Mie nashangaa! sioni tatizo hapa, jee tatizo ni nini? ni Hemed kumuona Lowasa? au Lowasa kuwaandikia psrc? na nnadhani Lowasa ameweka wazi kabisa kuwa sheria zifuatwe. Bado nnashangaa tatizo ni nini?
Sidhani kwa wale wanaosema kuwa awamu hii itaimaliza nchi walikuwepo wakati awamu ya kwanza inang'atuka, kwa kuwakumbusha tuu, hakuna awamu iliiwaacha nchi hii kavu na kwenye umaskini mkubwa kama awamu ya kwanza, awamu ya msifiwa nyerere.
NYERERE alivyong'atuka, benki kuu iliwashwa moto na kaikubakishwa hata dola moja ya kufutia machozi, Jee mnakumbuka? NYERERE alivyong'atuka,tulikuwa hata mafuta ya kwenye gari hatuna kwa kuwa tulikuwa hatuna fedha za nje za kununulia, kumbuka mzee ruksa alivyochukuwa nchi aliwaita wazee wa dar pale diamond akawaelezea kuhusu hili na ikambidi atumie mbinu za haraka za kwenda kuomba libya na imf na iran na kwingineko (hotuba ya mikuki miwili, mzee ruksa diamond.
Yaani hatukumbuki tulivyokuwa tunapangishwa foleni za unga, mchele, sukari, sabuni,viwembe, viberiti. KWA KIFUPI HATA WEMBE WA KUNYOLEA ilIkuwa hakuna BILA FOLENI
Nadhani wengi mnaoandika humu kusemasema hovyo, kama hii mada ya Lowasa, hata sijui tatizo nini? Nadhani wakati wa nyerere mlikuwa hampo au kwa waliokuwepo na wanachangia habari hizi zisizo na mantiki, basi ni wafupi wa kumbukumbu.
Sasa jamani mbona yeye (nyerere) hatumsemi alivyotuwacha pabaya kiuchumi! tunamsifu tuu?
Hebu waacheni hawa kina lowasa na kikwete wafanye vitu vyao, JEE, kwa ukweli wenu kabisa hamuoni kazi wanayoifanya? au ni chuki tuu za kibinafsi?[/QUOTE]
Mmh! Umenifanya niache shughli zangu ni respond maana umenitia hasira 😡 Hivi unalipwa kuja kutetea mabosi wako hapa?
Haya sasa kuwa makini:
1. Kwenda kumwona PM - mfanyabiashara yoyote ana haki ya kumwona PM lakini kama proposal yake haikukubalika na mawaziri na PSRC, kwenda kumwona PM na kuandikiwa kinoti ina maana wameshinikiza! Tusijifanye hatujui maana ya vinoti vya mabosi!
Kitila Mkumbo ameuliza swali zuri kwa nini alisema 'katika sheria zilizopo' kwa kiingereza within the law? Angesema 'accordng to law' yaani kufuata sheria. Sentensi hii ina maana 'piga ua - make the glove fit!' WE are masters at deciphering messages Bongo.
2. Kumsifu Nyerere na kusahau mabaya - hakuna aliyesahau uchumi ulivyoathirika under Nyerere, lakini watanzania wamemsamehe! Unajua kwa nini? Kwa sababu he was honest, he tried his best, what he thought was best. na alipoondoka madarakani akakiri makosa yake! Sasa hawa watawala wa sasa - they are no sincere wanawaza tumboni street. And FYI, free market economy was not MWinyi's invention, not Mkapa's invention and DEFINITELY not JK or EL invention. Shinikizo ilitoka mwisho wa miaka ya 80 after collapse of Communism, kutoka World Bank IMF na donors, kwamba Tanzania lazima ifungue milango. Nyerere alikataa lakini akaona hataweza kuendesha nchi hivyo alijiuzulu! If EL or JK is half the man that Nyerere is, basi na wao wajiuzulu!
3. Hatuoni kazi wanayofanya JK na EL - kwa taarifa yako according to latest poll iliyotayarishwa na 'mshikaji' wa JK more than half of Tanzania hawaoni kazi wanayo fanya. In fac approval rating ya EL ni 5.9%! Utajiju! Watanzania in fact wanaona kazi wanayofanya - ya kuiba nchi, ufisadi na kusafiri kwa pesa nyingi ya walipa kodi. Hivi umewahi kwenda nje ya Dar au unaendesha maRange Rover mliyojipatia kupitia ufisadi? Nenda hapo Chalinze tu nje kidogo utaona maisha halisi ya mtanzania!
Tafadhali acha kutetea bila kufikiri. If things are going well it's only for you! Mpaka watu kutoka nje wameshtuka tuna hali mbaya ya kiuchumi we unakuwa kama waziri wa ulinzi wa Iraq under Saddam! Usanii tu, alafu unafikiri you are a spin master.
Kwa taarifa yako hakuna chuki binafsi hapa, in fact watu wengi walikuwa wanamsupport sana Mungwana lakini ukweli ni kwamba ametuangusha watanzania! EL ndiyo hata tusieme....