Islam State (IS) wanataka nini Msumbiji?

Wakuhurumiwa sana wewe, hujui unachokiongea, unadhani Qur'an ni kama vitabu vingine unatranslate tu utakavyo!!

Uislamu ni dini ambayo inahimiza amani, upendo na uvumilivu

SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

Sala na salamu zimthibitikie Mtume wetu Muhammad Swallallahu Alayhi Wasallam, maswahaba wake watukufu na watangu wema hadi siku ya Kiyaamah.

Neno Uislamu linamaanisha amani kwa Kiarabu. Uislamu ni dini iliyoteremshwa ili kumwakilisha mtu pamoja na maisha yaliyojaa utulivu na amani ambayo yana huruma isiyo na mwisho ya Allah iko waziwazi. Allah anawaita watu kuja katika maadili ya Uisilamu kuwa ndio kigezo ambacho huruma, uvumilivu na amani vinaweza kufanyiwa kazi. Yafuatayo yanaelezwa katika aya 208 ya sura al-Baqara:

“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She’tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.”

Kama inavyoonekana katika aya, Allah anaeleza kuwa usalama wa watu unaweza kuhakikishwa tu kupitia kuukubali Uisilamu na kutekeleza kwa vitendo maadili ya Quran.

Uisilamu unaulinda uhuru wa kutafakari na uvumilivu

Uislamu, ambayo ni dini inayoeleza na kuhakikisha waziwazi uhuru wa kutafakari na maisha, imetoa maamrisho yanayozuia na kukataza kuwekana roho juu, migogoro kati ya watu, kusemana na hata kuwadhania watu vibaya.

Sio tu kutishia na matumizi ya nguvu, Uisilamu unakataza kuweka hata shinikizo dogo kwenye fikra za watu.

“Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu.” (al-Baqara, 2/256)

“Wewe si mwenye kuwatawalia.” (al-Ghashiya, 88/22)

Ni kinyume na maumbile na uhalisia wa Uislamu kuwateza nguvu watu ili waamini katika dini au kufanya ibada. Kwa kuwa, Uislamu umeweka utashi huru na ridhaa makini kuwa ndio sharti la imani. Bila ya shaka, Waislamu wanaweza kuonya na kuhamasishana hivyo wanaweza kutekeleza kwa vitendo sifa za kimaadili zilizofafanuliwa ndani ya Quran. Hata hivyo, hawawezi kutezana nguvu kuhusiana na hilo. Sio sawa kupendekeza vipaumbele fulani vya kidunia ili kumfanya mtu fulani afanye ibada.

Fikiria kuhusu kigezo cha jumuia kilicho kinyume cha mtindo wa hilo. Mathalani, jaalia kuwa watu wanatezwa nguvu kuabudu. Jumuia ya namna hiyo iko kinyume kabisa na Uisilamu. Kwa kuwa, imani na ibada vinakuwa na thamani vinapotekelezwa kwa ajili ya Allah. Ikiwa mfumo wa utawala utawalazimisha watu kuamini na kuabudu, watu watakuwa ni washika dini kwa sababu ya kuuogopa mfumo-tawala.

Kilichokuwa na thamani kwa upande wa dini ni kutekeleza dini kwa vitendo kwa ajili ya Allah katika mazingira huru kabisa.

Allah ameharamisha kuua watu wasio na hatia Kwa mujibu wa Quran, kumuua mtu asiye na hatia ni moja ya madhambi makubwa mno:

“…aliye muuwa mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.” (al-Maida, 5/32)

“Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini – na atakaye fanya hayo atapata madhara,” (al-Furqan, 25/68)

Kama inavyoonekanwa katika aya hapo juu, wale wanaoua watu wasiokuwa na hatia wanaonywa na adhabu kali. Allah anaeleza kuwa kumuua mtu mmoja ni uhalifu mkubwa mno kama kuua watu wote. Haiwezekani kwa mtu anayetii mipaka iliyowekwa na Allah kumdhuru hata mmoja achilia mbali kuua maelfu ya watu wasio na hatia.

Kukwepa haki

Wale wanaodhani kwamba wanaweza kuikwepa haki na kunusurika nayo hawatoweza kukwepa kisasi mbele ya Allah.

Kwa hivyo, waumini wanaojua kwamba watalipiziwa mbele ya Allah baada ya kifo wanatenda mambo kwa uangalifu mno ili kutii mipaka iliyowekwa na Allah. Allah anawaamuru waumini kuwa na huruma.

Maadili ya Mwislamu yanafafanuliwa kama ifuatavyo katika aya:

“Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.” (al-Balad, 90/17-18)

Moja ya sifa muhimu mno za maadili yaliyoteremshwa na Allah kwa waja Wake ili wapate wokovu Siku ya Kiama, rehema Zake na Pepo ni “kuamrishana subira”. Uisilamu, unaoelezwa katika Quran, una muundo wa kisasa, wenye kuelimisha na wa kimaendeleo. Mwisilamu wa kweli anayo haiba ya amani, uvumilivu, kidemokrasia, kitamaduni, utambuzi/usomi, uaminifu, jicho la sanaa na sayansi na ustaarabu.

Mwisilamu aliyelelewa na maadili ya juu yaliyotajwa na Quran anatangamana na kila mtu kwa upendo unaotumainiwa na Uisilamu.
Huu uislam upo nchi gani,
 
Ndipo hapo baadhi ya watu wakaamua kuwa magaidi kweli baada ya kusingiziwa na kutokana na kusingiziwa huko wakapata na manyanyaso pia.
Sasa ukisingiziwa kuwa mwizi,na wewe kwa hasira ukaamua kuwa mwizi kweli,ukikamatwa na mali za watu unataka uitwe nani,
kama siyo mwizi? Huwezi kuwa malaya eti kisa umesingiziwa hicho kitu.inakuwa tabia ipo moyoni,ukigundua umefahamika unatoka mafichoni
unafanya hadharani.
 
Huna mpango wa kuelewa bali una mpango wa kubishana na kwa bahati mbaya sana sina muda huo, am sorry boss!

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Ni nani humu JF anafahamu kwanini Islam State wameivamia Msumbji atujuze. Je, Ni Islam State kweli wanaopigana au ni wananchi wa Msumbiji wenye madai yao kwa serikali yao lakini wakabandikwa jina la Islam State? Yaani Call the dog a bad name then hang it.

Shabaha yao ni Nini na nani na Nani?

Kabla majirani hatujajiingiza humo lazima kwanza tujiridhishe Ni mapigano yenye lengo gani, na je, Ni Islam State kweli?

Call them ISS, Islamic extremists or the likes; their aim is and the reason behind is:-
1. That; they want to expand their influence and presence from there and possibly beyond.
2. That; they want to establish a strong base that would facilitate (1).
3. That; Mozambique army seems to be weaker and this paves way for (2).
4. That the environment in Mozambique provides an easy means for Resources soo needed for financial and military gains and as well as mobilization as these favours (1) and (2)
 
It may be this or not. For sure I do not trust most African leaders. Tulivyopatana wakati tunadai Uhuru kutoka kwa wakoloni sio hivi wanavyotufanyia. Viongozi wa Africa hawataki kukosolewa, hawatendi haki, Ni ving'ang'anizi, wanautumia majeshi yetu kwa manufaa yao na watu wao.

They give their opponents bad names so that they can hang them.
 
Kwanini IS wateke maeneo ambayo Kuna gesi asilia na mataifa mengi km vile China America, Russia eamewekeza hapo?
Wanachofanya hao wamakonde wa eneo hilo hawana tofauti na walichofanya wamakonde wa Tanzania wakati gesi yao inapelekwa Dar es Salaam bila wao kufaidika. Na wanachokipata wamakonde wa Msumbiji hakitofautiani Sana na walichokipata wamakonde wa Tanzania kuhusu madai ya gesi yao. Malalamiko yao yanafanana Sana Kama sio ya aina moja.
 
Unataka kutuaminisha kuwa wamakonde wananyanyaswa hivyo wameamua kudai haki zao!?
 
Umesahau kile kipigo Cha mbwa mwizi walichopigwa kwa kudai gesi? Wamakonde walisahauliwa kwenye keki ya Taifa, ghafla gesi hiyoo!! Ilipogunduliwa wakadhani ahueni imepatikana, Mara wanaona mitaro inachimbwa ya kuipeleka gesi yote kwa wajanja dar.
 
Na hilo ndilo tatizo ambalo litapelekea vurugu kuingia huku TZ, jamii zile ni moja tu. Wamakonde wa msumbiji na Tz wote makatili kabisa ikitokea wanadai haki zao au wakihisi kuonewa. Serikali itazame kwa namna ya kipekee ili kuondoa hiyo kadhia.
 
Sasa nyie mnataka wafaidike vipi hao wamakonde?au gesi iuzwe alafu watu wagawiwe pesa?kwa sababu serikali imeshajenga miundombinu ya kusambaza gesi majumbani yaani kama maji tu .alafu huko mtwara viwanda vimeanza kujengwa?nyie mnataka wafaidike vipi?only relevant answers are needed.
 
Wanachofanya hao wamakonde wa eneo hilo hawana tofauti na walichofanya wamakonde wa Tanzania wakati gesi yao inapelekwa Dar es Salaam bila wao kufaidika. Na wanachokipata wamakonde wa Msumbiji hakitofautiani Sana na walichokipata wamakonde wa Tanzania kuhusu madai ya gesi yao. Malalamiko yao yanafanana Sana Kama sio ya aina moja.
Unataka kutuaminisha kuwa wamakonde wananyanyaswa hivyo wameamua kudai haki zao!?
Umesahau kile kipigo Cha mbwa mwizi walichopigwa kwa kudai gesi? Wamakonde walisahauliwa kwenye keki ya Taifa, ghafla gesi hiyoo!! Ilipogunduliwa wakadhani ahueni imepatikana, Mara wanaona mitaro inachimbwa ya kuipeleka gesi yote kwa wajanja dar.
vurugu zile halikuwa jambo jepesi kama unavyotangaza
 
Ndugu zangu angalieni tofauti ya Ukristo na Uislamu..

UISLAMU..
AT-TAUBA 9:123 :- Enyi mlioamini Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu.

AT-TAUBA 9:73 :- Ewe Nabii pambana makafiri na wanaafiki, na wakazanie.

AT-TAUBA 9:5 :- Na miezi mitakatifu itakapopita, basi waueni washirikina popote mwakutapo.

AL-FURQAN 25:52 :- Basi usiwatii makafiri na pambana nao kwa Jihadi kubwa.

MUH’AMMAD 47: 35 :- Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda.

MUH’AMMAD 47:4 :- Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu.
i.e (MAKAFIRI = WATU WASIO WAISLAMU)

.............

UKRISTO..
MATHAYO 5:39 :- Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu, lakini mtu akupigaye shavu la kuume,mgeuzie na la pili..

Mathayo 11:29 :- Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu..

WAEFESO 6:11-12 :- Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani, Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Wakorintho 11:4,19-20 :- Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye.

......

Ukiangalia hayo maandiko utaona tofauti inayofanya Mabeberu waone ni vyema kuutumia uislamu kwenye kuiba rasilimali hapa duniani badala ya kutu ukristo..
Kwahiyo kwa upande wa ukristo mabeberu wanautumiaje ukristo?
 
Mnaoelewa tuelewesheni tusioelewa ili tuelewe.
Ni kwanini magaidi wanakomaa na kusema wanaitetea dini ya mwenyezi mungu kwa kupitia uislam?
hivi mnaridhiki na kitendo hiki? kama hamridhiki mbona hamuandamani na kuchoma bendera zao
kama ilivyofanyika miaka ya nyuma yalipofanyika maandamano na kuchoma bendera ya marekani kwenye viwanja vya jangwani
kupinga marekani kuivamia iraq?
Itasaidia nini? maana ishakaa vichwani mwa watu(hadi kwa baadhi ya waislamu wenyewe) kuwa gaidi lazima awe muislamu tu na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom