Islam State (IS) wanataka nini Msumbiji?

Jamani lazima tuwe makini Sana, watawala wetu Afrika wanazo mbinu nyingi sana wanapokusudia kuwatendea ubaya wananchi wao. Kuna watu wanaweza kukusanya majambia na kusema kuwa Ni ya waandamanaji. Kuna watu wanaoweza kutumwa kuandamana huku wamevaa kanzu na balagashia na kupigwa picha ili dunia iamini kuwa hao Ni alqaida
Ni kweli tusiwe wepesi wa kuhukumu kwa kile tukionacho kwa macho mawili
 
View attachment 1542429
Mtume mwenyewe anakuambia ameamriwa kupigana kwa upanga na kila mtu mpaka wakubali hakuna Mungu ispokuwa allah wewe ni nani hadi tukusikilize?
Huo ni uongo, mtu aliwaagiza waislam watafute elimu hata uchina huku akitambua kuwa huko uchina hakuna waislam. Hii inaonyesha kuwa Mtume Mohamed hakuwa na shida na makabila wala dini za watu wengine. Ila alikuwa na shida na watu wanaopinga dini ya kiislamu kwa kuzuia watu wasiiamini, kuibeza na kuzuia kuenea kwake. Mtu aliyezuia watu wasiabudu, aiamini na kuieneza alikutana na mkono wa chuma.
 
Ni mambo ya ndani ya msumbiji.
Yanahusu wananchi wa Cal Delgado na Frelimo.
Jimbo hili lina waislam wengi wamakonde.
Ni eneo la kaskazini na linapakana na Tanzania.
Baada ya uhuru frelimo walilitupa na kubagua wa eneo hili.
Hawamo serikalini.
Hawamo jeshini
Mji wao hauna huduma zozote zile muhimu.
Ni eneo maskini zaidi msumbiji.
Jimbo hili sasa limepata Gas kwa wingi lakini frelimo haina sera ya angalau kuwadanganya kwa jimbo hilo kufaidika na rasilimali hio.
Kuna kitu kingine Kina Samora na Mondlane walipo anzisha mapambano ya kuwaondoa wareno basi harakati hizo zilianza Tanzania kupitia eneo hili lenye wamakonde na waislam wengi.
Jeshi la frelimo la ukombozi lilikua na hawa jamaa na tuliwafundisha sisi
Kusini ya msumbiji walikuwepo Ranamo.
Kwa ufupi baada ya uhuru Samora na kundi lao lilianza kuwatoa jeshini wamakonde hawa na eneo ziliko anza harakati ya uhuru likatupwa kwenye dimbwi la umasikini
Hivo hizi ni harakati za ndani kudai usawa na haki ya utajiri wa gas.
Huwezi kundoa Uislam wa asili jimbo hili na kuubandika Isis.
Ni kawaida kumbandika mpinzani wako jina baya ili uungwe mkono na dunia.
Na kwa sababu hizi msumbiji wanaungwa mkono na SA na hata sisi.
Lakini hii ni vita ya ndani. Ni vema wakapatanishwa na kufanya suluhu kwani wanaungwa mkono na watu wao.
Tusiwe na double standard mfano Juba Sudan Ilipo taka kujitenga na Khatoum kwasababu walionewa na wakiwatenga kwa sabaabu wao ni wakristo tukawaunga mkono . Na hatikuwaita magaidi hata johnn Garang alikuwepo UDSM
Lakini hawa wa msumbiji ni magaidi kwa sababu ni waislam hivo sawa kuonewa


Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi hatukuwaunga mkono wapelestina na kufunga uhusiano wetu wa kidiplomasia na Israel?
Wapalestina hawakuwa waislam?

Acheni kutetea maghaidi kwa mgongo wa dini.
Tanzania hajutujawahi kuwaita wapalestina Kama maghaidi hata siku mmoja.

Kifupi tangu vile vikundi vya kutangaza dini kutoka Pakistan vije Afrika Mashaariki na kusini kufanya mihadhara miaka ya tisini ndipo vikundi vingine vya muundo was Kibiti na Msumbiji vikaibuka na balozi za Marekani hapa Tanzania na Kenya zikalipuliwa, vikundi vingine vya kufundisha Martial Arts vikaanza Misikitini na vurugu za kugombana na kutengana misikiti waislam zikashamiri.

Hawaendi wakajiita Sunni wale Ismailia...
 
Back
Top Bottom