Iron Dome ya Israel yazidiwa nguvu na vikombora vya wapalestina

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,017
10,653
Kwa mara nyengine tena Israel imekiri kuzidiwa nguvu na idadi ya vikombora vinavyorushwa na wanamgambo wa makundi tofauti kutoka Gaza. Taarifa hizo zimekuja katikati ya muendelezo wa machafuko makubwa yanayoendelea eneo la Jerusalem tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika mapigano haya mapya jumla ya wapalestina 28 wameshauliwa na mashambulizi ya ndege za kivita za Israel na waisrael 2 wamefariki kwenye mji wa Ashkeldon ambako mamia ya makombora kutoka Gaza huwa yanatua na kusababisha uharibifu wa majumba.

Makombora mengine machache kutoka Gaza yamefanikiwa kufika mbali hadi mji wa mkuu wa Telaviv ambako vingora kutoka jeshine vimewalazimisha wakazi wake kukimbilia sehemu za chini ya ardhi kujificha.

1620766490307.png
 
Iron Dom hawezi Linda kila eneo. Wakitaka kujua ina nguvu kiasi gani wajaribu kushambulia maeneo muhimu
Mambo mengine bwana! Kwa hiyo kwa maoni yako maeneo ya Jerusaleem na Tela Aviv hayana umuhimu?

Usiku huu nimeangali kwenye TV jinsi Iron Dome zilivyo zidiwa na maroketi ya wapalestina - yaani aibu tupu, mbwembwe zote za kuipigia debe na propaganda uchwara kwamba Iron DOME ndio baba lao kumbe wapi? Nilishangaa zilipo rushwa roketi tano Tela Aviv - Dome ikadhibiti moja tu nne zikapenya - sasa wanakuja na visingizio eti roketi za kipalestina wamezifanyia marekebisho zinaruka parallel na aridhi hazichukui mtindo wa ki-projectile hivyo si rahisi kuonekana kwenye scanning radar ili system ifanye mahesabu ya uhakika wapi pa kuzi-intercept - nilipo sikia kisingizio hicho cha Wayahudi nilicheka sana na kuwasikitikia, nikajua hapo Iran imekwisha wapa mbinu na wafunzo Wapalestina jinsi ya kuwazidi kete Waisrael.

Usiku huu tena nikaona matela yamebeba vifaru kwenda Gaza eti kuwamaliza wapiganaji wa kipalestina wanao rusha roketi, yaani mara hii Israel imekwisha sahau vifaru vyake vilivyo teketezwa huko Lebanon 2016 baada ya kuingia kichwa kichwa huko, hawakuamini macho yao, leo hii tena mjinga huyu Natenyahu anataka Wayahudi wapate balaa nyingine tena kwa kuvamia Gaza - hataki kuondoka madarakani anag'ang'ania kama luba - anaogopa kushtakiwa akiondoka madarakani - vita hii ndio itamumaliza kisiasa - akumbuke kwamba vita hii wapalestina hawapo peke yao huko Gaza,watasaidiana na kundi la Hezibolla,Wairan, Syria, Wa Lebanon na Waturuki,yaani dalili zinaonyesha Wapalestina wamejipanga kweli kweli ku-deal na ujeuri wa Natenyahu na genge lake vilivyo, wamefikia hatua ya kuvurumisha mpaka roketi za masafa marefu yenye uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa sana sana, nimeona kwenye TV live madhara ya makombora hayo si mchezo, Israel hisipo kuwa makini this time around watakuja kuaibika.
 
Mambo mengine bwana! Kwa hiyo kwa maoni yake maeneo ya Jerusaleem na Tela Aviv hayana muhimu? Nimeangali kwenye TV jinsi Iron Dome zilivyo zidiwa na maroketi ya wapalestina - aibu tupu, yaani mbwembwe zote zakuipigia debe na propaganda uchwara kwamba Iron DOME ndio baba lao kumbe wapi? Nilishangaa zilipo rushwa roketi tano Tela Aviv...
Sawa mwarabu mweusi 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sasa wamezidiwa vipi? Waisrael waliuwawa mpaka sasa ni wawili tu kwa mujibu wa taarifa yako. Wapalestine mpaka sasa wameshauwawa watu 28.

Sasa wepi wamezidiwa? Wapalestine au Waisraeli??
Mkuu kinacho isaidia Israel ni kwamba yale maroketi yana uwezo mdogo wa kusababisha mripuko kutokana na kwamba yametengenezwa kwa teknorojia duni, maana hayo maroketi yana tengenezwa kienyeji tu.

Na mbaya zaidi hayo maroketi yana kasi ndogo kwa hiyo ni rahisi kwa mifumo ya ulinzi ya Israel kakabiliana nayo lakini bado wameshidwa kuyazuia.

Hivi mkuu umesha fikiria ni hali gani ambayo wangekuwa nayo Israel iwapo hayo maroketi yangekuwa na uwezo sawa na kakombora ambayo Iran iliyatumia kukishambulia na kukiharibu kituo cha kijeshi cha Marekani?
 
Mambo mengine bwana! Kwa hiyo kwa maoni yako maeneo ya Jerusaleem na Tela Aviv hayana umuhimu?

Usiku huu nimeangali kwenye TV jinsi Iron Dome zilivyo zidiwa na maroketi ya wapalestina - yaani aibu tupu, mbwembwe zote za kuipigia debe na propaganda uchwara kwamba Iron DOME ndio baba lao kumbe wapi? Nilishangaa zilipo rushwa roketi tano Tela Aviv
Ngapi ngapi
 
Mambo mengine bwana! Kwa hiyo kwa maoni yako maeneo ya Jerusaleem na Tela Aviv hayana umuhimu?

Usiku huu nimeangali kwenye TV jinsi Iron Dome zilivyo zidiwa na maroketi ya wapalestina - yaani aibu tupu, mbwembwe zote za kuipigia debe na propaganda uchwara kwamba Iron DOME ndio baba lao kumbe wapi?...
Hakuna kitu kinazuia silaha huwa ni porojo tuu hizo
 
Back
Top Bottom