Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Uwe askari polisi , uwe daktari, uwe mwalimu, uwe mwanajeshi, uwe hakimu au jaji, uwe mkulima, uwe mfanyakazi, uwe bodaboda uwe Mama ntilie, uwe machinga au uwe jobless usipochukua hatua hiya Oktoba 29 ndo umeweka muhuri kwenye kunyanyaswa kwako na kuibiwa rasilimali zako huku wewe, familia yako, ndugu zako wakiishi maisha magumu wasiyostahili.
Wakati kikundi kidogo cha Wanasiasa na Viongozi kikiiba kodi na kutapanya kodi za Wananchi kwa kiwango cha kutisha na kwa dharau ya juu kabisa kwa Wananchi, maisha yetu sisi wananchi wa kawaida yanazidi kuwa magumu kila kukicha.
Hakuna Maji ya Uhakika, hakuna huduma za uhakika hospitali hasa madawa na vifaa tiba ya kutosha, Barabara zetu ni mbovu sana si mijini si vijijini, Watoto wetu wanasoma kwenye shule zisizo na miundombinu bora na ya uhakika huku wanaosoma kwenye jiji kubwa kama Dar wakipata shida kubwa ya adha ya usafiri.
Gharama za maisha zinazidi kupanda kila kukicha, bei za bidhaa zinazidi kupandishwa kila kukicha na kuzidi kufanya maisha yetu wananchi kuwa magumu kila siku, ajira hamna kwa vijana wetu huku matukio ya kuuwawa, kutekwa na kupotezwa ndugu zetu yakizidi kushamiri kila Leo
Enough is enough. Nitashiriki maandamano ya 29 Oktoba 2025. Vyovyote vile hata nikifa lazima nchi ipate ukombozi dhidi ya hawa madhalimu CCM.