Bwanamdogo
Member
- Aug 6, 2011
- 66
- 19
Kitendo cha Naibu katibu mkuu wa CuF kulalamikia matokeo ya kidato cha nne eti wanzanzibari wanabaguliwa kwa kuwa katika shule kumi bora ya Zanzibar ni moja tu (Lumumba sekondari) na eti shule nyingi zilizofutiwa matokeo ni za kutoka Zanzibar pia. Mimi natilia shaka uwezo wake wa kufikiri pamoja na kiwango chake cha elimu kwani sidhani kama NECTA huwa wanasahihisha mitihani kwa kuangalia unatoka upande gani wa muungano. Mimi nashauri kama anaona hawakutendewa haki awashauri wanafunzi wakate rufaa NECTA mitihani yao irudiwe kusahihishwa badala ya kuingiza siasa kwenye suala nyeti kama hilo. Nawasilisha
(Source: Nipashe Radio one)
(Source: Nipashe Radio one)