Isingekuwa Kujitoa CHADEMA na Kujiunga CCM...

Isingekuwa Kujitoa CHADEMA na Kujiunga CCM...

Mie kwa mtazamo wngu lipo la kujifunza kupitia andiko lake nakushauri jaribu kulisoma narudia tna ukiacha kkubari hongo ya nafasi ya ubalozi na kumpiga Kampeni Mh Magufuli lipo pia la kujifunza ndani yke...

Sent using Jamii Forums mobile app
La kujifunza lipo, nalo ni kwamba njaa ni mbaya! Inahamia kichwani kama ilivyohamia ya huyu Dr. Mihogo
 
Hiyo kali ndio maana CCM itaendelea kuwagawa ili itawale milele tuache ushabiki yani hkn la kujifunza mtaendelea kupokea makapi kutoka CCM km kweli unaitakia mema Chadema yko lazima lazima ukubari chama kilifanya makosa kumpokea Mh Lowasa na Mh Sumaye ilo lipo wazi kbs...
La kujifunza lipo, nalo ni kwamba njaa ni mbaya! Inahamia kichwani kama ilivyohamia ya huyu Dr. Mihogo
tapatalk_jpeg_1581335643965.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mpambano wa vyama kwa sababu vyama havina tena itikadi zinazoeleweka. CCM haijulikani inasimamia na kuongozwa na itikadi gani kama ilivyo kwa baadhi ya vyama vya upinzani

CCM inachotaka inachukua! Inachukua iwe ni "wanachama" iwe ni ushindi nk, inachukua kwa sababu CCM sio kwamba ni Chama Dola bali CCM ndio DOLA yenyewe(tafakari hata usajili wake). Hao kina Balozi Dr Slaa, Dr Mashinji, Mwanakijiji na weengi wengine ambao bado wapo vyama vya upinzani ni watumishi wa DOLA wakitumikia mfumo kwa kadri wanavyoelekezwa

Ajabu ni kwamba weledi ni kama unapungua/ umepungua katika kuyaendesha mambo haya kiasi cha watu wa kawaida kugundua na kuhisi uwepo wa nguvu hii ambayo kikawaida inatakiwa ijifiche sana. Tangia enzi za awamu ya kwanza kwa mfano kulikua na Majaji ambao ni wa kwenye "mfumo" lakini kulikua na weledi wa hali ya juu kutokuwa expose tofauti ilivyo sasa ambapo you can easily spot them

Mwalimu Nyerere alipotoa hoja na shinikizo kwa CCM(dola) kukubali mfumo wa vyama vingi alisema ni muhimu CCM(DOLA) isimamie kuanzishwa kwa siasa hizo ili "iuratibu" mfumo huo yenyewe kabda watu hawajaudai. Mwalimu alikua ni bingwa wa siasa na ndie aliyeusuka 'mfumo" na wengi hawakumuelewa alikua na maana gani aliposema CCM (dola) "iratibu" ujio na uwepo wa vyama vingi

Ushauri wa Mwalimu ulifuatwa ila kwa sasa kinachokosekana ni weledi. Angekuwepo nadhani CCM(dola) ingeshameguka kama "alivyotamani" na kungekua na vyama viwili vikubwa vyenye nguvu sawa vikiachiana madaraka kwa maelekezo kutoka "mahala" na huku kukiwa na stability ya kisiasa na kiusalama nchini. Ni wachache walimuelewa. Mwenyewe aliwahi kusema kua Marekani kuna chama kimoja tu hayo mengine mbwembwe tu

Alimaanisha uwepo wa Republican na Democrat ni uratibu wa Dola na hivyo vyama ndio Dola la Marekani. Ndio maana misingi ya kitaifa ya nchi ile ikiwa ni pamoja na ubabe na ubeberu kwa mataifa mengine uko palepale miaka yote, watawale Democrats au Republicans. Natamani watu waelewe
Nimekuelewa mkuu,
Kwamba hata mwalimu aliporuhusu upinzani nchini hakuwa anamaanisha upinzani per-say. Ila upinzani aliokusudia ni wa CCM kuweza kujikinga na upinzani! kwamba CCM ndio dola na ndio upinzani at the same time. kwamba mwalimu alituchezea akili watanzania!
 
Mkuu labda hujaijua organisation ya CCM. Hata kama unatamani lakini kuitoa CCM madarakani futa kabisa akilini mwako

Inawezekana ukawa sahihi kabisa au kinyume chake ,binafsi nnalia na Mfumo mzima wa Nchi kutotoa nafasi ya Ushindani ulio sawa.Tuna Taasisi zisizo huru kiutendaji,zinazo weza kuingiliwa kirahisi na wana Siasa .

Amaa kweli hii ndio Afrika na maajabu take.
 
Nimekuelewa mkuu,
Kwamba hata mwalimu aliporuhusu upinzani nchini hakuwa anamaanisha upinzani per-say. Ila upinzani aliokusudia ni wa CCM kuweza kujikinga na upinzani! kwamba CCM ndio dola na ndio upinzani at the same time. kwamba mwalimu alituchezea akili watanzania!

Na ndipo walipo shikilia mpaka wakati huu kila uchwao wanaongeza Sheria zenye maslahi kwao.
 
Nimekuelewa mkuu,
Kwamba hata mwalimu aliporuhusu upinzani nchini hakuwa anamaanisha upinzani per-say. Ila upinzani aliokusudia ni wa CCM kuweza kujikinga na upinzani! kwamba CCM ndio dola na ndio upinzani at the same time. kwamba mwalimu alituchezea akili watanzania!
Absolutely. Wakati Mwalimu Nyerere anawaambia CCM wakubali na kisha wasimamie ujio wa vyama vingi wengi hawakumuelewa wakidhani anataka kuleta upinzani ambao pengine unaweza kuchukua nchi. Hakua na maana hiyo na "wahusoka" walimuelewa alipokaa nao nyuma ya pazia na kuwaingiza darasani

Hii ilikua ni style yake tangia baada ya uhuru wakati huo kulikua na vyama vingine zaidi ya TANU. Mfano mdogo tu, kwa wenye kumbukumbu mara tu baada ya Mwalimu kufariki kulikua na vipindi kwenye televisheni ya Taifa wakati huo ikiitwa TVT vikionyesha namna watu waliowahi kufanyanae kazi walivyokua wanamuelezea

Vilikua ni vipindi vingi lakini siku moja alikuja mama mmoja akaelezea namna alivyotolewa TANU na Nyerere na kwenda Chama kiitwacho AMNUT huku akipewa maelekezo ya kuinanga na kuisasambua TANU na viongozi wake akiwemo Mwalimu mwenyewe kufikia hata kutaka kukosewa radhi na wazazi wake! Kumbe alienda pale kwa kazi maalum na hakua peke yake! Baada ya mama yule kuongea siku hiyo vile vipindi havikuonyeshwa tena na TVT!

Yule Mzee alikua bingwa na ndie aliyeusuka "mfumo" wa Tanzania. Kwa mfano hua nawaangalia tu watu wanaposema Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na Wazanzibari wenyewe na sijui kina John Okelo na Karume. Wengi hawajui maskini ya Mungu nani alikua fundi mkuu wa Mapinduzi yale, ambaye mkono wake wa chuma haukuwahi kuonekana na wengi ya waandishi wa historia wameishia kukariri yale yaliyoandikwa kwa uratibu wa Mwalimu huku mwenyewe akiwa kando tena mbaaali kabisa

Kwa kifupi Mwalimu hakua na dhamira ya kuwaachia wananchi wajichagulie Chama na watu wawatakao waendeshe nchi, si kwa Tanzania Bara wala Visiwani. Na dola ikajifungamanisha na kujivika joho la kijani likiweka watu wake wakiwa na udhibiti kamili katika vyama vyote vya siasa, wananchi wakichezewa michezo ya kuigiza na sinema za kila aina huku wenyewe wakiamini kua mambo ni uhalisia na iko siku "watatoboa" kwa wanaowapigia kura kushika dola! Acha niishie hapa
 
Hiyo kali ndio maana CCM itaendelea kuwagawa ili itawale milele tuache ushabiki yani hkn la kujifunza mtaendelea kupokea makapi kutoka CCM km kweli unaitakia mema Chadema yko lazima lazima ukubari chama kilifanya makosa kumpokea Mh Lowasa na Mh Sumaye ilo lipo wazi kbs... View attachment 1365112

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hao uliowataja wapo Chama gani kwa sasa? Na kama ni wabaya mbona wamepokewa ndani ya CCM kwa vifijo?
 
CHADEMA ingekuwa katika hali mbaya sana, kama wote waliojitoa ndani ya chama hicho, huku wakielekeza tuhuma zao kwa viongozi wa chama, wangekomaa tu, angalau kwa muda bila kujiunga CCM, watu wengi wangeelewa kwamba ndani ya CHADEMA pana matatizo makubwa.

Lakini hizi juhudi za kukidhoofisha CHADEMA kwa njia hii inayotumika sasa hivi, badala yake inaweza ikawa inawaongezea CHADEMA nguvu.

Kwa hali hiyo basi, juhudi za CCM kukidhoofisha CHADEMA zinafifishwa (diluted) kwa kutokuwa na kutoelewa mbinu sahihi kwa upande wa CCM.

Hao wanaolipwa na CCM humu mtandaoni kuwalaumu Mbowe, 'specifically', nao wanakosa weledi wa kujua kwamba historia ya mabandiko yao humu JF siku zote yanaelekezwa kwenye kumkatisha tamaa Mbowe ili CHADEMA isambaratike.
Sasa hii "Misimamo Rasmi" ndiyo itakayowaaminisha wasiokubali hadaa hizo?

Watu wenye kufikiri watajiuliza, leo itakuwaje huyo anayeiua CHADEMA ashutumiwe kwa vile anatimiza lengo lao?

N.B. Sina 'interest' yoyote na CHADEMA au Mbowe, mbali ya kutetea haki ndani ya nchi yetu Tanzania, na kutamani uwepo wa mabadiliko. CCM sasa basi, inatosha.

Kujipa moyo ni kuzuri
 
Lazima mkubari hkn jambo mzuri kwenye maisha km kufanya kosa na kkubari kosa kujipanga usirudie tna Chadema mlifanya makosa makubwa kupokea wezi wale...
Kwani hao uliowataja wapo Chama gani kwa sasa? Na kama ni wabaya mbona wamepokewa ndani ya CCM kwa vifijo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima mkubari hkn jambo mzuri kwenye maisha km kufanya kosa na kkubari kosa kujipanga usirudie tna Chadema mlifanya makosa makubwa kupokea wezi wale...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unajadili mada ki shabiki sana mpaka unapoteza point za maana; mara unapost kitabu cha Daktari kama ndo mwarobaini ya siasa za Tanzania.
 
Xhade[emoji848] CHADEMA itadumu miaka mia, kama una hoja za kupinga uwepoo waaa Chadema unajidangaa mwenyewe eeenasmea hivyo

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Ki uhalisia; ccm kama chama cha siasa kimeshapoteza ushawishi wa kichama kama chama cha siasa. Kwasasa wananchi wanazungumzia Magufuli kama ccm kitu ambacho ni hatari zaidi kwa ustawi wa ccm kama chama.. huondiyo ukweli wenyewe.

CHADEMA kama chama cha siasa kimeshaongeza ushawishi kwa wananchi kama chama bila kutaja au kutegemea mtu ili kukibeba CHADEMA kama chama ..na hicho ndicho ukweli wenyewe.

Dola imebaki kua tegemeo na egemeo la kulibeba chama cha mapinduzi kwenye harakati za kisiasa na ndo ukweli wenyewe. Kinachochelewesha ccm kutokubebwa na dola ni watu wanaokiunda dola kua waliandaliwa, kuzaliwa , kulelewa na kukulia kipindi ambacho ccm ndo wanaandaa mfumo husika. Hapa kinachosubiriwa ni hiki kizazi cha watu wenye umri wa miaka 45 kuendelea kuisha katika vyombo vyetu iwapo katiba hakitawekwa sawa; baada ya hapo mtashuhudia kinanachokikumba ccm kama chama.
Kama ukubaliani na hicho jaribu kurejea kwanini ccm imepoteza ushawishi kwa wananchi na hao wananchi wenyewe waliowengi ni mwenye umri wa miaka 18 adi 35.

Watumishi wa dola wenye miaka 18 adi 35 hawakipendi ccm na hawako tayari kukibeba na kibaya zaidi bado hawana maamuzi makubwa kwenye nafasi waliopo.
 
Nmepost kitabu na nmejaribu kuwaeleza ndugu zangu chadema lipo la kujifunza kupitia kitabu hicho ukiondoa Kampeni alizomfanyia Magufuli kwenye kitabu ila lipo pia la somo la kujifunza...
Mkuu unajadili mada ki shabiki sana mpaka unapoteza point za maana; mara unapost kitabu cha Daktari kama ndo mwarobaini ya siasa za Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waje kwa ruhusa ya nani wakati unajua hawaruhusiwi? -
Kila wakati huwa tunasikia CCM imekufa na baadae wanaosema imekufa wanahamia kwenye Chama hichohicho inachosemekana kimekufa.

CCM naiona ikishinda uchaguzi mkuu wa 2020 iwe kwa halali au kwahila. Tuambieni CDM mtatumia mbinu Gani Mpya kuitoa CCM? Mtawatumia USA na nchi zingine za magharibi? Kwani nchi hizo zinataka kuitoa CCM au zinataka rasilimali? Je CCM wakiamua kuwapa watakacho huo huko mnakosemelea hizo rasilimali za nchi Kama madini n. K mtakimbilia wapi kusemelea?

Rudi kwetu wananchi mtupange mpaka tuwaelewe njooni vijijini Huku maana Hatutumii hata social media Huku.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siasa za tanzania na africa kwa ujumla ni ujinga wa kiwango cha lami
 
usije ukamwamini mtu yeyote anayeitwa mwanasiasa hasa ktk hizi nchi zetu za africa na tanznia kwa ujumla
 
Back
Top Bottom