J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

kwanza wewe ni Muongo 1995 Lowasa ndiye alkuwa kampen meneja wa JK na makinda alkuwa msaidizi na ndiye pekee aliyewapokea airport dodoma JK na Lowasa walipoingia enzi hizo walkuwa wakiitwa Boys 2Men kutokana na kuelewana sana na kukubalika...pili Nyerere si Mungu so yale yalikuwa mawazo yake cz taarfa znazoitwa za kiintelijensia ndzo kila sku znatumika kuthbti watu threat na 2005 hiyo mbnu ilkuwa itumike kummaliza JK ila lowasa akaiwai akaitumia yeye kumbeba kikwete kwa sababu chaguo la mkapa lilikuwa salim ahmed salm na Sumaye...habari ndio hiyo so Nyerere si Mungu ni bnadamu alikuwa na mawzo yake mabaya na mazuri hakuwa malaika..
 
Tajiri anayeogopa mali zake ni huyo anayekulipa aliyejlmbkizia masheli na hoteli wakat hana kaz yenye kumuingizia pesa hiyo...fuatlia investment za lowasa zpo internationaly,,,si kariakoo na snza
 
hofu yenu ni baada ya kuona lowasa ameshashka chama muda wenu umefka..bado mtapelekwa ICU za kisiasa kashka kila kona...watoto wadogo wanapima ubavu kwa lowasa na siasa zao za maji taka na za kulalamika kwenye media kila sku...muda wa kuvuka daraja ndio atavuka daraja si sasa
 
UCHAGUZI WA 2005

Kama ilivyokawaida kikao cha kwanza cha kuchuja wagombea kilikua ni CC. Malecela, kwa mshangao wa wengi, naye pia aligombea na wakati huo alikua M/Mwenyekiti wa CCM. Kwa kutumia wadhifa huo, toka 1995 Malecela alizunguka nchi nzima na kufajhamiana na wajumbe wote wa vikao vyote muhimu hivyo wkt wa kuchukua na kujaza na kurudisha fomu yeye alikua wa kwanza kumaliza mchakato wote huo na takriban asilimia 85 ya wajumbe wa vikao vyote 3 walikua wanamkubali na Malecela mwenyewe na wapambe wake waliamini baada ya kifo cha Nyerere kusingekua na kikwazo tena. Mkapa,Mwenyekiti wa CCM alifungua kikao na kuwaonyesha alichosema Nyerere kuhusu Malecela. Wana-CC wengi walikumjegea hoja Malecela lakini hoja za msingi zilizojengwa na Mkapa na wengine kua chama kitashindwa kuonekana kinamuenzi Nyerere na pia itakua vigumu kumnadi MALECELA ambaye tayari alikua amechafuka. Hatimaye, kwa mara nyingine, Malecela akachinjiwa baharini. J. Kikwete ndiye akapererusha bendera ya ccm.

MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2) Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.

Kiongozi,

1. Unasahau kwamba Mkapa pamoja na ufisadi wake alikuwa na mamlaka na alijua kuyatumia...kwa upande wa pili JK ana mamlaka lakini hajui kama anayo.

2. Mkapa alikuwa mwanafunzi "mwaminifu" aliyekengeuka, haya yote ya kumuenzi Nyerere aliyafanya Mkapa na pengine kumtosa Malecela ilikuwa ktk kukimbia mzimu wa mwalimu wake...kwa upande wa pili JK si mmoja wa wafuasi watiifu kwa Nyerere. Nionyeshe wapi na lini JK amepata kumwita Nyerere baba wa taifa (anamwita mzee Nyerere), hilo pekee halijakushtua hata useme atamtosa EL kwa dhana ya kumuenzi Nyerere????

3. CC na NEC ya sasa haina marais wastaafu wala kina Kingunge (unaweza kunisahihisha), nitajie jina moja tu katika CC au NEC ya sasa mwenye ushawishi wa kubadili uelekeo wa upepo...

By the way wewe ni Nnape?????? just kidding
 
BISHOP HILUKA

Umeuliza "Wajumbe wa mkutano Mkuu wako tayari kuziachia pesa"

Labda tu nikueleweshe kua process ilivyo ni kwamba lazma kwanza Kamati kuu ikae inachuja majina matano na kuyapeleka NEC . NEC inayachuja na kuyapeleka Mkutano Mkuu majina 3. Sasa hoja yangu ni kua Lowasa jina lake haliwezi hata kufika NEC wachilia mbali mkutano mkuu. Pia umedai Nyerere hatakuwepo kutishia kurudisha kadi yake. But hata 2005 Nyrere hakuwepo bali Malecela aligombea na akapigwa chini maana MAWAAZO YA NYERERE 1995 NDIO DIRA NA NI PRECEDENT!!!


Kama Mkapa na Kikwete walikuwa ni wasafi machoni pa Nyerere 1995 je bado ni wasafi hii leo kwa kiwango kilekile cha alichotumia Nyerere? Je wametuhumiwa mpaka unapoleta uzi huu? Je, Nyerere alisema hata Lowasa akifanya kama mtoza ushuru aliyepanda mtini ili amwone Yesu na akamwomba Yesu ale chakula naye, na yeye akamweleza Yesu jinsi mali anavyowapa maskini, je Lowasa hatasamehewa? Kuhusu Richmond, please call a spade a spade. Waziri Mkuu wa Tanzania hajawahi kuwa na nguvu kiasi hicho cha kumzidi Rais mpaka afanye kitu asichokijua rais. Nafikiri hujui politics and responsibility. Rais anayo macho na mikono mingi-TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Jeshi na interpol inaweza kumuhabarisha. How were these organs involved to save embarrasment. Kama hawakufanya kazi yao. can all this be blamed to Lowasa? Lazima tuwe ni wakweli na kama tunataka Tanzania iliyonyoka tuangalie tulipojikwaa na sio tulipoangukia ili tusije anguka tena. Let's discuss the system and how it should work so as to avoid the Lowasa's from assuming highest office in the country. Ninasema Lowasas na sio EL. Hivyo unaponijubu be smart to contextualise your approach
 
POMPO,

Nashukuru mkuu. Pamoja sana. Nakuhakikishia mimi natumwa na UZALENDO. Mambo ya UVCCM hayanihusu.

Umeuliza ni kwanini JK aliweza kupita 2005 na ni vipi EL atashindwa kupita. Kama nilivyosema katika utangulizi wangu ni kua Nyerere alimkubali JK kwani hakuna na kashfa yoyote. Nyerere alimkataa EL kwakua alikua ananuka rushwa ingawa alikua bado kijana mdogo. NASISITIZA KAMATI KUU YA CCM 2015 haitakubali kumpitishwa EL.

Wale wote mnaoganga njaa gangeni jaa zenu lakini mjue kua at the end of the day EL atachinjiwa baharini. Habari ndio hiyo!

Galiya,

Karibu JF.

Sie tumetumwa na Lowassa na tuna njaa. Pundit wa siasa asingesema hayo maneno. Unaponyosha kidole kimoja kwetu vinne vinakuelekea wewe. Safi. Umepewa shs ngapi na wewe?

Nyerere ni Malaika au Mungu mpaka asemalo lazima liwe?. Je kama faili alilopewa "mungu" wako Nyerere lilikua la chuki utajuaje? (remember 'mungu' wako alikua hayupo kwenye system wakati huo)

Je hata kama ni kweli, haijaandikwa kwenye vitabu vitakatifu UKITUBU unasamehewa?, je unajuaje kua Lowassa ameshajirekebisha?

Au ndio magazeti yanafikiria kwa niaba yako?

Karibu JF.
 
Kama Mkapa na Kikwete walikuwa ni wasafi machoni pa Nyerere 1995 je bado ni wasafi hii leo kwa kiwango kilekile cha alichotumia Nyerere? Je wametuhumiwa mpaka unapoleta uzi huu? Je, Nyerere alisema hata Lowasa akifanya kama mtoza ushuru aliyepanda mtini ili amwone Yesu na akamwomba Yesu ale chakula naye, na yeye akamweleza Yesu jinsi mali anavyowapa maskini, je Lowasa hatasamehewa? Kuhusu Richmond, please call a spade a spade. Waziri Mkuu wa Tanzania hajawahi kuwa na nguvu kiasi hicho cha kumzidi Rais mpaka afanye kitu asichokijua rais. Nafikiri hujui politics and responsibility. Rais anayo macho na mikono mingi-TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Jeshi na interpol inaweza kumuhabarisha. How were these organs involved to save embarrasment. Kama hawakufanya kazi yao. can all this be blamed to Lowasa? Lazima tuwe ni wakweli na kama tunataka Tanzania iliyonyoka tuangalie tulipojikwaa na sio tulipoangukia ili tusije anguka tena. Let's discuss the system and how it should work so as to avoid the Lowasa's from assuming highest office in the country. Ninasema Lowasas na sio EL. Hivyo unaponijubu be smart to contextualise your approach

Kamanda kula KUMI.

Hawa wanafikiri sisi ndo wale MKAPA aliwaita wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.

Hakuna ambapo waziri mkuu anamzidi rais NGUVU au madaraka kwa katiba yetu. ENL sio Richmond. tatizo letu tu wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.

Mkapa was right! Wabongo wengi wapo hivyo
 
Mawazo kama hayo ni ya mtu aliyekata tamaa, aliyefika kabla ya kuanza safari.
Barabara ya kwenda IKULU ni sifa za kiongozi. EL je anazo sifa? Kama anazo sifa basi atakuwa Raisi, kama hana hawezi kuwa. Huu uwe ndiyo msimamo wa kila mtanzania na hasa mzalendo. JK alifanikiwa kuukwa urais kwa sababu umma wa watanzania hawakumjua bayana hata hayati Mwalimu Nyerere, kamusi ya watanzaia, msamiati wa JK hakuujua. Edward Ngoyai Lwasa anajulikana wazi kwa kila mtanzania. Kila mtanzania anaujua udhaifu wake na nguvu zake. Udhaifu wake kutaja vitu vichache ni kupenda Rushwa, matumizi mabaya ya ofisi hata udikteta.
Nguvu yake ni uchapa kazi bila kuzingatia taratibu, uwezo wa kifedha kuhonga wajumbe wa vikao vya maamuzi na kutengeneza mitandao ya kugawa chama. "To know an enemy is to be half equipped to conquer. Tunamjua Lwasa ni rahisi kushinda vita. Hata kushindwa vita pia ni rahisi ili mradi tunawajua watanzania kuwa ni wabovu wa KUPOKEA RUSHWA. Kama kipindi cha uchaguzi kitaendelea kuitwa kipindi cha mavuno ya Rushwa ni Dhahiri bin Shahili kuwa LUWASA ataingia IKULU. Si kwa ujanja wake bali kwa upumbavu wa CC, NEC na Mkutano Mkuu wa CCM.
Hapa sisemi upumbavu wa wananchi bali wa viongozi wachache wa chama tawala ambao wametwaliwa na tamaa ya kuvuna wasichopanda kwa njia rahisi ya mlungula.
Kwa kuwa mfumo wa rushwa ndiyo unaotawala basi hata kura watakazopiga wananchi watamkataa, kura zitackachuliwa ama zitaibiwa kwa sababu kila anayeaminiwa anatamani kuitumia imani aliyopewa na watanzania wenzake kujinufaisha yeye binafsi hata kama manufaa anayopata ni ya kipindi kifupi tu. Hakuna mzalendo kuna njaa na uroho tu.
 
sasa hivi ccm wanaangalia mtu ambae watamweka hapo kulinda maslahi yao, na wala sio mtu wa kuleta mageuzi. kwa hiyo sio ajabu sana wakimu-opt el. ccm kitu ingine bana, chezea weye!
kwa mtizamo na uchambuzi wangu, hiyo jumuia inayoitwa ccm achana nayo, yaani hapo atakayetunasua ni Mungu peke yake. kwa sababu; hata vurugu mnazoziona za waislamu sio wao, mnafikiri watatoka madarakani kiurahisi? si damu mpaka imwagike? kwa ninavyomfahamu mwislamu, wana uchungu, imani kali na mapenzi ya ziada kwa dini yao na kila kinachohusu dini yao, sio rahisi wapange eti mtoto akojolee juzuu au koraan ili tu wapate kuwachokoza wakristo.
ccm wanaweza kuhusika na hiyo dili wakijua kabisa hasira za waislamu kuwa hawashikiki wala hawaambiliki, napia wakielekeza matokea ya hasira hizo kuwa chuki kubwa kwa ukristo na cdm ambao sasa hivi propoganda imeelekeza kuwa ni chama cha kikristo.
kwa hiyo kama wanaweza kufanya hayo kumpitisha el sio big deal
 
Wasiwasi wangu ni huu; kwani mwenyekiti wa hicho kikao kitacho toa hizo shutuma si huyu jamaa yake? kama alikua anajua yote unayo yasema, mbona alimchagua kua PM wake? pamoja na huo ufisadi wa mamvi, kumbuka ndie aliyekua mtendaji wa serikali ya Kikwete, njaa ilipoingia wakati ule, huyu jamaa alionehsa kua kweli ni waziri mkuu, alienea nchi nzima, kingine ni hiki, kumbuka mwaka huu mwanzoni wakati huyu atakae kua mwenyekiti wa hicho kikao cha kumchinjia baharini, alibanwa na mamvi kwa muda wa dakika 7 tu, watafiti wanasema, tabia ya Kikwete kucheka cheka hukua nayo ndani ya zile dakika 7, so while mwenyekiti akijipanga kwa hilo, mamvi nae atakuja na single nyingine, kumbuka hawa jamaa wanafahamiana sana tu.

Mimi naamini hivi, kama Kikwete akiyatamka haya ulio jaribu ku-predict lengo litakua ni kuhakikisha kua mamvi haji kua rais si kwasababu nyingine, anahisi jamaa atalipiza kisasi (though binafsi nisingependa kusikia naongozwa na huyu mtu) sababu, kama madhambi kwenye hii awam, wamefanya wote lakini mzigo kabeba pekee yake, wote hawa kwangu mimi naona wapo sawa, Kikwete na huyu pacha wake, tofauti zao ni tu, mwingine anapenda sana mikasi while mwingine ni shabiki wa yale maji ya pale Ilala!
 
LINKOLI

Mi msimamo wangu ni kuwa RUSHWA NI MBAYA HIVYO SIKUBALIANI NA WEWE NA VIONGOZI WENGINE LUKUKI WA CCM WANAODAI ETI RUSHWA CHUKUENI LAKINI MTOA RUSHWA MSIMPIGIE KURA!Sisi ambao umri umeenda kidogo tutakukumbusha kua KANUNI YA 5 YA MWANA TANU 1965 ilisema "CHEO NI DHAMANA, SITATUMIA CHEO CHANGU KWA MANUFAA YANGU BINAFSI KINYUME NA SHERIA"

LOWASA HAFAI
 
YOUNG TANZANIAN

Kwakusema mimi ni mwongo kwamba si kweli SAMUEL SITA NA JK NA LOWASA hawakua pamoja 1995 bali JK NA LOWASA WALIKUA NA ANA MAKINDA inaonyesha ni jinsi gani hujui historia ya chama cha mapinduzi. Naamini wenzangu watakuelewesha maana unaonekana bado ni kijana mdogo
 
Kama kweli Lowassa amechafuka hivyo mnavyotaka tuamini mbona mapovu yanawatoka na kila kikucha ni kumponda?

Kama Lowassa hakubaliki kwanini msiwaachie wananchi waamue?.

Pigieni debe watu wenu, Tangazeni sera zenu.

Usiku kucha hamlali mnamuota Lowassa kisha mnasema hasafishiki.
 
LINKOLI

Mi msimamo wangu ni kuwa RUSHWA NI MBAYA HIVYO SIKUBALIANI NA WEWE NA VIONGOZI WENGINE LUKUKI WA CCM WANAODAI ETI RUSHWA CHUKUENI LAKINI MTOA RUSHWA MSIMPIGIE KURA!Sisi ambao umri umeenda kidogo tutakukumbusha kua KANUNI YA 5 YA MWANA TANU 1965 ilisema "CHEO NI DHAMANA, SITATUMIA CHEO CHANGU KWA MANUFAA YANGU BINAFSI KINYUME NA SHERIA"

LOWASA HAFAI

Jibu basi maswali hapo juu. Usiyakimbie mada umeleta mwenyewe. Au wewe ndio hakimu, mwendesha mashtaka na mtetezi pia?
 
BAGARAONE

Nakubaliana na wewe ndo maana nimesema inabidi tutafakari ili kumpata mtu anaefaa na sio THE LOWASAS ndo maana pia mi sitamtaja nani anafaa!! Tunjadiliane kwa kina Mkuu
 
GALILAYA,

Umeandika vema ila umesahau kuwa Mwenyekiti wa CC ndiyo huyo JK wa Chalinze na misemo kwamba hawa jamaa wamesigana si kweli wapo kishkaji nadhani zaidi kuliko mwanzo.Mimi naona iatakavyokuwa katika hicho kikao cha CC ni statement ya chairman kwamba hayo ya Nyuma ni "ajali ya kisiasa" na ni upepo utapita tu wacheni wan CCM wakaamue katika vikao vya NEC na Mkutano mkuu,Na hapo ndipo EL atakapochanua!!!

Lets wait and see,not too far everything will be revealed!!!
 
Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa uchambuzi wako uliokua mzuri kwa kweli nakupa ahsante sana kwa hilo.
Ila ukweli utabakia kua ndani ya CCM hakuna alie msafi hata huyo Kikwete sio msafi.
 
ASUNGWILE

Kati ya watu woote nimefurahia sana ulivyojenga hoja zako but conclusion sijaipenda. We unadai eti CC hawatewezakumkata kisa ni kwamba watapewa rushwa na wengi hawawezi kukataa. Kama unadhani ni rahisi hivyo mbona 2005 MALECELA alikua na robo tatu ya wajumbe wa vikao vyote vya chama wakiwemo wazee wenzake kwenye CC but alichinjiwa baharini????/
 
kama nyerere kweli alimkubali JK leo hii mwalimu angekua bado yuko hai hivi angesemaje kuhusu hali ya nchi hii JK alivyoifanya mtu ambae alikua anamuona anafaa? wazungu wanasema dont judge a book by its cover
issue ni kuwa, by then jk alikuwa safi bila kashfa! najua huko aliko nyerere hafurahishwi kabisa na madudu aliyoyafanya jk ndani ya ccm!
 
FAIRPLAYER

Inaonekana una CHUKI KALI baada ya kusoma hii makala. Nisemacho mimi nikua sisi wote ni watanzania hivyo ninachotaka ni kua tubishane kwa hoja na sio kuleta chuki. Ukiona mtu analeta chuki ujue hana pointi au kazidiwa hoja. Ni hilo tu kaka!
 
Back
Top Bottom