Is God fair ?

Hoja yangu ni logic.

Kwamba ukweli una logical consistency.

Maelezo yenu ya mungu (regardless ya yalipotoka) hayana logical consistency.

Nje ya vitabu vya dini hakuna suala la kuwapo kwa mungu unayemsema.

Inamaana kumbe wewe haujapinga uwepo wa Mungu ila unapinga Mungu wa kwenye vitabu?
 
Hapana, siwezi kukujibuni mkupuo mara zaidi ya nne huku nyie hamjibu maswali yangu.

Hata penalty kick huwa hazipigwi zote tano na timu moja halafu tano zingine zipigwe na timu nyingine.

Unajuaje kwamba katika majibu yenu siwezi kupata zaidi ya kujadili?

Unanimyima haki yangu ya kujadili sawa na kujibiwa maswali yangu.

Zaidi, unaonekana unaogopa kujibu kwa sababu huna majibu.
 
Ndiyo maana nikakwambia jenga hoja ya kupinga Mungu nje ya vitabu vya dini.

Ila Uwezo wa kukuthibitishia kuwa ni maneno ya Mungu ninao na huwezi kupinga hata chembe.

Hoja yangu ya kupinga mungu nje ya vitabu vya dini mbona nishaisema hapa?

Wewe hufuatilii tu.
Nimeaema, mungu aliyekamilika yote hana haja ya kuumba chochote, kwa sababu kakamilika kwa yote.

Kiwepo kwetu kunainyesha hakuna mungu aliyekamikika kwa yote.

Ambaye ndiye mungu pekee worth debating.
 
Hoja yangu ni logic.

Kwamba ukweli una logical consistency.

Maelezo yenu ya mungu (regardless ya yalipotoka) hayana logical consistency.

Nje ya vitabu vya dini hakuna suala la kuwapo kwa mungu unayemsema.

LOGIC LOGIC !Logic ni nini na ni nini/nani kazitengeneza ?

umekuwa ukijitawala kushusha kariri zako bila kutolea maelezo nawe wapeta tu kutujazia majinga majinga tu.
 
mbona wewe kila jibu unalopewa linazaa swali lakini wewe unataka ujibiwe tu.
mbona kuna maswali yameulizwa mara nyingi lakini una act vile kama huyaoni ?
 
Sasa ndiyo nini ulichokiongea hebu weka vizuri hoja yako,yani kuwepo sie binadamu ndiyo ushahidi ya kuwa hakuna Mungu?au mie sijakuelewa?
 
Sasa ndiyo nini ulichokiongea hebu weka vizuri hoja yako,yani kuwepo sie binadamu ndiyo ushahidi ya kuwa hakuna Mungu?au mie sijakuelewa?

Mungu mwenye uwezo wote, ukamilifu wote na ujuzi wote kwa nini ahitaji kuumba binadamu?

Kuhitaji kokote, pamoja na kuhitaji kuumba, si kupungua ukamilifu?

Mungu mkamilifu angejitosheleza mwenyewe.

Kwa nini kaumba binadamu?
 
Yeye ndiye muumbaji na ndiye mwenye haki ya kufanya atakavyo.
 
Hujajibu maswali.

Umeyakimbia tu.
 
Last edited by a moderator:

Na tatizo ni wewe kwa kuhoji vitu visivyo na mantiki baada ya kujibiwa maswali yako vizuri.
 
Mungu mwenye uwezo wote, ukamilifu wote na ujuzi wote kwa nini ahitaji kuumba binadamu?

Kuhitaji kokote, pamoja na kuhitaji luumba, si kupungua ukamilifu?

Mungu mkamilifu angejitosheleza mwenyewe.

Kwa nini kaumba binadamu?
kirangaa unatisha asee bravooooo
 
Hoja ni upendeleo,ndiyo nikakupa huo mfano kwahiyo ikiwa hao matajiri hawataki kuwasaidia watu basi sie hatuwezi kuwalaumu,Je vp umlaumu Mungu aliyeumba viumbe(vyake) na kuchagua yupi awe hayawani na yupi asiwe hivyo? Hakuna wa kumuhoji hata angetaka wote muwe machizi nani atahoji? kama matajiri tu hatuwezi kuwahoji hela zao pindi wasipotaka kuzitoa.
 
Hujajibu maswali.

Umeyakimbia tu.

Hakuna swali nimelikimbia na sina sababu ya kukimbia swali toka kwa mtu ambaye nafahamu uwezo wake wa kufikiri umeghoshiwa.
nimekumbusha kwamba usitake upewe jibu la roho kisayansi na sijui kama visivyovya kisayansi ubongo wako unavihimili...
umejibiwa sana kuhusu ROHO sijajua ni kwa nini warejea swali mara kwa mara
 
Mungu mwenye uwezo wote, ukamilifu wote na ujuzi wote kwa nini ahitaji kuumba binadamu?

Kuhitaji kokote, pamoja na kuhitaji luumba, si kupungua ukamilifu?

Mungu mkamilifu angejitosheleza mwenyewe.

Kwa nini kaumba binadamu?

Umesahau kuwa ana sifa ya kuumba, na sie hatumsaidii chochote wala kumpunguzia chochote,anaonesha uwezo wake wa uumbaji na sie ndiyo wahitaji kwake.
 
Kabla ya kusema sana habari za roho, unaweza kuthibitisha kwamba roho ipo na si hadithi za uongo tu?
 
mbona wewe kila jibu unalopewa linazaa swali lakini wewe unataka ujibiwe tu.
mbona kuna maswali yameulizwa mara nyingi lakini una act vile kama huyaoni ?

Nimejibu maswali yenu ya upepo ni nini na unapimwaje

Nijibu na wewe roho ni nini na inapimwaje na kuthibitishwaje kwamba ipo na si hadithi za uongo tu?
 
Umesahau kuwa ana sifa ya kuumba, na sie hatumsaidii chochote wala kumpunguzia chochote,anaonesha uwezo wake wa uumbaji na sie ndiyo wahitaji kwake.

Anaonyesha uwezo wake wa uumbaji kwa nani? Ili iweje? Anahitaji nini mpaka atake kuonyesha uwezo wake hivyo? Asipoonyesha atakosa nini?
 
God is fair,righteiuos and just.Shetani huleta matatizo aangushe watu wa Mungu,ila Mungu hutumia matatizo kukutana na watu wake..Mema yote tuyaonayo,ni ufumbuzi wa matatizo..Matatizo yanaleta ladha ya maisha.akisema kuwa yy ndo mponyaji,it means hawezi kukuponya bila wewe kuugua..ndo maana akawa mponyaji..#misuliyaimani #ambwene
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…