigumu sana kukubaliana na mambo ya kusema Nyerere alisema, Nyerere hakuwa Mungu, mwenyewe alituletea umaskini wa kutisha mpaka tulipompata Mwinyi. Bora kumpata Rais mwenye pesa na maendeleo kuliko maskini atakayeanza kutafuta pesa akiupata urais atatupa shida sana huyo.
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu galiya hayo uliyoandia Pasco wa JF anayajua ?.Angalia asije kukutoboa macho inaelekea fedha za Laigwanani zimempumbaza sana kiasi amekuwa mtetezi mkubwa utadhani si mTanzania.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. g

  galiya JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NDETIRIMA

  Mkuu naheshimu mawazo yako. Ila we na mwenzako mmeuliza "Kama kweli Nyerere alimtaka J.K , je akifufuka atajiskiaje? Jibu ni simple. Je Nyerere atajiskiaje akiona Mkapa alianzisha kampuni akiwa Ikulu wakati Nyerere aliwahi kuuliza "Ikulu ni mahali patakatifu, kuna biashara gani pale?

  Hata hivyo Bw Nderitima ujue mtu anatoa mawazo yake hivyo yakiwa ni tofauti na yako usikimbilie kusema kundi na wafuasi wako watafurahia maoni yako. Una ushahidi gani kwamba nina kundi??? Watu kama wewe wakiingia madarakani wanakua MADIKTETA maana hawataki kabisa maoni tofauti! Mimi naongozwa na UZALENDO, kaka
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  -Jasiri anayeogopa mali zake?Kazi kweli...Urais labda wa Chama chake au taasisi nyingine!
   
 13. g

  galiya JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngongo

  Mkuu mwambie huyo Pasco aje atoe maoni yake au ajibu hoja. Nia yangu ni kuwa sisi GREAT THINKERS tujadili ili tuweze kumpata mtu ambae anastahili kuliongoza Taifa letu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu galiya, hivi inakuweje hawa viongozi wa chama wanahongwa na wankubali mpaka kwenye kwenye box la kura? Wanamjua mtu ni fisadi, hawezi kuongoza nchi, cha kushagaza hawa watu wanasimama na kusema anaweza. Yaani wanajitoa fahamu kabisa? Hii ni nguvu ya rushwa au nguvu ya ujinga au nguvu ya ubinafsi? Mimi sielewi.

  Niliwahi kuwaambia dungu zangu kijijini kwamba mtu akikupa rushwa usikatae kwani atakujua kwamba humpendi na hiyo inaweza kupelekea chuki baina yake na wewe. Wewe chukua mshiko, munyime kura. Period. Hapo atajifunza kitu. Cha kushangaza dungu zangu wakipewa rushwa, utafikiri wamewekewa GPRS miilini mwao kwamba hata watakachokifanya kwenye box la kura, jamaa atawajua tu. Tanzania lazima ibardilike, bila hivi tutapiga hatua kubwa sana kwa kuwa masikini makubwa duniani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nyerere hakumkubali JK, in fact alimtumia ujumbe Mkapa kuwa mtu yeyote aliyeshindana nae kupata urais amtupe mbali, kwani nia ya kuutaka urais bado itakuwepo. Mkapa akamtupa JK Wizara ya Nje, akijua atakua harmless, kumbe kasahau mtandao ulikuwa umeshaanza kazi, na pia kuingia kwa wakina Rostam Aziz kwenye kundi hilo.
   
 16. Niambieni

  Niambieni JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Watanzania tuna amini ya kuwa maneno matupu hayavunji mfupa. Hivyo basi tutazungumza sana na mwisho wa siku yaani 2015 asiyetakiwa atachukua madaraka kiulaini bila ya jasho.

  Ni kweli kuna vithibitisho ya kuwa Lowasa ana mapungufu mengi sana, lakini ni lazima atachukua madaraka, penda msipende. Na zaidi hakuna nguvu yoyote itakayo mzuia.

  Bali tufahamu ya kuwa, kura za uchaguzi kwa nchi kama zetu hizi, huwa hazimfanyi mtu kushinda. Ni kweli Chadema yaweza kupata kura mia kwa mia, lakini zitakazo tangazwa ni tofauti na ukweli.

  Angalia watu wanavyojitokeza kwenye mikutano ya CHADEMA ni wengi sana, na mikutano ya CCM ni tofauti sana. Matokeo yanayotangazwa hata juzi na jana ni CCM imeshinda asilimia 75. hivyo maneno matupu ya CHADEMA au Mlala hoi hayawezi kufunja mfupa.

  Ni wazi ya kuwa Mwaka 2015 Lowasa anachukua nchi, na pesa wanazozitoa wamiliki wa migodi na wawekezaji wengine ili ashinde, tutazilipa sisi wenyewe baada ya uchaguzi.

  UKITAKA HAKI ISHINDE 2015 PIGA MAGOTI UINGIE MAOMBINI NA PIA FUNGA (KWA MAISHA YA KIROHO MANENO UUMBA). ACHA UBISHI KWANI HUJUI BIBLIA YAKO INASEMAJE KUHUSU SIKU ZA MWISHO?

  SHETANI YUPO KAZINI. TUKESHENI KWA MAOMBI WAPENDWA.
   
 17. m

  majebere JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Nyerere alimchagua Mkapa, na tumeona ujambazi alio ufanya.kwani nyerere ni mungu bana, yeye mwenyewe alifanya uharo mgapi wakati wa utawala wake?
   
 18. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  hivi nyerere alikuwa ni Mungu ? kwanza tunataka uchunguzi wa kifo cha SOKOINE ufanyike upya tujue ukweli uliofichwa miaka mingi.
   
 19. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Lowassa sawa na uamsho
   
 20. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mkuu Gallya!

  Sidhani kama Nyerere alimkubali J. K kwa kuwa alimwambia wazi kwamba yeye (J. K) alikuwa mtoto japokuwa alikuwa na umri wa miaka 45 na katiba inahitaji mgombea urais awe na umri usiopungua miaka 40. Hapo kulikuwa na haja ya kuutafakari "Utoto" alioumaanisha Mwalimu kwa j.k! Kuhusu hili la E. L kutopitishwa na CC mwaka 2015 nina mashaka! Kama CC, NEC na MKUTANO MKUU vitakuwa imejaa watu wake, watamkataje? Me Nadhani E. L ni unstoppable kwenye mbio zake za urais ndani ya chama chake!
   
Loading...