Itachukua muda gani kupata upinzani wa kweli Tanzania

Nani kakuambia China wananchi wana maamuzi na uwepo wa raisi na muda
wa kukaa madarakani? Saa nyingine upeo wa watu kama ninyi ndio unaotaka kunilazimisha niamini kuwa sisiemu itaendelea kutawala. Lakini aamini nakwabia kabla jogoo hajawika mkesha wa 2022 utakuwa umeikana CCM Mara tatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale fursa za vijana kutoka vyuoni zinapozidi kukwama na watu ambayo hawajapata ujuzi wanapokutana katika mgongano wa kimaslahi..maana fursa zitakuwa hazieleweki na kuchambulika kulingana na ongezeko la watu na kukosekana kwa ardhi ya kufanya shughuli za kawaida,shida itatokea katika mfumo uliozoeleka wa chama kimoja kuwa kinapata ridhaa..lakini serikali ikiweza kuongeza watendaji/watumishi katika kila sekta na kuboresha mipango miji na upatikanaji wa huduma za kijamii,kuwa na mfumo mzuri wa watu kufanya kazi kupata kipato na kuweza kulipa kodi,katika asilimia kubwa nadhani hakutakuwa na upinzani..
 
Ndio maana watanzania wakati ule wa kura za maoni kuhusu vyama hawakutaka mavyama ya watu kujitengezea ulaji..ila kwa maana na kwa maana ya kuleta challenge na kuibua madudu yanayofanywa na mwingine umuhimu upo..hatusemi serikali zote zitafanya kazi kwa uaminifu kama hii ya sasa ya Magufuli..ila tunatakiwa wote tujenge nchi kama tunakuwa na mtazamo mmoja..sio wengine wananunua ndege na kujenga miundombinu ya kimaendeleo wengine wanapinga wanataka pesa sijui ziende wapi..labda mifukoni wakazile...upinzani gani huu wa ajabu..wengine wanataka watu walipe kodi..wengine wanawatetea eti ni ukandamizaji..sasa nchi itaendeleaje..wengine wanawasaidia watu wakwepe kodi...wengine wanakumbatia mafisadi..
Uaminifu mbona wameiba tilioni 2.4 ,Ndio uaminifu huo vote no 20 . Kununua ndege za kuvuta na kamba ,vivuko vibovu kuvurunda korosho ,mbaazi , kashindwa kuajiri ,kuongeza mishahara ,kuteka ,kuua ,kufunga kwenye viroba ,kuua uchumi ,kaharibu mzunguko wa pesa ,kudhulumu wafanyabiashara wa viroba ,kaharibu uhusiano wa kimataifa na wawekezaji , ushamba ,ulimbukeni ,chuki visasi ,teua tengua zisizo na tija ,kuporomosha thamani ya shilingi ,kuteua mawaziri ,wakuu wa mikoa na wilaya wasio na sifa , dhuluma ,roho mbaya ,kuwanyima mikopo wanafunzi elimu ya juu ,kupora maduka ya fedha za kigeni ,wewe una yasupport Yote haya kabisa .
 
Wasalaam wana Jf.
Baada ya mambo mengi yanayotokea juu ya siasa za Tanzania na tetesi zinazoendelea kuwa tusubiri kuyaona makubwa zaidi ya haya Kwa vigogo wa cdm kuamia upande wa pili. Na hili ndio linanifanya nikubaliane na mwana jf mmoja ambaye ameandika kuwa ccm itatawala zaidi ya miaka Mia, sio Kwa kuwa ni chama imara ila kwasababu hakuna upinzani imara. Swali hapa ni Itatuchukua mda gani kupata chama cha upinzani kilichokuwa imara kushindana na ccm, na kikiweza kuchukua dola kiwe na uwezo wa kuunda serikali yake bila kuwa na mamluki wa chama tawala.
Uchambuzi yakinifu ndio msingi wa mada.

Nawasilisha

Chama imara cha upinzani kinapimwa kwa vigezo vipi? Kinaundwa na watu gani na kwa faida ya watu gani? Jibu fupi ni kuwa: siku wanaotarajia kunufaika na kuwepo kwa vyama mbadala (pinzani) imara watakapoamua wanataka viwepo basi vitakuwepo. Kama Watanzania wa aina hiyo hawapo au ni wachache sana basi haitawezekana! Na Tanzania itabakia kuwa nchi ya ajabu ajabu kama zilivyo Burundi, Rwanda na Uganda leo hii.
 
Back
Top Bottom