Ishu ya Msuva ni GSM au Mo Dewji nani kuibuka mshindi?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Kumekuwa na tetesi kuwa timu kubwa vigogo hapa nchini za Simba na Yanga zote zinaiwania saini ya straika Simon Msuva.

Msuva yupo nchini tangu mwezi Juni mwaka huu, baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya Al-Qadsiah, ya Saudi Arabia.

Yanga imeripotiwa kurdi tena upya kufanya mazungumzo nae ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la Ligi Kuu Tanzania Bara halijafungwa, hapo Agosti 31.

Endapo Yanga itafanikiwa kupata saini ya Msuva basi ataruhusiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, kuanzia hatua ya makundi.

Simba yenyewe hadi sasa inaruhusiwa na CAF kusajili hadi Agosti 31, huku ikidaiwa kuwa wako katika mpango wa kumsainisha.

JE KATIKA VITA HII NI GSM AU MO DEWJI NANI KUIBUKA MSHINDI
 
Dirisha la usajili CAF linafungwa lini?

Ishu ya Chama baada ya kutoka RS Berkane unaikumbuka?
Usiwe mbishi ndugu rejea ya musonda kwanza alafu ndo njoo uniulize wapi ujaelewa nikufafanulie vzuri na nakuongezea na ishu ya Mudathir Yahya kairejee nayo vizuuuuuri kabisa ujue alianza kutumika lini michuano ya kimataifa. wewe achana na kukazania dirisha limefungwa TU kwani alifunguliwi tena? Chama ishu yake tofauti yeye berkane walishawasilisha jina lake caf ndo mana akuruhusiwa kucheza
 
Kumekuwa na tetesi kuwa timu kubwa vigogo hapa nchini za Simba na Yanga zote zinaiwania saini ya straika Simon Msuva.

Msuva yupo nchini tangu mwezi Juni mwaka huu, baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya Al-Qadsiah, ya Saudi Arabia.

Yanga imeripotiwa kurdi tena upya kufanya mazungumzo nae ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la Ligi Kuu Tanzania Bara halijafungwa, hapo Agosti 31.

Endapo Yanga itafanikiwa kupata saini ya Msuva basi ataruhusiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, kuanzia hatua ya makundi.

Simba yenyewe hadi sasa inaruhusiwa na CAF kusajili hadi Agosti 31, huku ikidaiwa kuwa wako katika mpango wa kumsainisha.

JE KATIKA VITA HII NI GSM AU MO DEWJI NANI KUIBUKA MSHINDI
Mtu wake anaye msimamia Msuva ni mpuuzi Yanga hawana time nae,huyo wanampromote kupitia Yanga may magiant wengine wamchukue ila Yanga kutoka na msuguano wa kipuuzi na huyo mwanamama wamea amua kumuachia mchezaji wake.Japo mwanzo walimtaka ila washaachana nae.
 
Back
Top Bottom