Israeli yaelekea kushindwa kuwamaliza na kuwateketeza kundi la Hamas kama walivyoahidi

Israeli yaelekea kushindwa kuwamaliza kwa kuwaua wapiganaji wa kundi la Hamas kama walivyoitangazia dunia.

Ni siku 90 (miezi mitatu) imepita tangu Israeli iingize majeshi yake ya ardhini ndani ya Ukanda wa Gaza huku wizara ya afya ya Gaza ikisema kuwa wapalestina wapato 22,000 wamepoteza maisha wengi wakiwa ni watoto, akina mama na akina mama wengine wakiwa wajawazito.

Israeli kwa upande wao imepoteza wanajeshi wapatao 175 huku wengine wapatao 129 kubaki kushikiliwa na kundi la Hamas.

Israeli ilianzisha kampeni ya mashambulizi ya anga kuwashughulikia Hamas baada ya wapiganaji wa kundi hilo wakitumia njia za juu kwa juu, ardhini na majini kuvunja uzio wa ulinzi na kuwaua raia wa Israeli wapatao 1200. Ilikuwa ni tarehe 7 mwezi wa October pale wapiganaji hao walipovuka mpaka sehemu ya kusini mwa Israeli kwenye mji huo wa Ashkelon.

Umoja wa mataifa umesema wapalestina wapatao milioni 2 wamepoteza makazi yao huku wengi wakikabiliwa na njaa kali. Hata upande wa Israeli katika mji wa Ashkelon wakazi wengi wameachwa bila makazi yaoo baada ya kuteketezwa kwa moto au kuharibiwa vibaya.

Stratejia ya Israeli katika vita hii na Hamas imegawanywa katika hatua tatu ya kwanza au Phase One ilikuwa ni kufanya mashambulizi makali ya anga. Mashambulizi hayo yamefanya uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo hospitali ya Al-Shifa na kuua wapalestina wengi khasa watoto, akina mama na wale wagonjwa na wengi akina mama wakiwa na ujauzito.

Lakini uharibifu wa mabomu katika hospitali kubwa katika Gaza ya Al-Shifa ulisababisha dunia kulaani kitendo hicho cha Israeli kushambulia hospitali hiyo huku jeshi la Israeli likidai kuwepo kwa kituo cha kuongozea mashambulizi ya Hamas yaani "Command Centre".

Mwezi Novemba Israeli ikakubali kusitisha mashambulizi na kubadilishana mateka ambapo Hamas wakawaachilia mateka 80 huku Israeli ikiwaachilia wafungwa wapatao 240 walokuwa wakishikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Israeli. Nje ya makubaliano hayo pia mateka wapatao 25 wa kutoka nchini Thailand ambao walikuwa wakifanya kazi katika mashamba ya Israeli waliachiliwa na Hamas.

Baada ya kipindi cha kusitisha mapigano kuisha, mapema mwezi Disemba jeshi la Israeli likaanza hatua ya pili yaani "Phase Two" ya mapigano kwa kuingiza jeshi na vifaru ndani ya ukanda wa Gaza. Israeli iliita wanajeshi wake wa akiba (reservists) wapatao 300,000 na kuanza vita ya ardhini "Ground offensive" dhidi ya kundi la Hamas.

Hatua hii ndo hatua ngumu ambayo jeshi la Israeli limekumbana nayo ambapo wapiganaji wa Hamas wameweza kufanikiwa kuwaua wanajeshi wengi wa Israeli kwa kutumia njia ya kushtukiza adui "ambush", mjengo kwa mjengo au "urban warfare" na ile ya kuvizia au "asymmetric war" ambayo wapiganaji hawa hujificha katika majengo na kushambulia kifaru kinopita nje.

Ugumu wa hatua hii pia ni kitendo cha wapiganaji wa Huthi wa Yemen ambao wamezuia meli kadhaa ambazo zilikuwa zikipeleka mzigo wa silaha nchini Israeli. Algeria pia ilizuia meli moja ambayo ilikuwa na shehena ya silaha ilokuwa ikielekea Israeli. Marekani ambayo ni mshirika mkubwa wa Israeli imekuwa ikiwasaidia IDF (Israel Defence Forces) kwa kushambulia kambi za makundi ya Hamas na kundi la Huthi na pia kundi la Hezbollah lililoko upande wa kaskazini mwa Israeli kuingia nchini Jordan.

Kwa kuweka meli zake za kivita katika bahari ya Mediterranean, Marekani imeweza kukabiliana na wapiganaji hao wa kutoka Yemen, na pia hata nchini Iraq ambapo ni juzi tu wapiganaji kadhaa wanohusiana na Hamas waliuawa kwa makombora.

Iran ambayo ni wafadhili wakubwa wa makundi ya Hamas na Hezbollah mpaka sasa haijachukua hatua zozote za kujibu mashambulizi ya jeshi la Israeli dhidi ya mmoja wa makamanda wake Saleh Al Arouri. Al Aroui aliuawa pamoja na wapiganaji kadhaa wa Hamas kusini mwa mji wa Beirut kwa makombora. Kwa kujibu wa idara ya ujasusi ya Mossad, Arouri amekuwa akishiriki mipango mingi dhidi ya Israeli likiwemo shambulizi la tarehe 7 Octoba mwaka jana.

Mapema mwaka huu Israeli imeingia katika hatua ya tatu yaani Phase Three ambayo yahusisha vita iso na nguvu sana yaani "low intensity". Hatua hii yaweza kuonekana kuwa ni hatua iso na mwelekeo maalum au ulo wazi au Vague isoweza kusema kama Hamas imemalizwa nguvu zake au bado wana uwezo uleule ukizingatia kuwa eneo la Khan Yunis ambalo majeshi ya IDF yamo kwa sasa bado Hamas wameweza kurusha makombora hivyo kuonekana wana uwezo uleule wa tokea mwanzo.

Khan Yunis ni mji ulioko kusini mwa ukanda wa Gaza na ndio yaaminika kuwepo kwa mahandaki na njia nyingi za chini kwa chini. Pia yaaminika kuwa ndipo walipo mateka wa Israeli wanoshikiliwa na kundi la Hamas.

Pamoja na Israeli kufikia hatua hii ya tatu, bado imewaruhusu wanajeshi wake kurudi makwao kujumuika na familia zao wakionekana kuvuka mpaka wa Israeli na Gaza kurudi Gaza.

Mapema mwanzoni kwa vita hii, waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliahidi kuhakikisha kundi la Hamas likiteketezwa, kuvunja uwezo wake wa kijeshi na pia kuwaokoa mateka wake wote.

Leo hii miezi yaenda minne bado Israeli haijafanikiwa kuimaliza Hamas jambo linohatarisha Hamas kujitangaza washindi katika vita hii na kisha kuendelea na vita vyake dhidi ya Israeli kutokea pande zote za kaskazini na kusini mwa Gaza kwa maana kwamba majeshi ya Israeli sasa hivi yapo katikati ya Gaza (Mji wa Khan Yunis) na yamezungukwa.

Pia hali hii yaonyesha kwamba kunaanza kuonekana uwazi mkubwa kati ya malengo ya Israeli juu ya vita yake hii dhidi ya Hamas na hali halisi ya kinotokea ndani ya uwanja wa vita. Halikadhalika mauaji ya Arouri yanoaminiwa yamefanywa na Mossad (ingawa israeli haijakiri) yamewalazimisha wapiganaji wa Hamas kutoa kauli kwamba "watalipiza kisasi".

Jambo jingine kubwa ni hofu ya kutokea vita kubwa ya mashariki ya kati kati ya Lebanon Hezbollah na Hamas, wapiganaji wa Hauthi, wanamgambo wa Iran walioko nchini Iraq (Islamic Resistance) wenye makao yao makuu mjini Baghdad ambayo ilishambuliwa na makombora Marekani na wapiganaji wa ISIS walioko nchini Syria sehemu ya Bukamal.

Hofu hiyo pia yajiongeza zaidi pale Iran ilipoamua kutuma meli yake ya kivita iitwayo Alborz Destroyer kwenda katika mfereji wa Bab El Mandep ikiwa ni baada ya Marekani kushambulia wapiganaji wa Huthi wa Yemen.

Kwa kutambua hilo, Marekani wamemtuma tena Antony Blinken waziri wake wa mambo ya nje kwenda tena mashariki ya kati kujaribu kuishawishi Israeli namna ya kumaliza vita hii ambayo imekuwa ngumu kwake. Ikumbukwe kuwa bila msaada mkubwa wa Marekani kuzuia wapiganaji wa Huthi, na khasa Hizbollah wasijiingize katika vita hii,hali ingekuwa mbaya kwa Israeli.

Hivyo katika ziara zake hizo (hii ikiwa ni ya nne ndani ya miezi mitatu) Blinken amelenga kuishawishi Israeli khasa wale waisraeli wenye msimamo mkali na wanounda baraza la mawaziri la Benjamini Netanyahu kuachana na wazo la kuwahamisha wapalestina na kuwapeleka katika kambi za wakimbizi katika nchi jirani za kiarabu.

Hizbollah wahofiwa kuwa na silaha khasa makombora yanoweza kufika mjini TelAviv na miji mingine nchini Israeli na kusababisha maafa makubwa khasa miundombinu mingi ya kimkakati. Marekani imejaribu mara nyingi kuweka mapendezo katika umoja wa mataifa ili kuwazuia Hizbullah kutokuwepo mpakani na Israeli mipango ambayo imeshindwa. Mara ya mwisho Israeli kupigana na Israeli ilikuwa ni mwaka 2006 ambapo vita ile haikutoa mshindi.

Israeli leo kupitia waziri wake wa Ulinzi Yohav Gallant wametoa mpango wa kuitawala Gaza kijeshi huku wapalestina wakiishi ndani ya Gaza wakijitawala lakini bila uhuru wa kujiamulia mambo yao. Pia Hamas hawataweza kutawala Gaza,na Israeli itaratibu shughuli zote za kiutawala zitofanywa na uongozi wa Gaza chini ya wapelestina.

Gallant ametoa leo mpango huo uitwao "Vision for Phase 3 of the war" huku ikisemwa kuwa ni mpango aloubuni yeye binafsi na bado wahitaji kusomwa na kupitiwa na baraza la mawaziri na lile baraza la mawaziri la vita au War Cabinet. Hiyo ndo moja ya sababu kubwa Marekani wamemtuma Blinken haraka.

Ni dhahiri kuwa Israeli ipo katika kitendawili kikubwa cha ni namna gani waimaliza vita hii ama kwa kuendelea nayo hadi mwisho au kuishia katikati. Kuendelea kuwepo mjini Gaza kwaleta mfarakano zaidi kwa kuonekana bado waitawala Gaza na wapalestina hivyo kufifisha zaidi makusudio ya tokea mwanzo yanotaka kuwepo na mataifa mawili ya Israeli na Palestina.

Pia kuendelea kwa Israeli kuwepo Gaza ni kuendeleza chuki kutoka kwa Hamas na kuongeza idadi ya wapiganaji wa kipalestina ambao hawataki kuwaona waisraeli ndani ya Gaza.

Hivyo, kidogokidogo hali ya Israeli kushindwa kuhimili vita hii imeanza kujionyesha huku wanadiplomasia kadha wa kadha waliishauri Israeli ianze kufikiria kuondoa majeshi yake kutoka Gaza. Hii yaonyesha wazi kuwa Israeli yaelekea kushindwa vita hii ambayo imekwenda kinyume na mipango yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas.

Tusijeshangaa kuona wapiganaji hawa wa Hamas wakijitangazia ushindi lakini huku wakiendeelelea kupigana hali ambayo itapekelea Israeli kuchukua maamuzi magumu ambayo yatazidi kuifanya itengwe na mataifa mengi duniani.
Habari ndefu sana
 
Ni kweli Hamas wanachapika.

Lakini Israeli hawana uwezo wa kupigana “urban warfare” kama nikivyoeleza.

Ndo maana “ground offensive” yawapa shida.

Hamas wamefunzwa urban warfare, gorilla war na “asymmetric war” vita ambayo ni tofauti na ile vita ya kutupiana mabomu pekee kwa kutumia ndege za kıvita na UAVs na badala yake imeua raia waso na hatia sasa namba yasimama 22600.
Watapigana hivyo hadi lini mamia ya raia wanataabika? Shughuli za kiuchumi zimesimama, watoto hawaendi shule, maelfu wamesongamana kwenye kambi za wakimbizi.
 
wahuthi wa Yemen na Algeria wamesaidia Hamas kwa kuzuia meli za mzigo wa silaha.
Ficha upumbavu wako,
Hao wanaweza kutumia air tu na wakasmugler silaha vizuri tu Israel.
Houthi ni taka tu kwa US na EU wanauliwa asubuhi tu wasisumbue.
10 juzi hapo wametandikwa na wakazikwa humohumo majini waliwe na samaki,we bado unaongea kuhusu houth.
Jinga kabisa
 
IDF haija control Gaza yote still bado wanapambana kuithibiti na usichokijua ni kwamba Hizo rockets zinarushwa kwa kuvizia, mtu anajificha hata chooni anarusha rockets na hata zikirushwa idadi haizidi 20 tofauti na mwanzoni ambapo zilikuwa zinafika mpaka rockets 5000
Vita ni akili haijalishi roketi imerushwa toka wapi, iwe chooni ama hotelini jambo la muhimu adui auwawe.

Haijalishi roketi zirushwe 500 ama 20 ilimradi hizo chache zinazorushwa zimdhuru adui.

IDF wenyewe wanakiri kupoteza ila nyie waswahili mnawakanushia.
 
Mkuu, halikuwa kosa bali walikuwa na uhakika wa backup ya West na Marekani.

Ni wahuthi wa Yemen na Algeria wamesaidia Hamas kwa kuzuia meli za mzigo wa silaha.

Sasa waingia sehemu kama Gaza ilo na uwingi wa watu ni vigumu kuanza “ground operation” ambayo hufahamu alipo.

Backup ya West na Marekani namaanisha matumizi ya satellite kusaidia kufahamu walipo Hamas imeshindikana kwani Marekani kawekwa busy baharini Mediterranean na wahuthi.
Hayo ni maneno yako tu ila haysondoi ukweli kuwa Wayahudi wanadhalilishwa kila kukicha. Walichoganikiwa mpaka Sasa ni kuuwa wakimbizi na kulipua majumba
 
Mbona unaruka ruka kama maarage kwenye chungu mara Hizbollah mara Hamas kaa sehemu moja bas tukuelewe.

Kwa kukusaidia tu IDF inapambana na Hamas hao Hizbullah wanawashwa tu wakiendelea hivyo siku inakuja watakunwa vizur tu kama wenzao wa Gaza.
Mara ya mwisho vita ya Israeli na Hizbula iliisha Kwa mazungumzo ya mezani baada ya kutoa ngoma droo tena ilikuwa vita ya rusha nirushe sio ya kuviziana kama ya Hamas

IDF hafurukuti Kwa Hizbula
 
Nani alianzisha hii vita?next time usimchokonoe simba kwa kijiti, tumia RPG
F-GYNdxWoAAUfGD.jpeg

Simba mavi yanawato, acheni ushoga.
 
Tanzania tulichukua zaidi ya mwaka kumkimbiza Nduli dada, vita ya Dunia zaidi ya miaka mitano kummaliza Hitler, hawa wanaojificha ardhini kama viazi au mihogo na wanavaa hijabu hawana uniform hawana kambi utawamaliza miezi mitatu!!!
 
Hao wanaojiita makamanda wa mahamasi wenyewe wamekimbia na kujificha mashimoni hata ktk tv wanaogopa kujitokeza kwa kuogopa IDF, wkt kina Netanyahu wanatembelea Gaza wanavyotaka.
 
Kwa hiyo unasubiri refa aongeze muda ndo msawazishe? Hamas nao wanaomba muda uongezwe Ili wagonge misumari zaidi
Haya ndo tunawpenda kuyasikia. Acha wabondane hata kwa miaka kumi mwisho wa siku mbabe atajulikana. Mimi na wewe tuagize Pepsi
 
Tanzania tulichukua zaidi ya mwaka kumkimbiza Nduli dada, vita ya Dunia zaidi ya miaka mitano kummaliza Hitler, hawa wanaojificha ardhini kama viazi au mihogo na wanavaa hijabu hawana uniform hawana kambi utawamaliza miezi mitatu!!!
Mkuu, unawafamu uzuri Hamas?
 
Mara ya mwisho vita ya Israeli na Hizbula iliisha Kwa mazungumzo ya mezani baada ya kutoa ngoma droo tena ilikuwa vita ya rusha nirushe sio ya kuviziana kama ya Hamas

IDF hafurukuti Kwa Hizbula
Sasa hivi kuna makundi zaidi ya manne yale yanojulikana rasm ni Hamas, IJ, Hezbolla, na Wahuthi.

Hawa wajiita Axis of Resistance kwenye mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom