Is Tundu Lissu a Moderate?

Nimesikiliza,Nimeelewa na Nikashangaa sana....
Yana sentensi moja aliyosema Lissu inayo endana na headline yako tafadhari ...
Ni wakati sasa MOD muifanye hii website paid subscription ... maana kila mtu anapost utopolo tu ...
 
Maswali ya kijinga!
 
Umeandika pumba, karudie mahojiano yake tena na usipoelewa ni afadhali ukaomba kuelimishwa.
 
Eeenh Heee, mkuu 'andoza', hivi kweli kazi uliyofanya hapa inastahiri kupewa ujira wowote kwa kuifanya?

Utakwenda kabisa kudai uliweka mchango wa mawazo kuhusu/kupinga alichokisema Lissu katika mahojiano hata bila ya kueleza umepinga nini?

Nyinyi watu, hizi shule zenu zinatia hasara kubwa taifa hili. Yaani hata wewe utadai unacho cheo huko serikalini au ndani ya chama, na mchango wako kama huu hapa unahesabika ndiyo kazi uliyoajiriwa kuifanya?

Mbona taifa linapata hasara kubwa hili!
 
Mwakajoka alipewa ubunge kwa sababu alivunjwa mkono na Pccm ..... Kila aliposimama Alikuwa akiunadi mkono..
Mkono huu ...mkono huu...mkono huu

Labda yaweza kutokea Hivyo kwa TAL
 
Lissu ni muumini Mzuri wa utawala wa sheria...na ndicho anachokisimamia leo na milele.

Ni kiongozi mzuri na watanzania wanamkubali....
Matatizo ya wa Tanzania ni uchumi.
Ataleta Telex ngapi kwa wachimba dhahabu? Ataleta akina Lazier wangapi kwenye Tanzanite?
Atajenga mabwawa ya umeme wapi na kwa pesa IPI?
Kiwanda cha chuma , cement na vigae atazalisha Tani ngapi?
Kwenye kilimo atafungua viwanda vingapi vya mbolea na soko la chakula ataliwezeshaje?
Haya ni maswali yanayohitaji majibu.
Asituzuge na porojo za wanasheria.
 

Kwa maelezo yako nahisi hauna ufahamu mzuri wa maana sahihi ya mtu kuwa ‘moderate’.
 
Sera ni za chama sio za lisu hata magufuli hana sera yoyote bali ccm ndiye mwenye sera
 
Hata hivyo kipindi cha kampeni hakijaanza. Mambo yote yatakuwa bayana
 
Ndugu yangu,Laiti ungelijua msingi wa swali langu na kuelewa mantiki yangu na wewe ungeuliza swali hilo hilo.Kama umemsikiliza Tundu Lissu vizuri kwa aina ya maswali na aina ya majibu utaona kwa nini nimeuliza swali hili la muhimu na ni kwa nini ni muhimu uelewa kama TAL ni moderate.

Subiri baada ya matokeo uje uusome huu uzi utakuwa umeshaelewa
 
Wewe unauliza majibu. Lissu anafaa kuwa rais mara 16 zaidi ya magu. Ni mtu ambaye ni competitive kabisa amesoma akaelimika na ni jasiri. Kuna mambo mengi mno yamepindishwa nchi hii Lissu atayanyoosha.
 
ccm wote mmeshajiona hamna uwezo wa kuwa rais isipokuwa dingi yenu pekee, sishangai kuona ungependa mtu anayeabudu madaraja ndiye ashike nchi kuliko mtu anayependa haki.
Hakika kukosa haki/uhuru ni kama kuishi jela. Hatupendi tuishi jela kwenye nchi yetu wenyewe.
 
Kwahiyo utawala wa sheria ndo utatuondoa kwenye umaskini.
Ndio mkuu, vyombo vya habari vitakuwa huru kuibua ufisadi serikalini ili uchukuliwe hatua. Bunge litakua huru kuisimamia serikali bila hofu ya "mashangazi kuvunjwa viuno". Mahakama zitatenda haki sio kuwaachia mafisadi kisa tu ni CCM na kufunga wale tu wanaokuwa upinzani. Bajeti itatakelezwa kma ambavyo pesa ilipangwa bungeni bila kona kona za kufuja pesa za mfuko mkuu wa serikali.

Kiufupi kwa tafiti lukuki zilizofanyika kuna uhusiano mkubwa kati ya utawala wa sheria na maendeleo. Nadhani mifano hai unayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…