Israel Sasa inatosha

Israel Sasa inatosha

Mimi nasimama na Israel kwenye mapigano haya, ila tu kwa niliyoyaona Jana naweza kushauri kwamba Sasa inatosha. Nadhani kwa Sasa Israel isistishe mapigano na Hamas maana kwa Sasa wanaoumia sio Hamas ni raia wa kawaida wa Gaza. Kama ni kisasi kimeshalipwa. Maana mpaka Sasa wameuawa wapalestina 11,500. Ambao watoto waliokwisha uawa wanakaribia 5,000 hii inaumiza Sana.

IDF kashamsambaratisha Hamas sidhani Kama Kuna haja ya kuendelea na mashambulizi. Kwa Sasa Hamas Hana nguvu na wapalestina wamejifunza kwamba mbeleni wasifanye uchokozi kwa Israel wa aina ile.

Kuna mambo matatu nimeyaona yamenifanya nifikirie hivyo.

1. Kwanza, Jana Israel kashambulia na kuilipua kwa makombora shule ya watoto na kuua watu hamsini ikiwemo watoto wadogo. Shule hiyo inaitwa Al Buraq, na inasemekana mjukuu wa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa kwenye mashambulizi hayo.

Sababu kuu ya IDF kuishambulia shule hiyo ni baada ya kamanda wa Hamas Ahmed Siam aliyekuwa kwenye mapambano na IDF kwenye eneo la Hospitali ya Rantisi Kuzidiwa na kwenda kujificha kwenye shule hiyo. Hivyo Israel ikaona immalize pamoja na watoto waliokuwemo humo. Kwa kweli niliumia kuona watoto wasiokuwa na hatia wakiuawa kwa ujinga wa Hamas. Nikawaza itakuwaje kwa huko mbeleni?.

2. Pili, Kuna Jambo la kusikitisha kwenye Hospitali ya Al Shifa. Ni kwamba IDF imeizunguka hiyo Hospitali na kuanza mashambulizi. Tatizo ni kwamba Kuna vitoto vichanga karibia 39 vimo humo ndani, ndio kwanza vipo kwenye incubator. Sasa ninachoogopa IDF asije akailipua Hospitali nzima na kuua hao watoto.

Nasema hivyo kwa sababu IDF anaweza kuilipua Hospitali nzima ya Al Shifa kwa kuwa kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kajificha humo pamoja Viongozi wachache waliobakia.

Kingine ni kwamba ndani ya Hospitali hiyo Kuna wagonjwa wengi mahtuti na wazee. Hivyo kuilipua itasababisha mauaji ya halaiki.

3. Tatu, iwapo IDF itailipua Hospitali hiyo Kuna uwezekano wa Mataifa ya kiarabu kulazimishwa kuingilia kati na kuendeleza mgogoro kuwa mkubwa na kupelekwa hata vita vya tatu vya dunia.

Maana Al Shifa imekuwa Kama mtego. Ndio maana Hamas wameruhusu watu wengi wawe pale ili Israel asipate nafasi ya kuishambulia. Maana lile ndio eneo la mwisho kabisa kwa Hamas kujilinda. Hivyo hakuna haja ya kumwaga damu nyingi. Wakubaliane Israel asogee nyuma na Hamas wawaachie mateka basi. Mambo mengine yaendelee.

Hivyo basi, naishauri Israel ifanye yafuatayo.

1. Kutangaza kusitisha haya mapigano, maana wanaoadhirika ni watoto, wanawake na wazee na sio Hamas Tena.

2. Israel atangaze kuwepo na Kambi ya jeshi itakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Kambi hiyo iwe kilometa ishirini kati ya mpaka wa Israel na Gaza.

3. Israel ifanye makubaliano na Hamas ya kuondoka Al Shifa na Hamas wawaachie mateka waliowashika. Na makubaliano haya yasimamiwe na Umoja wa Mataifa.

4. Jukumu la kuisimamia Gaza liwe chini ya Mahmoud Abbas ambaye kisheria ndio Rais wa Palestina, Gaza ikiwemo. Ili kuendeleza makubaliano ya Oslo ya mwaka 1993 ili mchakato wa kuanzisha taifa la Palestine lianze..

4. Nanshauri kuwepo na makubaliano kati ya Palestina kwa niaba ya Hamas na Israel upande mwingine , kwamba hawatovamiana Tena.
1699715313370.png
 
Kabisa mkuu, tena Israel imekuwa ikiitumia Hamas kudidimiza uhalali wa mamlaka ya kipalestina kule west bank na kama mamlaka inayowakilisha Wapalestina wote.

Ikiambiwa izungumze na PA ya Mahmoud Abbas inasingizia hiyo mamlaka haiwakilishi wapalestina wote maana inawatawala west bank tu na haipo Gaza.

Ikiambiwa izungumze na Hamas inasema ni magaidi hawawakilishi Wapalestina wote.

Hivyo uhasama wa Hamas na PLO ya Mahmoud Abbas umetumiwa na Israel kuzima ndoto za Wapalestina kuwa na taifa lao huru.
na Netanyahu amekiri kuiwezesha HAMAS kifedha ili kujiendesha huko Gaza
 
Calendar of Resistance for Palestine! Events and actions around the world

7 October 2023

Everywhere around the world, millions are marching for Palestine. Over 300,000 took the streets of Washington, DC, in the belly of the beast, to stand with the Palestinian people against Zionist genocide. Labourers from Belgium to Japan to Barcelona have refused to load and carry weaponry for the occupation regime, while Block the Boat protests from Oakland to Tacoma have delayed, blocked and confronted US military ships loading war materiel. Palestine Action direct actions are challenging Elbit Systems from Cambridge to Leicester. In train stations, parliamentary and congressional offices and public venues, people are sitting in for Palestinian liberation.

Calendar of Resistance for Palestine! Events and actions around the world
 
Ina maana wanafunzi bado wanaenda shule huko gaza? Sounds really absurd!

Hii hali iliyoko huko ni bora watii lile agizo la kuondoka. Pia waache mikusanyiko kama hiyo.

No, shule hamna. Ila walifichwa hapo ili kuzuia Israel kuishambulia. Sasa makombora yakawa yanatokea hapo. Ndipo Israel kuishambulia bila kujali ni shule.
 
Suala la wao kuendelea au kuacha kupigana hilo ni juu yao mm na ww hatuna maamuzi juu ya hayo.

Lamsingi dunia nzima ime jua ya kuwa jeshi la Israel bila Marekani ni JWTZ iliyo chagamka, kwanza hata hapo nimewapendelea.

Mkuu acha unafiki ile tarehe 7 ulisherekea sana mbona sasahivi unatia huruma nini kimetokea.
 
Sasa Hamas utaidhibitije hali ya kuwa uwaacha hao Hamas badala yake unaenda kushambulia watoto na wanawake?

Hamasi wanawatumia hao watoto na wanawake kama ngao,pia gaza onyo lilishatolewa raia wema watoke so waliobaki ni vibaraka wa hamas acha wauawae tu.
 
Na matanki ya maji waliyolipua yalikua na viongozi wa Hamas ndani yake!?..toka mwanzo wanalipua shule, hospital na kudai kombora la Hamas limepoteza uelekeo,wameshindwa kupambana na Hamas wanabomoa majumba na kuua vichanga

Kwa hivyo Hamas wapo beach wanabarizi mpaka mji unatekwa?
 
Ujinga mtupu halafu ndio mnasema Israel ndio yenye TISS nzuri , wazayuni wameonyesha umbumbu ktk suala la Vita ,Jasusi Bora huwezi kupigapiga hovyo vitoto vichanga na wamama.

Ni Bora ya TISS yetu IPO vema ktk kukabiliana na Chadema kuliko hao mbuzi wa kizayuni.
Bro ebu twende taratibu. Ulitaka ufabyaje wakati hao HAMAS wanalimbilia humo masculinity, Mahospitalini, Makanisani na misikitini. Wao wanarusha makombora wakitokea humo au wanashambulia alafu wanakimbilia humo. Ulitaka Israel waende kuwabembeleza kwa kiwa kuna watoto? Je.wale vija a waliouawa kwenye Tamasha nao walikuwa wanapigana? Ebu bro tumia hiko kichwa kufikiria bro.
 
Kabisa mkuu, tena Israel imekuwa ikiitumia Hamas kudidimiza uhalali wa mamlaka ya kipalestina kule west bank na kama mamlaka inayowakilisha Wapalestina wote.

Ikiambiwa izungumze na PA ya Mahmoud Abbas inasingizia hiyo mamlaka haiwakilishi wapalestina wote maana inawatawala west bank tu na haipo Gaza.

Ikiambiwa izungumze na Hamas inasema ni magaidi hawawakilishi Wapalestina wote.

Hivyo uhasama wa Hamas na PLO ya Mahmoud Abbas umetumiwa na Israel kuzima ndoto za Wapalestina kuwa na taifa lao huru.

Divide and rule,mchezo ushaisha huo israel ndio ameshaipoteza gaza.
 
Hamasi wanawatumia hao watoto na wanawake kama ngao,pia gaza onyo lilishatolewa raia wema watoke so waliobaki ni vibaraka wa hamas acha wauawae tu.
Bora yako ambaye huto kufa.
 
Bro ebu twende taratibu. Ulitaka ufabyaje wakati hao HAMAS wanalimbilia humo masculinity, Mahospitalini, Makanisani na misikitini. Wao wanarusha makombora wakitokea humo au wanashambulia alafu wanakimbilia humo. Ulitaka Israel waende kuwabembeleza kwa kiwa kuna watoto? Je.wale vija a waliouawa kwenye Tamasha nao walikuwa wanapigana? Ebu bro tumia hiko kichwa kufikiria bro.
Toa ushahidi wa hayo unayo yasema.
 
Na matanki ya maji waliyolipua yalikua na viongozi wa Hamas ndani yake!?..toka mwanzo wanalipua shule, hospital na kudai kombora la Hamas limepoteza uelekeo,wameshindwa kupambana na Hamas wanabomoa majumba na kuua vichanga
It seems like u know nothing about war. That is strategic approach kumlazimisha adui aingie kwenye matakwa yako. IDF waliamua kutengeneza scarcity ya mahitaji ya muhimu ili raia watoke kama ambavyo waliamrishwa. Hiyo ni kawaida kwa sababu hata Urusi aliitumia kwa Ukraine
 
Mkuu kila kiumbe hai kitakufa,ila dunia lazima iwe mahali salama kwa kuhakikisha magaidi ya kidini yanauwawa na kudhibitiwa vilivyo.
Kuna ugaidi zaidi ya kuuwa vichanga badala ya kupigana na wanajeshi wenzako?
 
It seems like u know nothing about war. That is strategic approach kumlazimisha adui aingie kwenye matakwa yako. IDF waliamua kutengeneza scarcity ya mahitaji ya muhimu ili raia watoke kama ambavyo waliamrishwa. Hiyo ni kawaida kwa sababu hata Urusi aliitumia kwa Ukraine
Au siyo mtaalam wa war strategy,kwa hiyo ile kupiga hospital haikua kombora la Hamas lilishindwa kufikia shabaha Bali war strategy ya Israel!?
 
Back
Top Bottom