Iundwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iundwe

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kigarama, Oct 19, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama kuna mwananchi wa nchi hii (Jamiiforums) ambaye kifo chake (LifeBan) kilitingisha vyombo vya habari (Majukwaa) basi ni Dada/Kaka FaizaFoxy. Lakini haijajulikana ni nini hasa kilisababisha kifo chake. Mpaka sasa maelezo kuhusu kifo chake yanategemea zaidi porojo za mitaani na kwenye vile vikao vya ndani (Private Messages) vya vikundi mbalimbali.

  Inawezekana FF yuko hai (Active in JF) lakini watu wanamhisi tu au wanamuona kama ni mzukule (Kupitia user name zingine) na wakati mwingine haileti Raha kujibishana na Mizukule. Kifo chake kimesababisha nadhani kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa Mohamed Said ambaye kwenye uchangiaji yeye na FF walikuwa kama pacha vile.

  Ushauri wangu kwa wananchi wote (JF Members) tuishinikize serikali yetu (Moderators) iunde tume huru kuchunguza sakata hili la kifo cha FF. Na tume hiyo ihusishe wananchi wa kada zote bila kubagua na mtokeo yake yamwagwe humu bila ya kuvungavunga.

  Napigania haki ya uhuru wa kutoa maoni unaohakikishwa na Katiba yetu!!
   
 2. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  mh spika oh sory mh mtoa mada naunga mkono hoja yakundwa kwa tumehuru ya uchunguzi juu yahilo.ila kwenye kipengele cha mwisho kinachosema unapigani haki ya uhuru.naomba ufafanuzi unapigania mwenyewe huo uhuru?pili hapo mwisho tueleze uhuru wa kutoa maoni ya ainagani unaotaka utambuliwe na katiba?maoni yanaweza kua na vijineno vya matusi au kutumika lugha isyofaa
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vijineno na matusi yanaweza kudhibitiwa na Moderators hata mimi siungi mkono matusi lakini vijineno ndiyo Uswahili wenyewe huo!!
   
Loading...