Iweje Mtanganyika akiagiza mafuata ya kupikia kutoka Zanzibar alipe ushuru na kodi?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,170
Reaction score
8,622
Tanganyika na Zanzibar ni nchi moja.

Huwezi kufanya mapinduzi Zanzibar Sababu Zanzibar zio dola huru.

Iweje Mtanganyika akiagiza mafuata ya kupikia kutoka Zanzibar alipe ushuru na kodi?
 
Tanganyika na Zanzibar ni nchi moja.

Huwezi kufanya mapinduzi Zanzibar Sababu Zanzibar zio dola huru.

Iweje Mtanganyika akiagiza mafuata ya kupikia kutoka Zanzibar alipe ushuru na kodi?
Gentleman,
hivi hao watanganyika unaowahadaa wanafika hata 500 kweli hapa Tanzania?
huenda pia ni wazee sana right?
 
Ama kwa hakika hawajitambui. Huu ndio msimamo wangu. Vinginevyo ni akili gani mtabgabyika kulalamika kodi ya mafuta ya kula kytoka zanzibar isiyokuwa na kitu?
 
Kwa hiyo TRA nayo basi ifanywe kuwa ya Tanganyika peke yake na ajira wapewe Watanganyika peke yao for the sake of fairness.
Mfumo wote wa muungano ni wakuufumua hauko fair kwa upande mmoja.
Changamoto ya muafrika ni Ubinafsi tu Mkuu,
Yani hata wewe unapinga juu ya mfumo huo ukiingia tu kwenye mfumo wa ulaji unapiga kmyaa.
🙏
 
Tanganyika na Zanzibar ni nchi moja.

Huwezi kufanya mapinduzi Zanzibar Sababu Zanzibar zio dola huru.

Iweje Mtanganyika akiagiza mafuata ya kupikia kutoka Zanzibar alipe ushuru na kodi?
Nitakuelewesha Mkuu. Hapo nyuma Zanzibar walikuwa na utaratibu wa kutoza ushuru kama sehemu ya Tanzania. Viwango vya ushuru vilifanana bara na Zanzibar. Sasa ilikuwa ni kipindi cha Mwinyi kama raisi na Komandoo kule Zanzibar wakala njama. Wakaamua kutelemsha sana viwango vya ushuru Zanzibar (import duty) chini ya kiwango ambacho ungetozwa Tanzania bara. Walisema walitaka kuifanya Zanzibar kama port of convenience sijui neno gani walitumia. Kama kitovu fulani hivi kilichofanya Singapore watajirike.

Sasa matokeo ikawa kwamba Watanzania wote wakawa wanaagiza vitu kutoka nje na kuvipitisha Zanzibar, ambako ushuru ulikuwa chini, kisha wanavileta bara,bila kutozwa ushuru mara ya pili. Hata magari watu walifanya hivyo. Kukawa na utitiri wa magari yenye namba za Zanzibar (ZNZ nk) huku bara. Pia ikawa watu wa bara wanaenda Zanzibar kufanya shopping ya TV, mafriji, majiko, viatu, nguo, na kila kitu kwa sababu kule bei zilikuwa chini sana ukilinganisha na bara. Zanzibar ikaanza kutajirika, na huku bara mapato ya kodi ya import duty yakapungua sana.

Sasa TRA wakalalamika, kwamba Zanzibar wanaikosesha Tanzania bara mapato. Maana wimbo uligeukakuwa Zanzibar kila kitu. Nyerere alipoambiwa - akiwa raisi mstaafu na Mwenyekiti wa CCM, akasema, waambieni Zanzibar, watoze import duties kwa viwango vile vile vinavotozwa huku bara. Kina Komandoo wakakataa, wakidai walifanya hivyo ili kuikuza Zanzibar kiuchumi, mishahara kule na kipato kule ni kidogo nk. Ndipo Nyerere akasema, okay, kama haiwezekani kuweka viwango vya import duty sawa na huku bara, basi mtu akileta bidhaa huku bara ambazo alizipitisha Zanzibar, huku bara zipigwe kodi ili "kusawazisha" kodi (yaani kama top up duty). Ikawa kwa mfano, kama uliagiza gari kupitia Zanzibar likatozwa kodi ya asilimia 20% chini ya kodi inayotozwa bara, ukilileta bara litozwe ile tofauti ya 20% ya kodi.

TRA wakaaza kufanya hivyo. Zanzibar wakaja juu, mnatuonea, sie tunataka kuendeleza uchumi, hizi ni kero za muungano nk. Nyerere akasema wanapiga kelele nini tena? Si wamesema tusiwaingilie, kwani sie tumeenda Zanzibar kutoza kodi? Tunatoza kodi huku bara, kama mtu anaona ni gharama kubwa kutozwa kodi mara mbili basi asipitishe bidhaa Zanzibar, azilete moja kwa moja bara.

Ndipo Nyerere siku moja kwenye hotuba akagusia hili, na akasema hawa watu wanafanya mambo kama watoto wadogo. Mtoto mdogo atakunyea halafu analia yeye. Eboo, unaninyea mimi halafu unalia wewe badala ya mimi ulieninyea! Sasa hiyo ndio historia ya kodi kwa bidhaa toka Zanzibar kuja bara ilipoanza, hadi leo inaendelea.

Sasa sema wewe Mkuu, ikiwa watu Nyerere asingewaambia TRA wafanye hivyo, na import duty ya Zanzibar kuwa ndogo kuliko bara, unafikiri athari zingekuwa nini kwa bara? Ingekuwa Tanzania yote inanunua vitu Zanzibar au kuagiza vitu kupitia Zanzibar. TRA bara isingekuwa na mapato yoyote na uchumi wa bara ungekufa. Kumbuka Zanzibar wakitoza kodi hawaleti fedha bara, kwa hiyo bara ingebidi tuwaombe fedha za kulipia mishahara!

Na utaona kwamba tukiwa na raisi wa Tanzania Mzanzibar kuna mambo yanavurugika sana. Hata hili jambo lakodi lilileta mtafaruku sana kati ya bara na Zanzibar, na ni mojawapo ya sababu uhusiano wa Nyerere na Mwinyi uliharibika sana, kwa sababu ilionekana hili jambo lilikuwa na support ya Mwinyi - au labda Mama Sitti.

Wakati Mwinyi akiwa Raisi Nyerere alisimamia sana mambo ya bara kama Mwenyekiti wa CCM, tofauti na sasa ambapo raisi ndie huyo huyo mwenyekiti wa CCM hivyo hakuna mwenye mamlaka ya kuisimamia bara
 
Mtu kanunua tv Zanzibar nchi 32 akafurahie na watoto wake manzese, anafika pale bandarini anaambiwa alipie 180,000 kama Kodi 🤔
 
Huu ni utani pana vitu inatakiwa Watanzania walipie ila sio tv tena used kutoka Zanzibar..
 
TRA haipaswi kuwaajiri Wazanzibari kwani hakuna Mtanganyika aliyeajiriwa ZRA, pesa zinazokusanywa na TRA hazipaswi kutumika upande wa Zanzibar kwani zile zinazokusanywa na ZRA hazitumiki Tanganyika.
Haya mambo ukiyafuatilia yanatia hasira sana, kama hakuna uwezekano wa kuwa na serikali moja inapaswa muungano uvunjike na kila mtu arudi kwao. Watakao taka kwenda kwa wenzao kufanya shughuli zozote waingie kama foreigners na wafanye applications za kama ni working permits au business permits au students permits kama foreigners wengine wanavyofanya.
 
Back
Top Bottom