Kwanini Tundu Lissu anapewa airtime kubwa sana ITV kuliko Rais wa nchi? Serikali iwachunguze!

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,577
7,117
Kuna vyombo vya habari nchi hii vinashabikia uvunjifu wa amani, wanashabikia habari hasi dhidi ya serikali. Je ni kwamba wana ajenda ya siri, wanatumiwa na vibaraka kuchafua taswira ya nchi yetu? Je, nchi hii ikiparanganyika wao wana nchi nyingine ya kuishi? Imekuwa kawaida vyombo vya habari km ITV na Mwananchi kuhujumu jitihada ya serikali yetu. Taarifa itakayopewa kipaumbele ni ile ya kizushi, ya kipotoshaji, taarifa yoyote hasi.

Kwa mfano jana, ITV ilitumia dakika zaidi ya 10 Tundu Lissu alivyokuwa anabwabwaja jana kwa mbwembwe atakavyoishughulikia serikali yetu ya Tanzania, yule mwehu anaongea utafikiri siyo raia wa nchi hii. Lissu na genge lake wanajulikana ni vibaraka vya wazungu, wasaliti wa Taifa ndio maana Magu alitaka kumalizana naye. Lissu ni mtu hatari kwa Taifa hili siyo wa kumpatia coverage kubwa namna ile.

Rais wetu jana alifanya mambo mengi sana ya kimaendeleo kwa watanzania, alizindua miradi mikubwa lakini haikutangazwa inavyostahili, kulikuwa na waandishi wa ITV ktk msafara wa Rais lakini taarifa hairushwi inavyostahili, Rais wa nchi ndio raia namba moja, taarifa zake ndio ya kwanza kutangazwa ht vyombo vya nchi zilizoendelea ndivyo vinavyofanya.

Gazeti la Mwananchi wanajulikana ni maadui wa maendeleo na amani ya nchi yetu. Serikali iwafukuze waandishi wa hivi vyombo ktk msafara wa Rais na misafara mingine ya viongozi wa serikali, isiwape kazi yoyote, serikali ivifanyie uchunguzi wa kina hivi vyombo ikiwemo mwenendo wa uendeshaji, ulipaji wa kodi. Km wanaihujumu serikali basi serikali nayo iwahujumu.

Serikali ina nguvu kubwa. Angalia Mwananchi ya leo, taarifa kubwa "Lissu atoa msimamo" eti hii ndiyo habari kubwa ktk nchi yetu siyo ziara ya Rais wetu. Mh. Rais unawachekeaje wasaliti km hawa? Na nyie vyombo vya intelligence mmezubaa wapi, mbona hamumsaidii Rais? Hivi vyombo vya ITV na Mwananchi serikali isiwape ushirikiano, isiambatane nao kwenye shughuli zake.
 
Wewe mwenyewe ni kibaraka baadala ya kufungua uzi kumuongelea Rais umeamka asubuhi na kuanza kumuongelea Lissu

1000012670.jpg
 
Halitasalia jiwe juu ya jingine bila kubomoshwa mpaka museme porini huwa mnakwenda kufanya nini.
Dami ya mtu ni mbaya sana. Wakati wa Daniel kwenye Utawala wa Mfalme Dario( Darius) baraza la mawari( maliwali) lilimlia njama Nabik Daniel ili vyombo vya Dola vimkamate na kumuua kwa Kumtupa kwenye Shimbo la Simba.

Aisee kilichotokea ni kwamba Wake, na watoto wa mawaziri na mawaziri wenyewe wote waliupwa wao. Simba waliwalarua vibaya mno wakafia mle.

Na sasa Mungu amemfunulia haki Tundu Lissu kwa namna nyingine kabisa ambayo hakuna aliyewahi kuifikiria.

Kweli Mawazo.ya Mungu sio kama ya Wanadamu.
 
There we go again.

Hii ni serious social thinking issue Tanzania.

Ya watu kudhani wengine wanamajukumu na responsibility ya achievements.

Ili ni moja ya tatizo kubwa sana amongst many others in social thinking.

Lazima apatikane mtu wa kunyoosha akili watanzania. Social thinking ya watanzia is serious problem to development.
 
Back
Top Bottom