Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
 
Arejeshe fao la kujitoa. Fao hili ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi. Kijana akiacha kazi,au akiachishwa au kampuni yake ikifunga biashara akipewa fedha yake aliyoichanga kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii,Kijana huyu ataanzisha biashara, ataendelea kjlipa kodi,ataweza kuajiri watu wawili au watatu.
 
naam,hatakubali ccm ife mikononi mwake itakuwa aibu

Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
Board ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
 
AUNDE TUME ITEGUE KITENDAWILI TUJUE WASIOJULIKANA N BINADAMU AU MARUHANI MAJINI?
Je AZORY GWANDA,BEN SAA NANE WAKO WAPI?
NAN ALIMSHAMBULIA TUndu LISSU
NI KINA NAN WAlIGAWANA BILION MOJA YA MO?
NAN ALIMTEKA ROMA MKATOLIKI
WASANII NA VIONGOZ WA DINI WASIRUHUSIWE KUSHIRIK MIKUTANO YA SIASA?
MCHAKATO WA KATIBA MPYA UANZE MARA MOJA
 
Back
Top Bottom