Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,981
Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amemuhukumu mkazi wa Vingunguti, Dar es Salaam, Ismail Ramadhan, kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua mwenzake bila kukusudia wakiwa wanagombania mwanamke. baada ya mshitakiwa kukiri kosa, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuanza usikilizwaji upande wa mashitaka.
Mshitakiwa huyo, kabla ya kuanza na usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka waliomba kumkumbusha mshitakiwa kosa lake ambapo baada ya kukumbushwa alikiri kosa la kuua bila kukusudia.
Baada ya mshitakiwa kukiri alisomewa maelezo ya awali na wakili wa Serikali Mosie Kaima kisha mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Wakili Mosie alidai Novemba 13, mwaka 2015, maeneo ya Vingunguti mji mpya wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Mohamed Kamogela bila kukusudia.
Alidai siku hiyo saa 2, usiku mtuhumiwa walikuwa wanagombania mwanamke ambaye anaitwa Ester ambaye walikuwa wanamahusiano naye kwa muda tofauti.
Wakili Mosie alidai ugomvi huo uliibuka baada ya marehemu kumtuhumu kuwa anaendelea na huyo mwanamke huku mshitakiwa akamueleza kwamba hana tena mahusiano wa kimapenzi na huyo mwanamke.
Alidai wakati wa mabishano hayo marehemu alikuwa ameambatana na watu wanne wakiwa na mapanga ambapo walianza kumpiga mshitakiwa kwa bapa na mapanga hayo.
Akiendelea kusoma maelezo hayo, Wakili Mosie alidai wakati tukio hilo linaendelea kuna mtu ambaye alijulikana kwa jina la Ally rafiki na mshitakiwa akiwa eneo hilo alimrushia kisu ili aweze kujiokoa.
Baada ya kudaka kisu hicho mshitakiwa alikitumia kisu hicho na kisha alimchoma katika mkono wa kushoto ambapo marehemu alikimbia na kuangukia varanda ya nyumba ambayo ilikuwa karibu na eneo hilo kisha kufariki.
Marehemu baada ya kufariki askari polisi walipata taarifa ambapo mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Amana na kisha Hospitali ya Taifa Muhimbili na katika uchunguzi ulibaini kuwa alipoteza damu nyingi.
Alidai askari polisi walikwenda eneo la tukio kisha kuchora ramana na Novemba 16, mwaka 2015 mshitakkwa alikamatwa.
Baada ya maelezo hayo mshitakkwa alikiri kosa la kuua bila kukusudia na Hakimu Joyce alisema Mahakama inamtia hatiani kama alivyoshitakiwa.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mosie, aliomba Mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria kwani mshitakkwa alitumia kisu kumchoma marehemu.
," Marehemu akiwa na wenzake kama walikuwa wanataka kumuua mshitakkwa wangemuua muda mfupi, hawakuwa na nia ya kumuua, hivyo mshitakiwa apewe adhabu kwa mujibu wa sheria," alidai.
Kwa upande wa Wakili wa utetezi, Yohana Kibinda, aliomba Mahakama kwamba mteja wake amekaa gerezani kwa kipindi cha miaka saba ni muda mrefu kwani wakati huo alikuwa na miaka 20.
," Mteja wangu hakuwa na nia ya kumuua marehemu bali alitaka kujiami na kujiokoa kwa bahati mbaya wakati wa purukushani aliweza kuua bila kukisudia
Kwani ugomvi unatokea mshitakiwa hakuwa na silaha, hivyo hakuwa na nia ya kusababisha kifo naomba apewe adhabu nafuu ili aweze kutumikia taifa lake kwani ana wazazi na mtoto mdogo wanamtegemea, "alidai