Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,763
- 145,548
Ni vigumu saa nyingine kupata majibu
Ni vigumu kupata majibu kama utalazimisha uwepo wa mungu.
Ukiweka uwezekano wa mungu kutokuwepo, kwamba ni story tu katungwa na wanadamu, everything makes sense.
Ushenzi unaoendelea duniani all of a sudden hauwi mgumu kuuelezea, hakuna mungu mwenye uwezo wote na upendo wote wa kuuzuia.
Lakini ukisema kuna mungu, mwenye upendo wote na uwezo wote, huwezi kuelezea kwa nini kaumba dunia ambayo mabaya yanawezekanika wakati alikuwa na uwezo wa kuumba dunia ambayo mabaya hayawezekaniki.
Hata binadamu tu mwenye roho nzuri akiwa na uwezo wa kuwapa wanawe good time anawapa.
Inakuwaje mungu mwenye uwezo wote na upendo wote awe na uwezo wa kutupa good time halafu atubanie?