Mimi naamini Mungu lakini sijawahi hata siku moja kuona mwamini Mungu mwenzangu akijibu hoja zako kwa ufasaha hapa JF.
Ni afadhari mimi ninayeamini Mungu yupo kwani siku ya mwisho hata kama kweli hayupo i will lose nothing.
Sasa mbona unakanyaga matapishi yako mwenyewe!
Lete hoja za kupinga Mungu nje ya vitabu vya dini.
Kwanza kabisa objection si kwamba ulimwengu unanikera, bali ni kwamba ilimwengu inapingana na nature yake ya mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote.
Pili ingekuwa vizuri unaposema nilishajibiwa unipe link.
Maana unaweza kufikiri umejibu muafaka kwa kusema :mungu haulizwi kwa nini kafanya hiki au kile", mimi nikakwambia hilo si jibu, ni kukinali kwamba hujui jibu.
Unaposema mungu katofautisha viymbe vyake, wengine kawapa akili ya kufikiri, wengine hayawani, huyu mungu gani ana ubaguzi?
Kwa nini wengine kawapa akili na wengine kawafanya hayawani wakati alikuwa na uwezo wa kuwapa akili wote bila ya kipungukiwa na kitu?
Kwa nini hawa hayawani kawabania? Wamemkosea nini? Yeye si mungu wa upendo wote? Mbona anapendelea viumbe wake wengine anawapa akili ya kichambua mema na mabaya, wengine anawafanya hayawani?
Huyu mungu ana upendo wote kweli?
Huyu mungu yupo kweli?
Upepo ni mwendo wa hewa kwa mawimbi kutoka eneo lenye presha kubwa kwenda kwenye presha ndogo, unapimwa kwa kipimo kinachoitwa anemometer kinachoweza kupima upepo unaelekea wapi na kwa kasi gani.
Anemometer - Wikipedia, the free encyclopedia
Roho ni nini na inapimwa kwa kipimo gani?
Tatizo unanipa ushahidi wa maandiko ya mungu badala ya kunipa ishahidi wa uwepo wa mungu.
Sababu unajengea hoja kwa kutumia maneno ya Mungu,hivyo jenga hoja nje ya maneno ya Mungu.
Upepo ni mwendo wa hewa kwa mawimbi kutoka eneo lenye presha kubwa kwenda kwenye presha ndogo, unapimwa kwa kipimo kinachoitwa anemometer kinachoweza kupima upepo unaelekea wapi na kwa kasi gani.
http://en.m.wikipedia.org/wiki/Anemometer
Roho ni nini na inapimwa kwa kipimo gani?
Kama mungu yupo, muweza yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote, kwa nini kaumba dunia ambayo ina uwezekano wa kuwa na mabaya, mateso, dhiki, etc wakati alikuwa na iwezo wa kuumba dunia ambayo hivyo haviwezekani?
Katika ulichonukuu, wapi kumetajwa kitabu cha dini?
Matapishi gani hayo unayoyasema?
Bill Gates kanywa maji yaliyochujwa kutoka mavi, wewe unaona hatari kula matapishi tu?
Hewa ni nini ?
presha kubwa na presha ndogo ni nini ?
kwanini iwe ni presha inasababisha na sio kitu kingine ?
Narudia tena kusema kwamba
Mungu angetaka kuumba ulimwengu ambao watu
hawafanyi maovu,basi yeye angejua kila kitu kuhusu hivyo viumbe kabla hata hayajatokea mwanzo hadi mwisho(sababu ni mjuzi wa yote).Na pia yeye ndiyo angepanga kila kitu kuhusu hao viumbe,hakuna ambacho
kingetokea pasina yeye kukitaka
kutokea,hivyo Mungu anaumba na
hufanya vile atakavyo sababu ndiyo mwenye nguvu na muweza yote. Sasa tunapokuja kwenye ulimwengu wetu ambao tunafanya maovu na mambo mengine,ni vilevile tu kwamba Mungu
anayajua yote ambayo tunayoyafanya na ambayo bado kuyafanya,Yote ambayo yanatokea ktk ulimwengu basi ni yeye(mwenye uwezo wa yote)
ndiyo ametaka yatokee hakuna
kinachotokea ambacho hakikuwa ni matakwa yake. Matakwa yake yapo aina:yapo ya aina mbili,kuna mipangilio ya kiulimwengu ambayo kama kuchomoza kwa jua na kuzama,mvu n.k(na ndiyo ktk dalili za uwepo wake), hayo yote ni matakwa yake..halafu matakwa ya aina ya pili ndiyo haya tunayofanya sisi kama hayo maovu na mengineyo,ametuacha tufanye
tutakavyo lakini ni ndani ya matakwa yake,kwa maana hiyo ambalo hatolitaka hatutoweza kulifanya.Ndiyo maana anasema kuwa anaumba na kufanya atakavyo. Nalaiti angependa hao wanaofanya maovu kutokufanya hayn maovu basi wasingefanya,kama alivyowafanya malaika.
Unahoji upendo wa Mungu,sasa huo upendo wa Mungu umeusikia wapi wewe kama sio vitabu vya dini(maneno ya Mungu ambaye hauamini kama yupo)?
Kwanza kabisa objection si kwamba ulimwengu unanikera, bali ni kwamba ilimwengu inapingana na nature yake ya mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote.
Pili ingekuwa vizuri unaposema nilishajibiwa unipe link.
Maana unaweza kufikiri umejibu muafaka kwa kusema :mungu haulizwi kwa nini kafanya hiki au kile", mimi nikakwambia hilo si jibu, ni kukinali kwamba hujui jibu.
Unaposema mungu katofautisha viymbe vyake, wengine kawapa akili ya kufikiri, wengine hayawani, huyu mungu gani ana ubaguzi?
Kwa nini wengine kawapa akili na wengine kawafanya hayawani wakati alikuwa na uwezo wa kuwapa akili wote bila ya kipungukiwa na kitu?
Kwa nini hawa hayawani kawabania? Wamemkosea nini? Yeye si mungu wa upendo wote? Mbona anapendelea viumbe wake wengine anawapa akili ya kichambua mema na mabaya, wengine anawafanya hayawani?
Huyu mungu ana upendo wote kweli?
Huyu mungu yupo kweli?
Hewa ni mchanvanyiko wa gas mbalimbali.
Presha kubwa na ndogo ni matokeo ya mtiririko wa uzito wa molekyuli za hewa.
Ni presha inayosababisha na si kitu kingine kwa mujibu wa second law of thermodynamics.
Maswali yenu nawajibu, swali langu hamjajibu.
Unaweza kuyjibitisha roho ipo? Kwa kipimo gani?
Hiyo sio hoja kabisa tena ni vichekesho.
Hivi hawa masikini waliyopo duniani na wakati kuna matajiri kibao na wanahela nyingi kupitiliza, Je tunaweza kuwalaumu na kusema wanaroho mbaya kwa kutokuwapa hizo hela zao masikini?
Itasemaje najengea hoja maneno ya mungu kabla hujathibitisha kwamba mungu yupo?
Umejuaje maneno haya ni ya mungu na si ya binadamu tu kabla hujathibitisha kuwepo kwa mungu?
gas ni nini ? gas inasababishwa na nini/nani ?
molekyuli ni nini na zinasababishwa na nini / nani ?
second law of thermodynamics nani aliitengeneza au kuiweka ?
nani kakwambia umemaliza kujibu maswali yetu ?
Ndiyo maana nikakwambia jenga hoja ya kupinga Mungu nje ya vitabu vya dini.
Itasemaje najengea hoja maneno ya mungu kabla hujathibitisha kwamba mungu yupo?
Umejuaje maneno haya ni ya mungu na si ya binadamu tu kabla hujathibitisha kuwepo kwa mungu?
Nimejibu maswali mara ai chini ya nne mfululizo.
Kabla ya kuendelea kujibu, ili nisiuelemee sana upande wako kwa kujibu maswali yenu sana bila ya yangu kujibiwa, nakupa nafasi ujibu swali langu.
Roho ni nini? Unathibitishaje kwamba ipo na si hadithi ya uongo tu? Kwa kipimo gani?