Mributz
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 297
- 658
Jeshi la Israel limeanza oparesheni kubwa za kijeshi pembezoni mwa jiji la Gaza hatua inayoashiria maandalizi ya kuutwaa kikamilifu mji huo, huku ikiapa kuongeza mashambulizi kwa lengo la kuzidisha shinikizo la kuachiliwa kwa mateka waliosalia na kulitokomeza kabisa kundi la Hamas.
Hatua hiyo imekosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa na kuzusha wasiwasi kuhusu usalama wa raia zaidi ya milioni moja. Jiji la Gaza ndio kubwa zaidi kwenye ardhi hiyo ndogo ya Wapalestina. Inakadiriwa kuna Wapalestina milioni 1 kwenye jiji hilo.