Serikali ya CCM iache mbinu hizi ambazo tulishazijua. Serikali ikatatue tatizo la msingi la MZOZO WA MIONGO KADHAA KATI YAKE NA WAISLAMU. CCM iwaache waislamu watafute uongozi wao huru kabisa, wanaouamini. Kufikiri ATI maoni ya waislamu yataendelea kusimamiwa, kuratibiwa na kuongozwa na BAKWATA ni kupoteza muda na kijidanganya. Mbona sisi wakristu tuna taasisi zetu muhimu na imara za kidini na tunaziamini? Kwa nini serikali ya CCM inaendelea kuwashika waislamu na kuwadhibiti kwa kuitumia taasisi ambayo waislamu hawaiamini?"
................."Ikiwa atauawa Ponda mmoja eti kwa sababu anadhaniwa kuwa "mtu hatari", in the next morning watazaliwa Ponda wengine hatari zaidi wapatao 1000. Uhuru wa Dokta hauzimwi kwa RISASI."
Julius Mtatiro,