Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Wotu tunafahamu kuwa serikali haina dini ila ni serikali hii hii inayosimamia uanzishwaji wa makanisa na misikiti na hata kuyasajili.
Binafsi naona wakati umefika serikali isiishie katika kuyasajali tu makanisa haya bali tuwe na sheria itakayoruhusu serikali kupitia chombo/maafisa maalumu kukagua matumizi na mapato katika nyumba za ibada.
Nasema hivi kwassababu siku hizi katika makanisa yetu(sisi wakristo) tumekuwa na michanga mingi kwa jina la sadaka,n.k mpaka inakuwa kero kwa waumini.
Hoja yangu ni kuwa,japo kunaweza kuwa na udhibiti ndani ya nyumba zetu hizi za ibda,lakini nadhani kuna umuhimu wa kuwa na udhibiti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha hizi utakaokuwa unafanywa na chombo kutoka serikalini kama extenal auditer.
Vile vile sheria hiyo itumike katika kusimamia aina ya michango inayoanzishwa kuanzia katika ngazi za jumuiya mpaka makanisani na ikiwezekana kuwe na ukomo wa kiwango cha kuchangisha waumini na kama itabidi kuvuka kikomo kilichowekwa, basi kanisa husika lipaswe kuomba kibali au kutoa taarif kwa chombo kitakachoanzishwa na ambacho kitakauwa mamlaka ya kudhibiti mapato na matumizi katika nyumba zetu za ibada.
Lengo la kuwa na ukomo katika michango hii ni ili kuzuia waumini wasio na uwezo kukamuliwa michango isioendana na vipato vyao halisi na pia kudhibiti michango inayoweza kuwa na ulakini lakini kwa alie tayari kuchagia zaidi, aruhusiwe mradi tu muhusika mwenyewe ameridhia.
Na ili kuondoa uwezekano wa kutokea mgongano au mgogoro baina ya serikali na taasisi za kidini,chombo hichi kiundwe kwa kushirikisha serikali na taasisi zote za dini.
Tusisahau kuwa baadhi ya viongozi katika siasa au vyama vya siasa,taasisi za serikali,taasisi binafsin.k ndio wakati mwingine huwa ni viongozi katika taasisi hizi za kidini hivyo kama wanakaguliwa katika taasisi zingine wanazoziongoza,basi hata katika taasisi hizi za kidini pia wakaguliwe jinsi wanavyodhibiti na kusimamia mapato na matumizi katika nyumba za Ibada.
Kama tunavyoona umuhimu kuwa na sheria ya kudhibiti mapato na matumizi katika vyama vya siasa,vyama vya ushirika,SACCOS,n.k,umuhimu huo pia unahitajika katika nyumba zetu za ibada kwani siku hizi mambo katika nyumba zetu za ibada yamebadilika sana tofauti na siku za nyuma.
Ni kweli serikali haina dini,lakini waumini katika taasisi hizi za kidini ndio hao hao ambao wanaunda SACCOS,vyama vya ushirika,n.k ambako serikali ina mkono wake katika uendeshaji wa taasisi hizi ili kulinda masilahi ya wananchi wake.