ITV ndani ya DSTV via Channel 293 kuanzia kesho

Matukutuku

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
269
126
ITV itaanza kuonekana DSTV kuanzia kesho! Ila sijajua itakuwa chaneli gani, tusubirie hiyo kesho

ITV imeingia rasmi kwenye king'amuzi cha DSTV kwa chanel namba 293.
dstv1.jpg

Hatimae kilio cha muda mrefu cha watazamaji na wapenzi wa ITV juu ya ITV kuingia kwenye king'amuzi cha DSTV kimesikika na sasa ITV imeingia rasmi kwenye king'amuzi hicho na itaonekana kwenye vifurushi vyote vya DSTV.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhavile amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya ITV na DSTV kuhusu ITV kuingia katika king'amuzi chao sasa wamefikia muafaka ambapo watazamaji na wapenzi wa ITV wenye ving'amuzi vya DSTV kwa sasa watakuwa wanapata matangazo yote ndani ya DSTV.

Meneja uhusiano wa Multichoice Tanzania Bi Barbara Kambogi mbali na kueleza furaha ya kampuni yake baada ya ITV kuingia kwenye king'amuzi chao amesema wakati mwingine walikuwa wanashindwa kufikia lengo la kupata wateja wengi zaidi kutokana na kukosa chanel ya ITV hivyo kuanzia sasa ni imani yao kuwa idadi ya wateja itaongezeka maradufu na kuongeza kuwa ITV itapatikana kwenye chanel namba 293.
 
Safi! Supa brandi ndani ya supa brandi!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
good news. alafu nackia DSTV wameshusha bei balaa! nashkuru hizi habari zimekuja mwisho wa mwezi naenda kufanya maamuzi magumu kesho. nimechoka na ving'amuzi uchwara vya uswahilini
 
good news. alafu nackia DSTV wameshusha bei balaa! nashkuru hizi habari zimekuja mwisho wa mwezi naenda kufanya maamuzi magumu kesho. nimechoka na ving'amuzi uchwara vya uswahilini

Ha Ha Ha Kwa hiyo unawasema Startimes ha ha ha
 
Back
Top Bottom