Dua
JF-Expert Member
- Nov 14, 2006
- 3,229
- 662
Mie nashangaa! sioni tatizo hapa, jee tatizo ni nini? ni Hemed kumuona Lowasa? au Lowasa kuwaandikia psrc? na nnadhani Lowasa ameweka wazi kabisa kuwa sheria zifuatwe. Bado nnashangaa tatizo ni nini?
Sidhani kwa wale wanaosema kuwa awamu hii itaimaliza nchi walikuwepo wakati awamu ya kwanza inang'atuka, kwa kuwakumbusha tuu, hakuna awamu iliiwaacha nchi hii kavu na kwenye umaskini mkubwa kama awamu ya kwanza, awamu ya msifiwa nyerere.
NYERERE alivyong'atuka, benki kuu iliwashwa moto na kaikubakishwa hata dola moja ya kufutia machozi, Jee mnakumbuka? NYERERE alivyong'atuka,tulikuwa hata mafuta ya kwenye gari hatuna kwa kuwa tulikuwa hatuna fedha za nje za kununulia, kumbuka mzee ruksa alivyochukuwa nchi aliwaita wazee wa dar pale diamond akawaelezea kuhusu hili na ikambidi atumie mbinu za haraka za kwenda kuomba libya na imf na iran na kwingineko (hotuba ya mikuki miwili, mzee ruksa diamond.
Yaani hatukumbuki tulivyokuwa tunapangishwa foleni za unga, mchele, sukari, sabuni,viwembe, viberiti. KWA KIFUPI HATA WEMBE WA KUNYOLEA ilIkuwa hakuna BILA FOLENI
Nadhani wengi mnaoandika humu kusemasema hovyo, kama hii mada ya Lowasa, hata sijui tatizo nini? Nadhani wakati wa nyerere mlikuwa hampo au kwa waliokuwepo na wanachangia habari hizi zisizo na mantiki, basi ni wafupi wa kumbukumbu.
Sasa jamani mbona yeye (nyerere) hatumsemi alivyotuwacha pabaya kiuchumi! tunamsifu tuu?
Hebu waacheni hawa kina lowasa na kikwete wafanye vitu vyao, JEE, kwa ukweli wenu kabisa hamuoni kazi wanayoifanya? au ni chuki tuu za kibinafsi?
Kaangalie neno chuki binafsi kwenye kamusi ya kiswahili lina maana gani kabla ya kuja kukurupuka hapa.