Itachukua muda gani kupata upinzani wa kweli Tanzania

Wajinga wapi sasa unaozungumzia..na wewe ukiwemo au..?? Au wewe haumo..be specific..!cha msingi hapa wananchi tunataka maendeleo ya kiuchumi kwa jumla..kama ccm itaendelea kuleta maendeleo ya kweli kama inavyofanya kwanini tuiondoe madarakani..wacha itawale milelee....utakuwa ni ujinga.kuamua.kisa eti zamu ya wengine kula..upumbaf...
Maendeleo gani yanayoletwa na CCM hii tunayoijua ?!. Maendeleo wakati uchumi wa wananchi umekufa ?!
Yapi hayo ? Ya ndege !!.
Ethiopia wanazo ndege kuliko taifa lolote Africa , lakini kila siku ni njaa, ukimbizi nk nk

Hawa wetu ni wasanii na hawawezi kuleta chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana Jf.
Baada ya mambo mengi yanayotokea juu ya siasa za Tanzania na tetesi zinazoendelea kuwa tusubiri kuyaona makubwa zaidi ya haya Kwa vigogo wa cdm kuamia upande wa pili. Na hili ndio linanifanya nikubaliane na mwana jf mmoja ambaye ameandika kuwa ccm itatawala zaidi ya miaka Mia, sio Kwa kuwa ni chama imara ila kwasababu hakuna upinzani imara. Swali hapa ni Itatuchukua mda gani kupata chama cha upinzani kilichokuwa imara kushindana na ccm, na kikiweza kuchukua dola kiwe na uwezo wa kuunda serikali yake bila kuwa na mamluki wa chama tawala.
Uchambuzi yakinifu ndio msingi wa mada.

Nawasilisha
Labda kwanza utusaidie tufafanua upinzani ni nini kabla ya kuzungumzia upinzani wa kweli au uogo
2
 
Hahahaha hizi ni ndoto..upinzani wa kweli utatoka wapi bana..??? Kuna binadamu gani asiyetaka kula..akiona huko hapati mkate wake na watoto wake si anaenda sehemu yenye maziwa na asali...nani anataka kufa na njaa..sasa kama mapesa ya ruzuku yanaliwa nawatu wawili watatu, ungekuwa wewe ungevumilia..??? Upinzani unawexa kuwa na nguvu kama serikaii ni dhaifu haitekelezi ahadi zake..lakini ukipata serikali kama hii ya ccm, nakwambia milele hutakaa uende ikulu eti mpinzani...ndio maana kama China waliamua Rais wao aendelee mpaka wananchi watakapoamua vinginevyo..kwa manufaaa ya taifa na sio kwa manufaa ya tumbo la mtu
Hujamuelewa huyo jamaa? Watanzania wote kwa ujumla wetu hatuwezi kutegemea kushibisha matumbo yetu naya watoto wetu kwa kutegemea tu ruzuku inayopewa chama fulani cha siasa.so upinzani wa kweli unatoka kwetu wananchi.Jitahidi kujifungua kutoka kwenye box la vyama mkuu
 
Mkuu huyo Babeli anakaa kwa dada yake asikuumize kichwa. Kwake yeye maendeleo ya shemeji yake ni kununua flat screen
 
Wajinga wapi sasa unaozungumzia..na wewe ukiwemo au..?? Au wewe haumo..be specific..!cha msingi hapa wananchi tunataka maendeleo ya kiuchumi kwa jumla..kama ccm itaendelea kuleta maendeleo ya kweli kama inavyofanya kwanini tuiondoe madarakani..wacha itawale milelee....utakuwa ni ujinga.kuamua.kisa eti zamu ya wengine kula..upumbaf...
Jr ni kweli maendeleo haya ya kiuchumi yaliyopo sasa yanamgusa mwananchi moja Kwa moja? Ukiusianisha na ununuzi wa ndege, kupanda Kwa dola dhidi ya tsh na issue ya wakulima
 
Wasalaam wana Jf.
Baada ya mambo mengi yanayotokea juu ya siasa za Tanzania na tetesi zinazoendelea kuwa tusubiri kuyaona makubwa zaidi ya haya Kwa vigogo wa cdm kuamia upande wa pili. Na hili ndio linanifanya nikubaliane na mwana jf mmoja ambaye ameandika kuwa ccm itatawala zaidi ya miaka Mia, sio Kwa kuwa ni chama imara ila kwasababu hakuna upinzani imara. Swali hapa ni Itatuchukua mda gani kupata chama cha upinzani kilichokuwa imara kushindana na ccm, na kikiweza kuchukua dola kiwe na uwezo wa kuunda serikali yake bila kuwa na mamluki wa chama tawala.
Uchambuzi yakinifu ndio msingi wa mada.

Nawasilisha

Upinzani imara unaupima kwa kipimo gani. Kama mtawala anajibu hoja za upinzani kwa risasi badala ya hoja ujue upinzani ni imara kuliko unavyofikiri.
Upinzani ungelikuwa dhaifu kusingekuwa na wanasiasa kufungwa kiholela na kutishiwa maisha yao kiholela.
Unachokitaka wapinzani nao wajibu mapigo kwa risasi ili ujue wako imara!?
Unatakiwa uwasifu kwa hekima na uvumilivu wao!
 
Wasalaam wana Jf.
Baada ya mambo mengi yanayotokea juu ya siasa za Tanzania na tetesi zinazoendelea kuwa tusubiri kuyaona makubwa zaidi ya haya Kwa vigogo wa cdm kuamia upande wa pili. Na hili ndio linanifanya nikubaliane na mwana jf mmoja ambaye ameandika kuwa ccm itatawala zaidi ya miaka Mia, sio Kwa kuwa ni chama imara ila kwasababu hakuna upinzani imara. Swali hapa ni Itatuchukua mda gani kupata chama cha upinzani kilichokuwa imara kushindana na ccm, na kikiweza kuchukua dola kiwe na uwezo wa kuunda serikali yake bila kuwa na mamluki wa chama tawala.
Uchambuzi yakinifu ndio msingi wa mada.

Nawasilisha
Tanzania tutapata demokrasia ya kweli pale CCM itapokuwa na kuachia dhana ya kuwa chenyewe ni chama dola chenye kushika hatamu ya kila kitu na chenye hatimiliki ya taifa.

Tanzania itakata minyororo ya ukiritimba wa mawazo mgando yasiyopingwa na yanayolidumaza taifa, pale itapoelewa kuwa siasa za upinzani zinaleta afya

Vyama vya upinzani vitanawiri pale CCM itapokubali kuviacha vikuwe badala ya kutumia vyombo vya dola na rasilimali za nchi kuviangamiza
 
Hujamuelewa huyo jamaa? Watanzania wote kwa ujumla wetu hatuwezi kutegemea kushibisha matumbo yetu naya watoto wetu kwa kutegemea tu ruzuku inayopewa chama fulani cha siasa.so upinzani wa kweli unatoka kwetu wananchi.Jitahidi kujifungua kutoka kwenye box la vyama mkuu
Pengine hilo ndio tatizo, chama cha siasa sio ruzuku ambayo inatolewa ili tushubishe matumbo yetu na ya watoto, Kwa kuwa sio lengo la msingi la chama cha siasa. Chama cha siasa ni kundi la watu (wananchi) wenye mfumo Fulani wa Sera na itikadi yake ambayo inaiuza Kwa wananchi ili ipewe ridhaa ya kushika dola. Chama cha siasa kinajipambanua Kwa Sera na itikadi yake bila kuyumbishwa,
 
Mkuu hawa wafia ccm wengi wao wamefeli ama darasa la saba au form form so wapo karibu sana na ccm angalau watupiwe makombo wajaze matumbo yao
 
Labda kwanza utusaidie tufafanua upinzani ni nini kabla ya kuzungumzia upinzani wa kweli au uogo
2
Mkuu, Sijijui sijafanya utofautishaji Kati ya upinzani wa kweli na upinzani wa uongo, kinachozungumzwa hapa ni kusimamia kile unachokiamini, kuwa muharisia na kujipambanua vyema dhidi ya kile unachohitaji Kwa maslahi mapana ya watu wako.
 
Hahahaha hizi ni ndoto..upinzani wa kweli utatoka wapi bana..??? Kuna binadamu gani asiyetaka kula..akiona huko hapati mkate wake na watoto wake si anaenda sehemu yenye maziwa na asali...nani anataka kufa na njaa..sasa kama mapesa ya ruzuku yanaliwa nawatu wawili watatu, ungekuwa wewe ungevumilia..??? Upinzani unawexa kuwa na nguvu kama serikaii ni dhaifu haitekelezi ahadi zake..lakini ukipata serikali kama hii ya ccm, nakwambia milele hutakaa uende ikulu eti mpinzani...ndio maana kama China waliamua Rais wao aendelee mpaka wananchi watakapoamua vinginevyo..kwa manufaaa ya taifa na sio kwa manufaa ya tumbo la mtu

Mtwara,Songea,MBEYA, Kigoma,tabora,shinyanga kuna miradi IPI inayotekelezwa?
 
Babeli ni buku saba tu unatafuta ama ni udc unatafuta.
Swali gumu la kuuliza siyo "ni lini tutapata upinzani wa kweli" bali "ni lini tutapata serikali ya ccm itakayoheshimu democrasia ya kweli na kuheshimu vyama mbadala kama sehemu ya uongozi wa nchi kama wafanyavyo ulaya?"
Kama alivyosema Mh. Sana January Makamba viongozi waache chuki, waheshimu wengine kama wao wanavyopenda kuheshimiwa.
Viongozi wa ccm wengi wao hawatendi haki, hawaheshimu wengine, hawana utu hata kwa raia wao.Wanadhani wapiga kura hawaoni. Wanadhani wao ni watu juliko wengine. Ni kama kwenye kitabu cha Animal Farm-some are more equal than others!
Unapomnyima binadamu moja haki yake ya matibabu na kumpatia binadamu mwingine 50m na ndege ya serikali bure wote wakiwa raia wako kama vile watoto wako nyumbani, moja akiwa mbishi, mwenye kuhoji kila kitu, mwenye kuchukukia tabia fulani fulani za mzazi wake lakini ni mzalendo labda hata zaidi kuliko huyo mtoto wa pili ila hajui kauli nzuri. Na mtoto mwingine ni mtoto aliye katika nafasi ya kuweza kukupromote, ana kauli nzuri sana ambayo ewe unaifurahia. Kweli mbele ya Mungu au hata mbele ya uma ulio na haki na unaomwogopa Mungu, wanakuonaje iwapo utamwadhibu mtoto wa kwanza kwa adhabu ambayo unajua inaweza hata kupoteza maisha yake??? Na wa pili anayekuwa katika shida iliyo sawa na hiyo ukamtendea ubinadamu wa hali ya juu sana!
Binadamu wote tutarudi udongoni. Kama Ruge! Ruge wengi hatukumjua lakini wema na utu wake umetujulisha yeye ninani. Je serikali zetu hizi kwa mambo wanayofanyia watu walio nje ya chama chao wanatufundisha nini?
Upendo, utu ama chuki?
Democratic Party na Republican Party za USA zote ni vyama viongozi. Moja inaongoza ya pili ni pinzani. Hakuna anayedharau mwenzake. Wanapingana kwa hoja. Wanaamua kukubaliana ama kutokubaliana ! Kuna wanachama wao wanatoa lugha chafu kwa mwingine lakini mwenzake anamjibu kwa ukali huohuo. Hakuna cha polisi wala silaha.
Wanasiasa mliohudhuria mazishi ya kijana mdogo sana Ruge, naomba mjifunze kutoka kwake. Aliweza kuwaheshimu watu wa aina zote, viongozi wote aliwaona sawa, watoke upinzani ama opposition. Hakuna aliyewahi kumsikia hata siku moja akimtukana mtu wala kumwumiza kwa ajili ya tofauti zao.
Badala yake alitafuta suluhu. RIP Ruge. Huyu alikuwa umri wa mwanangu. Lakini ameweza kuwafundisha viongozi wengi, kama alivyosema Mh. January Makamba.
JMakamba nakuombea siku moja Mola akujalie uwe kiongozi wa nchi yangu.

Sasa wewe unataka upinzani wenye nguvu Tanzania. Utatoka wapi wakati watu kama wakina musiba, na wengine wanaruhusiwa watukane lakini wapinzani wanatakiwa wawe bubu????Mola atusaidie!
 
Upinzani wa kweli unatoka moyoni mwa mtanzania tena yule mwananchi wa hali ya chini ..ambaye Kila siku anakumbana na (1)kodi ya kichwa_20000
(2)kurudishiwa korosho kuwa hazina ubora
(3)kutokupewa uhuru wa kujieleza na demokrasia
(4)kutumiwa kwa kodi anayolipa kununua ndege zisizo na manufaa kwake
(5)kuhujumiwa na tume ya uchaguzi inayoteuliwa na chama kimoja ili kukidhi matakwa binafsi ya chama hicho
N.k
Huyo ndo mpinzani wa kweli tunaye mngoja ...
100 mia moja miaka
 
Kwa vyama vilivyopo Tz na mazingira ya play ground ni ngumu,nadhani Ccm hadi chama chenyewe kigawanyike
 
Back
Top Bottom