KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
CHADEMA ingekuwa katika hali mbaya sana, kama wote waliojitoa ndani ya chama hicho, huku wakielekeza tuhuma zao kwa viongozi wa chama, wangekomaa tu, angalau kwa muda bila kujiunga CCM, watu wengi wangeelewa kwamba ndani ya CHADEMA pana matatizo makubwa.
Lakini hizi juhudi za kukidhoofisha CHADEMA kwa njia hii inayotumika sasa hivi, badala yake inaweza ikawa inawaongezea CHADEMA nguvu.
Kwa hali hiyo basi, juhudi za CCM kukidhoofisha CHADEMA zinafifishwa (diluted) kwa kutokuwa na kutoelewa mbinu sahihi kwa upande wa CCM.
Hao wanaolipwa na CCM humu mtandaoni kuwalaumu Mbowe, 'specifically', nao wanakosa weledi wa kujua kwamba historia ya mabandiko yao humu JF siku zote yanaelekezwa kwenye kumkatisha tamaa Mbowe ili CHADEMA isambaratike.
Sasa hii "Misimamo Rasmi" ndiyo itakayowaaminisha wasiokubali hadaa hizo?
Watu wenye kufikiri watajiuliza, leo itakuwaje huyo anayeiua CHADEMA ashutumiwe kwa vile anatimiza lengo lao?
N.B. Sina 'interest' yoyote na CHADEMA au Mbowe, mbali ya kutetea haki ndani ya nchi yetu Tanzania, na kutamani uwepo wa mabadiliko. CCM sasa basi, inatosha.