Kupitia ripoti ya haki Jinai; tunawezaje kuunda chombo kimoja cha uchunguzi bila mabadiliko ya katiba?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Nimesoma ripoti ya tume ya Mhe. Rais kuhusu mabadiliko ya haki jinai; kupitia mapendekezo yaliyotolewa ninaamaoni kwamba tumeanza kupunguzwa kasi ya kutaka katiba mpya au upo uwezekano wajanja wameanza kuunda vipengele vya katiba kwa mfumo wa tume za maboresho.

Endapo tutaruhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo tutakuwa tayari tumeanza kuingilia mambo ambayo tulilazimika kuyaweka kwenye katiba na siyo sheria. Naomba nitaje mambo matatu ambayo yanahitaji mabadiliko ya katiba na siyo sheria;

1. Kuundwa kwa chombo kimoja cha uchunguzi (TANZANIA NATIONAL INVESTIGATION BUREAU). Hili pendekezo linahitaji fedha nyingi lakini pia linahitaji utafiti mkubwa kabla ya kulitekeleza: wananchi lazima washirikishwe upya wasema wanapenda chombo cha muundo gani, watendaji wake watapatikanaje, je kitakuwa na kinga? Uwajibishwaji utakuwaje NK. Aidha pendekezo hili naamini limesukumwa zaidi na wakuu wastaafu wa polisi wakitaka mamlaka ya uchunguzi ibaki polisi. Tunafahamu kwa polisi tulionao sasa ili jukumu la uchunguzi liliwashinda na kupelekea baadhi ya kazi kuundiwa mamlaka zake ikiwemo madawa. Je waliofanya utafiti wakaona polisi wameshindwa kuchunguza kesi za madawa tayari utafiti wao unakwenda kufutwa na tume?

Lakini pia tujiulize; kama taasisi za uchunguzi zipo kikatiba, hiki chombo kikubwa cha uchunguzi kitafanyaje kazi bila kuundwa kikatiba?

Napendekeza: Tusiwekeze fedha za umma kuunda chombo cha uchunguzi kwa sasa; tuwekeze fedha kuunda katiba ambayo itatuambia ni muundo na mfumo gani wa haki jinai unatufaa kikatiba. Tukiruhusu taasisi zianze kujitengeneza tutashindwa kuja na kitu cha kueleweka kwenye katiba tunayopanga kuiandika.

2. Nimeona na kushtushwa na kauli kwenye tume ya uwepo wa utitiri wa majeshi nchini; hapa kuna mtego tunataka kuletewa tuondoke kwenye hoja ya kikatiba iliyopo mbele yetu na ambayo tunalenga hii iwe agenda. Ndugu wananchi; hakuna jeshi kwa mujibu wa katiba linaanzishwa bila idhini ya Mhe. Rais wa nchi; majeshi yote yameidhinishwa na Mhe. Rais na baadhi ya Majeshi hayo kama Uhamiaji ni juzi tu Mhe. Samia Suluhu Hassan alipisha na kusaini sheria waziri wa Mambo ya ndani akiwa Mhe. Simbachawene. Wakati hoja ya uhamiaji kuwa jeshi ilipojitokeza tulihoja hapa JF lakini waziri alitamka kwenye vyombo vya habari kwamba Mhe. Rais ameridhia kwa sababu za kiusalama na nidhamu Uhamiaji wawe Jeshi. YouTube clip ipo na hapa mada za kuzungumzia Uhamiaji kuwa jeshi zipo.

Je, kama vyombo hivi hivi vilimshauri Mhe. Rais akasaini sheria baadhi ya wajumbe wakiwemo ma IGP wastaafu naamini walishiriki huu mchakato, je ni utafiti gani mpya wamefanya wanaonyesha kwamba Mhe. Rais aliyepitisha haya majeshi alidanganywa? Pendekezo ili kwangu mimi naliona kama uchochoro wa kutuondoa kwenye agenda ya kitaifa ya kujadili muundo wa vyombo vya ulinzi na usalama kikatiba na baadaye kisheria. Tusikubali kuanza kuvuruga taasisi tusubiri wananchi wapitishe katiba mpya ndipo tuunde vyombo hivi upya. Bora tunachelewa Ila tukaruhusu wananchi watuambie vyombo vipi ni majeshi na vipi siyo majeshi kikatiba. Lakini pia mamlaka ya kuunda jeshi kikatiba iangaliwe pia ili huko mbele atahari zilizoelezwa na tume zisijitokeze ikiwemo hoja ya kuzagaa silaha. Vinginevyo mimi naliona pendekezo ili kwa sasa linalenga maslahi binafsi na wivu wa kitaasisi zaidi( rejea kauli kwamba majeshi yanajilinganisha na JW) kuliko kule ambapo tunapaswa kwenda. Hatutaki wivu wa taasisi tunataka ufanisi wa taasisi bila kujali ni yakuraia au kijeshi.

Pendekezo; hoja ya kutafsiri jeshi ni hoja ya kikatiba, na Mhe. Rais amesema tunahitaji katiba. Ninashauri Muundo uliopo ubaki kama ulivyo hadi pale katiba mpya itakapotuelekeza tafsiri mpya ya jeshi, idadi ya majeshi, muundo, majukumu nk. Tukumbuke ili eneo limepelekea sana Polisi na vyombo vingine kutuumiza wananchi; tusiwaruhusu wajirekebishe kwa Muundo wanaotaka wao; tayari wameonyesha pendekezo lao linalenga kulinda saluti na si kule wananchi tunapotaka kwenda.

3. Tume imeenda kugusia mamlaka ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya; hapa napo kuna mtego. Haki jinai haikosekani kwa sababu ya DC na RC kutumia madaraka vibaya; haki jinai imeonekana wazi kwamba inakosekana kutokana na mamlaka makubwa aliyonayo mkuu wa nchi. Tume ilipaswa kurejea kilichofanywa na awamu ya tano. Mamlaka ya wanasiasa ilikuwa kubwa sana kila mtu alilazimika kutii bila kujali sheria wala katiba. Ndugu wananchi, pendekezo la tume likiruhusiwa kutekelezwa kabla ya mabadiliko ya katiba tutajikuta tumepokonywa nguvu ya kudai katiba kwa kitakachoitwa nia njema. Nampongeza Mhe. Rais kwa nia njema lakini je tunahitaji Mhe. Rais mwenye nia njema au tunahitaji taasisi ya urais inayoelekezwa na katiba namna ya kuongoza kwa nia njema? Tusikubali fedha zikawekezwa kwenye eneo hili tusubiri katiba ije iseme mamlaka ya viongozi wa kisiasa ni yapi na watumishi wa umma Wana mamlaka gani? Kwanza lipo pendekezo la kufuta baadhi ya vyeo vya kisiasa; tuwekeze kwenye katiba.

Haya mambo matatu nimeyaweka hapa kuwafungua macho kwamba hayawezi kufanywa bila mabadiliko ya katiba; tusiruhusu fedha za umma ziingizwe hapa kwenye haya maeneo kwa sababu katiba inalenga pamoja na mambo mengine kuyatibu haya.

Uwezi kuunda chombo cha uchunguzi ambacho kitaleta mabadiliko kwa katiba huu, uwezi pia kubomoa mfumo wa majeshi nje katiba kama ambavyo ni vigumu kuyaangalia mamlaka ya kisiasa nje ya katiba.

MNAPENDA KATIBA BORA, MNAOPENDA MATUMIZI MAZURI YA RASILIMALI NA MNAOAMINI KWENYE TAASISI IMARA MSIKUBALI HAYA YAKAFANYWA NJE YA KATIBA.
 
Mimi siongozwi na Mwenyekiti; naongozwa na Roho wa Mungu.
Tunapojadili mambo yenye tija kwa Taifa jaribu kunyamaza maana tunakutengenezea kesho yako.

Tunapomshauri Mhe. Rais njia bora ya kuendana na mapendekezo ya tume ni kwa sababu kutualika tufanye hivyo. Ndio maana tunauliza kipi kutangulie kati ya katiba na utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya tume.

Lakini tunapendekeza kumkumbusha Mhe. Rais kwamba baadhi ya mambo ambayo tume imemwambia kwa lugha isiyopendeza (UTITIRI WA MAJESHI) yeye ni mmoja wa waanzilishi wa hayo majeshi hivyo kauli iliyotumiwa na tume si nzuri kwetu wenye nia naye nzuri....watafute kauli isileta picha kwamba Marais wanadanganywa.

Mwisho, tujadili hoja siyo vihoja
 
.MNAPENDA KATIBA BORA, MNAOPENDA MATUMIZI MAZURI YA RASILIMALI NA MNAOAMINI KWENYE TAASISI IMARA MSIKUBALI HAYA YAKAFANYWA NJE YA KATIBA.
Moja shika sii kumi nenda rudi!. Mchakato wa katiba ni long process, ukiweza pata kidogo, pokea.
P
 
Moja shika sii kumi nenda rudi!. Mchakato wa katiba ni long process, ukiweza pata kidogo, pokea.
P
Mwandishi nguli Pascal nisaidie kujua; unaweza ukawa na Taifa lenye chombo cha uchunguzi kisichotambulika kikatiba?

Unawezaje kuunda au kubadili majeshi bila kubadili katiba?

Unaweza kupunguza madaraka ya kisiasa yanayokwaza mfumo wa haki jinai bila kubadili katiba?
 
Mwandishi nguli Pascal nisaidie kujua; unaweza ukawa na Taifa lenye chombo cha uchunguzi kisichotambulika kikatiba?

Unawezaje kuunda au kubadili majeshi bila kubadili katiba?

Unaweza kupunguza madaraka ya kisiasa yanayokwaza mfumo wa haki jinai bila kubadili katiba?
Katiba sio Msahafu, unaweza kuchomekea chochote muhimu kwenye katiba ya sasa kwa kufanya marekebisho ya katiba bila kulazimika kubadili katiba.

Mfano tunakwenda kuunda upya NEC na kubadili sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2025.
p
 
Katiba sio Msahafu, unaweza kuchomekea chochote muhimu kwenye katiba ya sasa kwa kufanya marekebisho ya katiba bila kulazimika kubadili katiba.

Mfano tunakwenda kuunda upya NEC na kubadili sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2025.
p
Lengo la kuweka viraka nikutaka kufikia malengo gani?
 
Back
Top Bottom