Ishara za Nyakati: Bendera ya CHADEMA yapepea kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,363
FB_IMG_1679487752597.jpg

Hii ndio Taarifa ya sasa kwenda kwa jamii yote Duniani, kwamba hivi ninavyoandika hapa Bendera ya CHADEMA imepandishwa na kusimikwa rasmi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, yaani hivi sasa inapepea juu ya mlima huo.

Ndugu David Kilawila ndiye Shujaa aliyefanikiwa kuipandisha bendera hiyo kileleni hapo.

Sasa kwa kadiri ya maono ya Wadau hili jambo linatajwa kufanana na na lile Jambo la MAMA JUSI watatu walioona nyota iking'aa angani.

Je, kwa maoni yako Jambo hili linaashiria nini?
 
Tanzania tunaonekana watu wa hovyo kwa mambo kama haya, kulikuwa na ulazima gani? Bendera ya Tanzania haitoshi huko? Kila chama kikiweka yake tutegemee mlima kufunikwa na vitambaa badala ya theruji. Aiseee!
 
Nasikitika kuona kijana akijihangaisha na siasa za maji taka badala ya kujikita kwenye uzalishaji mali utakaoweza kumkomboa yeye na familia yake dhidi matatizo ya kiuchumi.

My friend amka kutoka kwenye huo usingizi usije ukakojoa kitandani, hakuna mwanasiasa atakayekuletea kiroba cha unga nyumbani kwako.
 
Watu huwa wanapandisha kanga(vitenge) kwenye mti wakati wa Harusi huko vijijini baadaye inaanza shughuli ya kula biriani, we umepandisha linguo mlimani unaona ajabu gani? Baadaye utalila?
 
Hii ndio Taarifa ya sasa kwenda kwa jamii yote Duniani, kwamba hivi ninavyoandika hapa Bendera ya CHADEMA imepandishwa na kusimikwa rasmi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, yaani hivi sasa inapepea juu ya mlima huo.

Ndugu David Kilawila ndiye Shujaa aliyefanikiwa kuipandisha bendera hiyo kileleni hapo.

Sasa kwa kadiri ya maono ya Wadau hili jambo linatajwa kufanana na na lile Jambo la MAMA JUSI watatu walioona nyota iking'aa angani.

Je, kwa maoni yako Jambo hili linaashiria nini?
Hii alama ya ukombozi mpya wa kifikra ili kuondoa ile alama ya mwanzo iliyowekwa na mwenge katika kilele hicho cha Kibo kupitia fikra potofu za waganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom