Isiwe furaha ya muda tuu

Isiwe furaha ya muda tuu

Mawakili wetu walikuwa wasikilizaji tu kazi imefanywa na yule sa. Sidhani kama wakili anaweza kufanya kazi za uwakili katika nchi nyingine bila kuwa registered kule. Pia bado hatujaambiwa ukweli halisi mazingira ya kuachiwa ndege yetu ndio maana tumesitisha safari za huko kwa kisingizio cha vurugu
Nimekuelewa vema... Basi acha tu pongezi zangu kwao nisizibatilishe naweza kuwekwa kwenye kundi la watumwa na mabeberu
 
Niwapongeze mawakili walioenda South Africa kupambana hadi kufanikiwa kuirudisha ndege aina ya airbus mali ya serikali ya Jamhuri? Ya Tanzania.. Nawapongeza sana kwakuwa ni nadra sana kutokea mawakili wetu kushinda kesi za nchi hasa nje ya nchi

Angalizo muhimu kwao:
Wasibweteke wakalewa sifa... Hii fungate ya ushindi isiwe ndefu... Wajipange... Hii ngoma bado mbichi sana... Ndege imerudi lakini deni bado liko pale pale na linazidi kuongezeka kutokana na riba
Bwana stein kadhamiria... Hata kama hatakata rufaa south Africa bado kuna mahakama ya Africa anaweza kukimbilia huko na bado kuna mahakama ya haki za binadamu anaweza kukimbilia huko na kusajili upya kesi yake
Ameshalipwa za kutosha na pengine ameshaona hakuna dalili za kulipwa tena hivyo atakachofanya sasa ni kusumbua na kuharibu taswira ya nchi kimataifa...
Hii inaitwa NIGUSE UNUKE.. unamwaga mboga namwaga ugali...
Kipindi hiki cha fungate zitafutwe mbinu za kumalizana na mzungu kiroho safi ILI maisha yaendelee bila hofu... Hapa Tanzania vinapokamatwa vitu kwenye misako ya polisi watu hutangaziwa kwenda kuvitambua vitu vyao
Akikamatwa jambazi sugu wananchi hutangaziwa kwenda kumtambua...

Nina hofu wadeni wetu wanatafutana na kutengeza group za mawasiliano ILI siku mali yetu ikikamatwa popote watoke kila kona.... Tuna nafasi bado ya kulimaliza hili kabla madhara hayajawa mengi
ushauri uliotukuka ambao haupo kisiasa , umenena vizur sana mkuu tena kwa uzalendi na kwa maslahi ya nchi.
 
Washauliwe mara ngapi kuwa kunahitajika majasusi wa kiuchumi.. Hawa ndo wataweza kupambana vizuri na kwa uendelevu makini matukio mengine ya kiuchumi yatupasa kuyasikia tu na si mpk hiyo mijizungu itugalagaze mahakamani
Kwahiyo tuachane na ujasusi wa kisiasa? Chama chetu pendwa si kitakufa kibudu.
 
Niwapongeze mawakili walioenda South Africa kupambana hadi kufanikiwa kuirudisha ndege aina ya airbus mali ya serikali ya Jamhuri? Ya Tanzania.. Nawapongeza sana kwakuwa ni nadra sana kutokea mawakili wetu kushinda kesi za nchi hasa nje ya nchi

Angalizo muhimu kwao:
Wasibweteke wakalewa sifa... Hii fungate ya ushindi isiwe ndefu... Wajipange... Hii ngoma bado mbichi sana... Ndege imerudi lakini deni bado liko pale pale na linazidi kuongezeka kutokana na riba
Bwana stein kadhamiria... Hata kama hatakata rufaa south Africa bado kuna mahakama ya Africa anaweza kukimbilia huko na bado kuna mahakama ya haki za binadamu anaweza kukimbilia huko na kusajili upya kesi yake
Ameshalipwa za kutosha na pengine ameshaona hakuna dalili za kulipwa tena hivyo atakachofanya sasa ni kusumbua na kuharibu taswira ya nchi kimataifa...
Hii inaitwa NIGUSE UNUKE.. unamwaga mboga namwaga ugali...
Kipindi hiki cha fungate zitafutwe mbinu za kumalizana na mzungu kiroho safi ILI maisha yaendelee bila hofu... Hapa Tanzania vinapokamatwa vitu kwenye misako ya polisi watu hutangaziwa kwenda kuvitambua vitu vyao
Akikamatwa jambazi sugu wananchi hutangaziwa kwenda kumtambua...

Nina hofu wadeni wetu wanatafutana na kutengeza group za mawasiliano ILI siku mali yetu ikikamatwa popote watoke kila kona.... Tuna nafasi bado ya kulimaliza hili kabla madhara hayajawa mengi
Taarifa hizi kwamba kesi bado inaendelea umezipata wapi
 
Huyo mzugu hana ubavu wa kupambana na sisi, wako wengi wanaotudai na mpaka wenyewe kwa wenyewe tunadaiana na hatulipani.Mzungu akawaulize wazee wa EAC wamedai mpaka wakaandamana na kulala barabarani lakini wakaambulia virungu na hakuna aliyethubutu kushitaki,sasa huyo mzungu wa Makuyuni aoneshwe ungangari wetu ili akome.
yani hawa ndo wananiumiza moyo manake babu yangu ni mhanga
yani wanateseka kila wiki lazima waende keko kufatilia alafu ni wazee haswa wengine wanatembea kwa miguu kilomita za kutosha manake kugombea mabasi hawawezi
ningekua na uwezi nimwambie mheshimiwa rais awaambie tu hawatalipwa ili wabaki nyumbani watulie manake wengine adi wanaangushwa mabarabarani kugombea mabasi wanapata ulemavu!Hali ni mbaya
 
Ana P. I (prohibited Immigrant) hivyo hawezi kuingia hapa mpaka zuio litenguliwe
Kwahiyo mlifanya hivyo kwakua aliwashinda mahakamani ...ili inaonyesha ni jinsi gani Taifa lenu linapenda sana dhuluma....HII NI HARAMU
 
Hapana mimi sijuwepo nilikuwa kilingeni
 
Watanzania huwa tunalipa deni, baada ya deni kuwa kubwa. Wanaoshangilia tusilipe deni, wanataka riba iwe kubwa na deni liwe kubwa. Deni liko kwenye mfumo was dola, dola ikipanda, na deni linapanda.
 
Liwagu..na wewe unamuamini Msiba kabisaa. Mzungu kaburu hajawahi samehe Deni kamwe. Na kwa taratibu za kisheria kesi inafutwa Mahakamani sio kwa kuambiwa Musiba sijui Msiba. Mawakili Ni wawakilishi tu wa mfungua madai wala sio wenye kesi Hivyo hawawezi kuzuia kesi isifutwe japo wanaweza kushauri. Hivyo kesi haijawahi kufutwa kabisa na tulishindwa kwenye Rufaa mwaka 2018. Tutafute namna kulimaliza hili jambo tusisingizie usaliti Wala mbwembwe zingine.
Lile batamzinga lilikuwa linajiropokea tu.
 
Mawakili wetu walikuwa wasikilizaji tu kazi imefanywa na yule sa. Sidhani kama wakili anaweza kufanya kazi za uwakili katika nchi nyingine bila kuwa registered kule. Pia bado hatujaambiwa ukweli halisi mazingira ya kuachiwa ndege yetu ndio maana tumesitisha safari za huko kwa kisingizio cha vurugu

Uko sahihi mkuu. Hebu fikiria hili: eti umeshinda kesi lakini gharama za kesi pia uzilipe wewe. Kuna mambo hayajakaa sawa lakini bora ndege imerudi.

Honesty (ukweli) ni bidhaa hadimu katika uongozi wa nchi zetu hizi.
 
yani hawa ndo wananiumiza moyo manake babu yangu ni mhanga
yani wanateseka kila wiki lazima waende keko kufatilia alafu ni wazee haswa wengine wanatembea kwa miguu kilomita za kutosha manake kugombea mabasi hawawezi
ningekua na uwezi nimwambie mheshimiwa rais awaambie tu hawatalipwa ili wabaki nyumbani watulie manake wengine adi wanaangushwa mabarabarani kugombea mabasi wanapata ulemavu!Hali ni mbaya

Hili la wazee wa EAC linatisha saana,ni vizuri kuwauliza wenye kumjua na kumuogopa MWENYEZIMUNGU ni nini madhara yake.Kuna mtu anaandika saana jinsi Karma inavyotukula sisi walimwengu.
 
Back
Top Bottom