ITV leo mmethubutu kupitia kipindi cha "Malumbano ya Hoja"

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,683
149,887
Mada yenu ya leo kuhusu Hukumu ya Mahakama ya katiba ya Afrika Kusini kumtia hatiani Raisi Zuma na kwamba inatoa funzo gani kwa viongozi wa bara la Afrika na hasa hapa nchini,ni mada inayolenga kutuamsha watanzania juu ya kinga ya raisi wa nchi hii kutoshitakiwa.

ITV ni kama mmeamua kuchokoza na kuanzisha mjadala kuhusu kinga hii na niambo huu uwe mwanzo wa sisi kipitia upya kipengele hiki cha Katiba.

Nasema ITV wamethubutu kwasababu kumekuwa na uoga wa kichinichini kwa vyombo vya habari hapa nchi kuendesha mijadala kuhusu kipengele hiki cha 46 cha katiba ya nchi yetu kinachotoa kinga ya raisi kutoshitakiwa.

Fuatilia ITV mjadala unaendelea.
 
Kwa Tanzania yetu akitoka Mungu ni rais ndie anafuatia tunahitaji katiba mpya.. Na hili mh Pombe akilitekeleza atakuwa rais wa kuigwa
 
Mjadala umetulia Sana, ukiachilia mbali wachokoza mada, leo star wa wachangiaji japo wengine wanaendelea kuchangia ni G.Rutabuzinda.
 
Tanzania ni fundi seremala.huyu mzee kamzidi hoja balile,kaonyesha unafiki wa magu,unatumbua majipu huku katiba mbovu,zanzibar hoi
 
Ngowi amesema katiba ya Warioba lazima irudishwe na amemuomba Rais Magufuli arudishe katiba mpya.
 
Huyu nae naona anatafuta ukuu wa wilaya maana naona katoka kabisa nje ya mada anajadili maswala ya kukusanya kodi na waongoza kipindi wamemvumilia kwasababu tu nadhani yuko meza kuu.
Balile huyu siyo balile yule niliyemfahamu kabadilika moja kdg kwa moja
 
Balile amejitoa ufahamu kabisaaaaa, anachojibu nje ya hoja iliyopo mezani, jamani hizo ajira 46 na zitoke tu watu akili ziwakae sawa.
 
Back
Top Bottom