IST ina tatizo la coolant kutorudi kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank

walcot

Senior Member
Oct 13, 2012
105
22
Habari Wakuu!

Naomba msaada wa kiufundi kwa IST kutorejesha coolant kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank ambayo imekuwa ikimwagika baada ya kujaa. Nimejaribu kubadilisha kifuniko cha rejeta lakini tatizo bado linaendelea.
 
Ungeweka maelezo yenye kujitosheleza ili watu waweze kukusaidia.

Mfano, gari uliponunua ilo tatizo lilikuwepo ama la, na maelezo mengine.

Huyo fundi airudishe hiyo thermostat aliyoitoa.
Gari nilinunua 2017 haikuwa na hiyo tatizo ilianza gafla mwaka jana mwezi wa 7 na wala haichemshi. Kuondolewa kwa thermostat kuna athari yeyote?
 
Gari nilinunua 2017 haikuwa na hiyo tatizo ilianza gafla mwaka jana mwezi wa 7 na wala haichemshi. Kuondolewa kwa thermostat kuna athari yeyote?

Thread zake zimo humu JF, pitia upate elimu.
 
Usifanye masihara na system ya kupoza engine. Kama gari yako inarudisha maji Kwenye tank ya coolant inawezekana itakuwa WATER PUMP IMEKUFA, jaribu kuwasha Kwanza gari yako huku umefungua bonnet alafu kasikilize mlio wa water pump jinsi inavyozunguka na uangalie belts zote kama zipo tight au loose
 
Usifanye masihara na system ya kupoza engine...
Kama gari yako inarudisha maji Kwenye tank ya coolant inawezekana itakuwa WATER PUMP IMEKUFA,jaribu kuwasha Kwanza gari yako huku umefungua bonnet alafu kasikilize mlio wa water pump jinsi inavyozunguka na uangalie belts zote kama zipo tight au loose
Belt na water pump ziko vizuri hata feni inafunguka
 
Thanks kwa ushauri Mkuu, naomba nisaidie aina ya mfuniko mzuri maana nimebadili mara mbili na kuna fundi alidai inasababishwa na thermostat akaitoa lakini tatizo likaendelea
Mwambie huyo fundi arudishie hiyo thermostat haraka sana...hapo utakuja kutengeneza tatizo lingine ambalo ni kubwa zaidi...
Then tafuta fundi mzuri akague hizo njia za kurudisha coolant kwenye radiator huenda zimeziba...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Belt na water pump ziko vizuri hata feni inafunguka
Tatizo ni mfuniko kama ulivyoelezwa apo juu. Nenda kwenye duka wanakouza original toyota radiator cup (bei yake imechangamka kidogo), au tafuta duka wanakouza rejeta used wakutolee mfuniko kwenye izo rejeta wanazouza utakua umetatua tatizo.
 
Usifanye masihara na system ya kupoza engine...
Kama gari yako inarudisha maji Kwenye tank ya coolant inawezekana itakuwa WATER PUMP IMEKUFA,jaribu kuwasha Kwanza gari yako huku umefungua bonnet alafu kasikilize mlio wa water pump jinsi inavyozunguka na uangalie belts zote kama zipo tight au loose
Hajasema maji kasema coolant sijui mnashindwaga nini kuelewa kiswahili? Na kama na wewe ni mtu miongoni mwa wale wanaotumia maji badala ya coolant kupooza engine zao mnakosea na unaua gari bila kujijua kumbuka maji yanasababisha kutu kwenye rejeta! Naishia hapo ila hajasema maji kasema coolant

Duuuu hii ya leo Kali jamani!
Kwa hiyo ina maana hiyo coolant inasukumwa kutoka Kwenye radiator Hadi Kwenye engine Kwa kutumia nini?
Au coolant unapita Kwenye mfumo tofauti na maji?

Wapo wanaotumia maji badala ya coolant lakini mfumo ni uleule mmoja....ninamiliki gari ndiyo maana najua kile nilichosema na pia sijawahi kutumia maji ya kawaida Kwenye gari Yangu zaidi ya coolant Tu huu ni mwaka wa 5 natumia hiyo kitu.

Usidharau mtu usiyemjua sikuzote
 
Thanks kwa ushauri Mkuu, naomba nisaidie aina ya mfuniko mzuri maana nimebadili mara mbili na kuna fundi alidai inasababishwa na thermostat akaitoa lakini tatizo likaendelea
Kutoa thermostat ni kuharibu gari yako kabisa,engine itakua inaoperate under minimum temp.

dodge
 
Back
Top Bottom