Ishara za Kuanguka na Kusambaratika kwa Serikali na Sisiemu ya Jakaya Hizi Hapa!!!!

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
Sources: Magazeti ya Mwananchi ya Jumapili 28, Novemba, 2010 na Tanzania Daima ya Jumapili, 28, Novemba 2010:

(1) Mwananchi: Wabunge 20 wa sisiemu ni batili, wakiwemo Waziri Mkuu, Spika na Naibu wake, na mawaziri kadhaa- kesi ziko mahakamani-hawamo kwenye katiba!!!!!!!!!!!!!!!Baadhi yao tayari kesi zimefunguliwa mahakamani kwa madai kwamba majimbo husika waliojiandikisha walinyimwa haki ya kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua wawakilishi bungeni!!!!!!!!!hivy chaguzi zifanyike kwa kuwa hazikufanyika!!!!!!!!!!!!!!Waliowateua ni wana sisiemu wasiokuwa katika daftari

(2) Tanzania Daima: Mpasuko mpya Sisiemu!!!!!!!!!!!!!!!Kama alivyosema na kusababisha kukolimbwa yule jasiri kwamba sisiemu imepoteza mwelekeo-sisiemu sasa haina mwenyewe zaidi ya kumilikiwa na mafisadi papa kwa malengo yao ya kifisadina kimafia kuimilikisha taifa hili kwa nchi ya Iran kupitia mikono ya RA, na stooges wake JK, AC, EL, wakiongoza wengine wadogo waliojificha katika migongo ya hawa mapapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Si muda mrefu ujao sisiemu inakwenda kuanguka chali kama mende na kusambaratika kama KANU ya mzee wa mama ngina!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Laana ya Mungu tayari imeanza kuwatafuna kutokana na wao kunyonga haki za Watanzania kwa nia njema na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa 31.10.2010????????????????????????? Ni dhuluma isiyokuwa na mfano wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mawaziri 16, wabunge 20 mahakamani
Sunday, 28 November 2010 11:17

Waandishi wetu
SERIKALI mpya ya Rais Jakaya Kikwete iliyoanza kazi rasmi baada ya kuapishwa jana, ipo katika majaribu kutokana na mawaziri wake 17 kufunguliwa kesi mahakamani kupinga matokeo yaliyowapa ushindi kwenye nafasi za ubunge.Jana Rais Kikwete aliwaapisha mawaziri wake wapya 50, Ikulu, jijini Dar es Salaam ambao atafanyakazi nao katika ngwe yake ya mwisho ya miaka mitano akiwa rais.

Mbali ya mawaziri hao, kimbunga hicho cha kisiasa huenda kikawakumba wabunge 20, ambao tayari wamefunguliwa kesi mahakamani kupinga ushindi wao.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, umebaini kuwa matokeo ya ubunge yamepingwa na waliokuwa wagombea kutoka vyama mbalimbali, kwa madai kuwa uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu ulijaa dosari, ikiwamo ukiukwaji wa sheria.

Mawaziri watakaokumbana na sekeseke hilo pamoja na majimbo yao katika mabano, ni Naibu Waziri wa Ajira na Vijana, Makongoro Mahanga (Segerea), ambaye amefunguliwa kesi na aliyekuwa mgombea wa Chadema katika jimbo hilo, Fred Mpendazoe; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (Mtama), ambaye amefunguliwa kesi na aliyekuwa mgombea wa NCCR-Mageuzi, Worfam Ndaka.

Wengine ni Mbunge wa Newala, George Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), ambaye Chama cha CUF kimefungua kesi kupinga ushindi wake; pamoja na Wiziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini.

Mwingine anayepingwa ushindi wake ni Christopher Chiza, Mbunge wa Buyungu Naibu Waziri wa Kilimo, ambaye Chama cha NCCR-Mageuzi kimeapa kwenda mahakamani kupinga ushindi wake.

Waziri mwingine ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu ambaye ni Mbunge wa Hanang mkoani Manyara.

Mbunge wa Viti maalum, Wilaya ya Hanang, Rose Kamili ambaye anapinga ushindi wa Nagu, aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa anasubiri ushauri wa kisheria kutoka makao makuu ya Chadema kabla ya kwenda mahakamani.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godluck Ole Medeye ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, matokeo ya ushindi nayo yanapingwa na mgombea wa Chadema, Matias Ole Kisambo.

Habari zinaeleza kuwa tayari maandalizi ya kufungua kesi hiyo yapo katika hatua za mwisho na kwamba wakati wowote atakwenda mahakamani.

Ole Kisambo aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa tayari amefikisha maombi ya kupinga matokeo kwa wakili wake na makao makuu ya Chadema ili kuona msingi wa kesi kabla ya kufikisha mahakamani.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyepita bila kupingwa naye ameingia katika sekeseke hilo pamoja na mawaziri wengine waliopita kwa mtindo huo katika majimbo yao kutokana na Chama cha DP, kuazimia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa.

DP inayoongozwa na Mchungaji Christopher Mtikila imeeleza kuwa kitapinga ushindi huo walioupata kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi uliopita kwa madai kuwa sio halali, huku kikieleza pia nia yake ya kuifikisha Serikali mahakamani.

Mwenyekiti wa DP, Christopher Mtikila, alieleza wanahabari katika mkutano nao kuwa wiki ijayo chama chake kitafungua kesi hizo.

Mbali na Mizengo Pinda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Katavi,mawaziri wengine wengine watakaopingwa na DP ni Profesa Anna Tibaijuka, Mbunge wa Muleba Kusini ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Profesa Mark Mwandosya,Mbunge wa Rungwe Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Maji; na William Ngeleja wa Jimbo la Sengerema ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini.

Wengine ni Philip Mulugo (Singwe), Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi; na William Lukuvi (Ismani), ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).

Wamo pia Celina Kombani (Ulanga Mashariki), ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria; Gregory Teu (Mpwapwa) ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi; pamoja na Ezekiel Maige ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.

Pamoja na mawaziri hao, Spika wa Bunge Anne Makinda (Njombe Kusini); na naibu wake, Job Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa, wanapingwa na DP.

Wabunge wengine waliopita bila ya kupingwa ni , Christopher Ole Sendeka (Simanjiro); January Makamba (Bumbuli); Nimrod Mkono (Musoma (Vijijini); na Deo Filikunjombe (Ludewa).

Filikunjombe amepingwa na Menrad Mtitu akidai fomu zake zilikataliwa na msimamizi wa uchaguzi baada ya kudai kuwapo mtu mwingine aliyetumwa na Chadema kuwania ubunge.

Kabla ya kuingia katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, CCM ilipata wabunge 21 waliopita bila kupingwa na madiwani 236 nchi nzima.

Wabunge ambao ushindi wao unapingwa mahakamani, ni pamoja na Mbunge wa Mwibara wilayani Bunda, Kangi Lugola kupitia CCM, ambaye ushindi wake umepingwa mahakamani na mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kupitia Chadema, Chiriko David.

Kesi hiyo ya rufaa namba 7/2010 imefunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ambapo mgombea huyo anadai kuwa uchaguzi jimboni humo haukuwa huru na wa haki.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 jimbo hilo lilikaa miaka minne bila ya kuwa na mbunge kutokana na aliyekuwa mgombea wake kupitia TLP Mtamwega Mugaywa kufungua kesi mahakama Kuu Kanda ya Mwanza akipinga ushindi wa mbunge wa CCM, Charles Kajege ambaye hata hivyo alishinda kesi hiyo na kurejea bungeni.

Akizungumza jijini Mwanza, Chiriko David alisema mgombea huyo wa CCM, akiwa katika kura za maoni za CCM alitumia rushwa, ikiwa ni pamoja na kutumia gari la Ubalozi kugawa pembejeo za kilimo kwa wapiga kura.


Wakati hali ikiwa hivyo katika Jimbo la Mwibara, katika jimbo la Magu wilayani Magu aliyekuwa mgombea ubunge wa UDP, Julius Ngongoseke amefungua kesi akipinga matokeo ya Ubunge yaliyomtangaza mshindi mbunge wa CCM, Dk Festus Limbu.

Mbali na Limbu, pia matokeo ya Ubunge katika Jimbo la Busega yaliyomtangaza mgombea wa CCM, Dk Titus Kamani pia yamepingwa baada ya mgombea, Jacktas Katinde (Chadema), naye kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Mwanza.

Akielezea kesi hiyo, mgombea huyo Katinde alisema amefungua kesi hiyo akilalamikia matokeo ya uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Busega ambayo yalimpatia ushindi mgombea wa CCM, Dk Titus Kamani.

Akizungumza na gazeti hili, Katinde alisema kesi hiyo imefunguliwa Jumatatu iliyopita kwa lengo la kuitaka mahakama hiyo kutengua ushindi wa CCM kwa madai ya kutumika kwa rushwa ya pombe, nyama pori ya nyati pamoja na kutumia gari la Serikali, wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Katika kesi hiyo namba 9/2010, imedaiwa kuwa ushindi wa Kamani siyo halali kutokana na kushinda kura za maoni kwa kutumia rushwa dhidi ya wapinzani wake, akiwamo aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dk Raphael Masunga Chegeni wa CCM.

Kesi hiyo imekuja siku chake baada ya mpinzani mwingine katika Jimbo la Magu Mjini, Julius Ngongoseke wa UDP kufungua kesi No 8/2010 akilalamikia kuporwa ushindi wake, na kwamba anaiomba mahakama itengue mara moja ushindi wa Dk. Festus Limbu.

Wabunge wengine ambao ushindi wao unapingwa ni pamoja na Murji Mohamed wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CCM, Juma Njuayo wa Jimbo laTandahimba,kupitia CCM ; Zubeir Mtemvu (CCM) mbunge wa Temeke, Esmail Abdulkarim wa Mafia na Richard Ndassa wa Sumve, ambapo Chama cha Wananchi CUF kimesema tayari kimeanza mchakato wa kupinga matokeo katika majimbo hayo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Siasa wa CUF, Mbarara Maharagande, tayari chama hicho kimefungua kesi kupinga matokeo katika Jimbo la Mtwara Mjini na kwamba wanakamilisha taratibu ndogondogo katika majimbo mengine matano waliyoyataja.

Miongoni mwa sababu zinazotolewa na CUF ni pamoja na kutofautina kwa matokeo ya vituoni na yale yaliyopelekwa katikaTume ya Uchaguzi kwa ajili ya majumuisho.

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Sumve, Julius Samamba alidai kunyang'anywa ushindi katika jimbo hilo akidai matokeo yaliyokuwapo katika vituo vya kupigia kura yalikuwa na tofauti wakati wa majumuisho.

"Mfano katika vituo sita, niliongoza na kumuacha mbali sana mshindani wangu, lakini wakati wa majumuisho, matokeo yale yalionyesha kuwa mimi nimeshindwa na Ndassa wa CCM kuibuka mshindi," alisema.

Kwa upande wa NCCR-Mageuzi, wao wamesema wanapinga matokeo katika majimbo matatu ya Kawe, Babati Vijijini na Moshi Mjini. Halima Mdee wa Chadema aliibuka kidedea dhidi ya mgombea wao, James Mbatia katika Jimbo la Kawe, wakati Babati Vijijini, Jitu Soni alishinda.

Mgombea Ubunge Moshi Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Faustine Sungura amefungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Philemon Ndesamburo akidai ushindi wa mbunge huyo ulikuwa batili.

Katika kesi hiyo ya uchaguzi namba 1/2010, Sungura amemshitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mlalamikiwa wa kwanza na Ndesamburo ambaye ni mbunge kupitia Chadema akiwa kama mlalamikiwa wa pili.

Ndesamburo aliibuka mshindi baada ya kupata kura 28,697 akifuatiwa na Justine Salakana wa CCM aaliyepata kura 16,972.

Aliyekuwa mgombea wa CCM katika Jimbo la Arusha Mjini, Dk Batilda Burian naye anatarajiwa kumfikisha mahakamani Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, Godbless Lema.

Kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Arusha, imefikishwa kwa wakili, Alute Mungwai na tayari baadhi ya mashahidi wa mgombea huyo wa CCM juzi walikuwa wanakamilisha taratibu za mwisho kufungua kesi hiyo.
Aliyekuwa mgombea wa Chadema katika Jimbo la Tarime, Mwita Mwikwabe, naye yupo katika maandalizi ya kupinga matokeo ya ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Nyambari Nyangwine.

Katika Jimbo la Rorya, aliyekuwa mgombea wa Chadema, Martin Ndira anakwenda mahakamani kutaka mahakama itengue ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Lameck Airo.

Majimbo mengine ambayo wabunge wake ushindi wao unapingwa mahakamani ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, ambaye amefunguliwa kesi na Ally Alfan Mlee katika Mahakama Kuu ya Tabora.
Mbunge mwingine ambaye ushindi wake umepingwa mahakamani ni Stevene Masele wa Jimbo la Shinyanga Mjini na aliyekuwa mgombea wa Chadema,Philipo Shelembi.

From: Mawaziri 16, wabunge 20 mahakamani
 
Mshahara wa dhambi ni mauti!!!!!!!!Watavuna walichopanda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Hasira na chuki halisi ya Watanzania wanaolilia kura zo zilizochakachuliwa sasa zinaelekezwa kwenye kesi hizi kiasi kwamba haitakuwa rahisi kuhongeka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom