Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,205
- 10,953
Kwa mara nyengine tena Israel imekiri kuzidiwa nguvu na idadi ya vikombora vinavyorushwa na wanamgambo wa makundi tofauti kutoka Gaza. Taarifa hizo zimekuja katikati ya muendelezo wa machafuko makubwa yanayoendelea eneo la Jerusalem tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Katika mapigano haya mapya jumla ya wapalestina 28 wameshauliwa na mashambulizi ya ndege za kivita za Israel na waisrael 2 wamefariki kwenye mji wa Ashkeldon ambako mamia ya makombora kutoka Gaza huwa yanatua na kusababisha uharibifu wa majumba.
Makombora mengine machache kutoka Gaza yamefanikiwa kufika mbali hadi mji wa mkuu wa Telaviv ambako vingora kutoka jeshine vimewalazimisha wakazi wake kukimbilia sehemu za chini ya ardhi kujificha.