Isingekuwa Kujitoa CHADEMA na Kujiunga CCM...

Isingekuwa Kujitoa CHADEMA na Kujiunga CCM...

Km kweli unaitakia mema Chadema yko naushauri tafuta hicho kitabu ukisome Kuna ya kujifunza pia ukiacha Kampeni aliyomfanyia Mh Magufuli Dr Slaa Ana hoja nzuri na nzito khs Chadema pia... View attachment 1363659

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani.
Hii ni nje ya mada inayojadiliwa, lakini ni mhimu sana kunyoosha haya mambo.

Utapeli umekuwa mwingi sana siku hizi, kila sehemu na hasa kwenye siasa.

Naangalia 'cover' ya kitabu alichoandika Slaa, inaonyesha "WILLBROD Peter Slaa, PhD."

Swali langu ni kuhusu hiyo 'PhD'.

Slaa anayo PhD? au doctorate ya aina zinginezo zinazotolewa sehemu mbalimbali duniani?

Ukiwa tapeli kwa mambo madogo madogo, kwenye makubwa ndio utakuwa mwenyewe hasa.

Hii inaweza kueleza tabia ambayo amekwishaionyesha kwenye jamii, toka kwenye upadre hadi kwenye siasa.

Anayejua kama Slaa ana PhD, aweke hapa ushahidi huo.
 
Absolutely. Wakati Mwalimu Nyerere anawaambia CCM wakubali na kisha wasimamie ujio wa vyama vingi wengi hawakumuelewa wakidhani anataka kuleta upinzani ambao pengine unaweza kuchukua nchi. Hakua na maana hiyo na "wahusoka" walimuelewa alipokaa nao nyuma ya pazia na kuwaingiza darasani

Hii ilikua ni style yake tangia baada ya uhuru wakati huo kulikua na vyama vingine zaidi ya TANU. Mfano mdogo tu, kwa wenye kumbukumbu mara tu baada ya Mwalimu kufariki kulikua na vipindi kwenye televisheni ya Taifa wakati huo ikiitwa TVT vikionyesha namna watu waliowahi kufanyanae kazi walivyokua wanamuelezea

Vilikua ni vipindi vingi lakini siku moja alikuja mama mmoja akaelezea namna alivyotolewa TANU na Nyerere na kwenda Chama kiitwacho AMNUT huku akipewa maelekezo ya kuinanga na kuisasambua TANU na viongozi wake akiwemo Mwalimu mwenyewe kufikia hata kutaka kukosewa radhi na wazazi wake! Kumbe alienda pale kwa kazi maalum na hakua peke yake! Baada ya mama yule kuongea siku hiyo vile vipindi havikuonyeshwa tena na TVT!

Yule Mzee alikua bingwa na ndie aliyeusuka "mfumo" wa Tanzania. Kwa mfano hua nawaangalia tu watu wanaposema Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Wazanzibari wenyewe na sijui kina John Okelo na Karume. Wengi hawajui maskini ya Mungu nani alikua fundi mkuu wa Mapinduzi yale, ambaye mkono wake wa chuma haukuwahi kuonekana na wengi ya waandishi wa historia wameishia kukariri yale yaliyoandikwa kwa uratibu wa Mwalimu huku mwenyewe akiwa kando tena mbaaali kabisa

Kwa kifupi Mwalimu hakua na dhamira ya kuwaachia wananchi wajichagulie Chama na watu wawatakao waendeshe nchi, si kwa Tanzania Bara wala Visiwani. Na dola ikajifungamanisha na kujivika joho la kijani likiweka watu wake wakiwa na udhibiti kamili katika vyama vyote vya siasa, wananchi wakichezewa michezo ya kuigiza na sinema za kila aina huku wenyewe wakiamini kua mambo ni uhalisia na iko siku "watatoboa" kwa wanaowapigia kura kushika dola! Acha niishie hapa
Kwa hio mkuu unadhani nini kifanyike ili watanzania kuweza kujinasua kutokana na hali hii tuliojengewa na hawa tunaowaita 'waasisi wa taifa' ?
 
Sesten Zakazaka

Umeweka somo gumu kwenye mada hii.

"DOLA" iliyoko juu ya "SIASA"?

Najaribu kuiwazia, muundo wake na inapotoa nguvu zake, nashindwa kabisa kuelewa.

Majeshi/TISS na vyombo vingine, mboana wanatumiwa na kuamrishwa na wanasiasa wa chama hicho hicho kimoja na wakati wowote viongozi wao wanafurumushwa na wanasiasa?

Hii 'DOLA' inaendeshwa na watu gani?

Mbaya zaidi, ukaweka na mfano halisi, wa Marekani - Democrats na Republicans, hivi vyama na wao wanaitegemea "DOLA"!

Ipi/ipo wapi?

Tutaendelea kukuna vichwa juu ya hili.

Kwa sasa siamini uwepo wa hiyo "DOLA". It is a myth!
 
Mkuu Kalamu1, how I wish ingekua ni just a myth. But this is real. The fact that this subject is so confusing ndio mafanikio ya mpango mzima.

Stability tunayoiona nchini(namaanisha tranquility) haipo by chance, imefanyiwa kazi. Vinginevyo mambo "yangeshaharibika" siku nyiingi sana.

Tufungue macho yetu. Tuangaze huku na huku, karibu yetu na hata mbali ya hapo. Kuanzia mtaani kwetu kwenye serikali za mtaa, angazia kwenye taasisi za umma, serikali kuu, halmashauri za miji na majiji, vyombo vya sheria, jumuiya na vyama vya kijamii zikiwemo hata NGOs, vyama vyote vya wafanyakazi, jumuiya za wanafunzi, taasisi za dini, vyama vya michezo na hata vilabu vikubwa vya michezo kama Simba na Yanga.

Kote huko kumejaa watu wanaohakikisha "mfumo' unafanya kazi na kila kitu kina ratibiwa. Chukulia mfano Taasisi moja kubwa ya miongoni mwa dini kubwa hapa nchini uendeshwaji wake unaonekana waziwazi kua unaratibiwa kutokea mahali fulani. Na hata waumini wa dini hiyo wanajua. Pamoja na kutoikubali wanajikuta hawana budi bali kufuata tu. Kwenye vyombo vyote vya habari vikiwemo vya binafsi hasa vikubwa ndio kabisaaa wamejaa

Wanasiasa tunaoona wanaamrisha na kuviendesha hivi vyombo ni kwa mambo yanayokubalika tu na "mfumo", na wakivuka mstari huvutwa mkono. Kwa mfano leo hii kwenye uchaguzi mkuu atokee Rais wa Tanzania kutoka CCM atake kufanya uadilifu, kwenye uchaguzi wa Zanzibar awe kama anawapa Serikali chama kingine kikichoshinda tofauti na CCM(dola) ndio utajua kama kweli Rais anamamlaka ya kila kitu au la! Nguvu inayoongoza mambo kwenye nchi (dola) haitamkubalia, itamdhibiti mchana kweupee

Kwa Marekani ni hivyohivyo pia. Sio kama vyama vyao vinaitegemea Dola bali vyama hivyo ni zao la makusudi (sio bahati mbaya) la Dola ya Marekani. Ila wenzetu wametuzidi weledi kiasi kwamba inaonekana wananchi ndio wanaziweka Serikali madarakani! Kwamba kwa zaidi ya miaka 150/200 ya uhai wa Taifa hilo lenye kusifika kwa "demokrasia" duniani eti imeshindikana kuibuka chama kingine kiundwe na watu wenye ushawishi wa hadhi na pesa(na wapo wengi tu huko)ili na chenyewe kichukue Serikali ni jambo lsiloingia akilini kabisaa

Haingii madarakani Rais Marekani kisha akajiamulia tu kwa kusema "Mimi leo sitaki vita, nataka amani duniani, kwa hivyo majeshi yetu yaliyopo nje ya Marekani yarudi nyumbani". Nakuhakikishia huyo Rais asipoondolewa kwa taratibu za kisheria hata kwa kosa lisilokuwepo basi ataondolewa kwa "njia mbadala" ambazo wenye kuendesha nchi wanazijua the next day!

Hiyo nguvu imekuwepo Marekani miaka yote kama ambavyo ipo Tanzania kwa kipindi kirefu sana ila kwetu tumekosa weledi kiasi cha kujulikana kwa kila kinachoendelea kama hizi cross overs za wanasiasa ambazo naona ni mbinu za ki amateur amateur sanaaa
 
Sesten Zakazaka,
Ngoja nikujibu kwa kifupi tu.

Lakini naomba usinielewe kwa ubaya kwa haya maneno nitakayotumia hapa, kwa sababu naona wewe ni mtu mwenye busara hasa na mwenye akili inayo'charge' kwelikweli kuliko wengi wetu tuliomo humu jukwaani.

Haya yote uliyoandika hapa ni 'dhana' tu; wengine wanaweza kutumia maneno makali kama "figment of imagination" ikiambatana na "conspiracy theory" kem kem.

Naweza hata nikathubutu kwa kusema kwamba upo vizuri sana kwenye eneo hili, kama mwenye kuwa na kipaji juu yake.

Sasa ngoja kidogo niivute akili hii inayo'charge' hasa, kuunganisha "mfumo" (DOLA) ya kimarekani inavyo'control' wapiga kura wa nchi hiyo.

Chaguzi nyingi katika nchi hiyo, pamoja na hizi nyingi zilizoendelea, kama Japan, Ujerumani, Uingereza na kwingineko na sasa hata kwenye nchi zinazoendelea zinaangukia huko..., chaguzi zao kuu utakuta hata nusu ya wananchi wanaoshiriki haifiki katika kuwachagua viongozi wao haifiki!

Najua hapa ndipo 'conspiracy theory' yako inaposhamiri kabisa.

Uamini wangu ni huu kwa Tanzania yetu hii.

Vyama vyetu vya upinzani bado havijajua mbinu za kuwa'engage' wananchi na kupata baraka yao kuwaondoa CCM.

Kilichopo sasa ni kwamba CCM pamoja na uozo mwingi ilionao kwa miaka hii ya karibuni, lakini muundo wake ulioimarishwa sana tokea zamani, huko vijijini, hicho ndicho kinachowabeba hadi sasa.

Muundo wao ni imara sana tokea mashinani na kupanda juu.

Itakapotokea pawepo na chama kitakachoweza kuuvuruga mpangilio huo, na wao wakajiimarisha tokea huko chini, CCM itaanguka vibaya sana bila ya kujali hiyo "mifumo' unayoiongelea wewe.

Dawa pekee ya vyama vya siasa ni kuuvuruga mpangilio wa CCM tokea chini.

Kwa sasa hivi wanategemea tu kuvuruga huko juu, ambako haiwezekani, kwa sababu hao walioko huko juu wameshikilia silaha zote, mabunduki yote na majela yote ya kuwaumiza wanaotafuta kuwaondoa madarakani.

Niliandika hapo juu nitaandika kwa kifupi...najikuta nikiendelea kutiririka tu bila kujifahamu!
 
Back
Top Bottom