EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
IDADI ya watu wanaoripoti kunyanyaswa kijinsia wilayani Iringa mkoani Iringa imeongezeka huku ukatili wa kingono ukiwa kwa asilimia 29 juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 20. Watu 219 wakiwemo watoto 11 na wanaume 51 wameripoti makosa ya kunyanyaswa kijinsia kati ya Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu, mengi yakiwa ya kingono na kipigo.
Matukio hayo yameripotiwa kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto wa Vijijini (Tarwoc) kupitia kituo chake cha Family Drop in Centre cha mjini Iringa. Meneja Mradi wa kituo hicho, Amani Nduhise alisema juzi kuwa ili kurahisisha kazi yao, mradi wao wa kupambana na unyanyasaji wa kijinsia unafanya kazi kwa karibu na Polisi, Mahakama na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto.
Alisema ili kurahisisha upatikaji wa taarifa sahihi, mradi wao umepata mabalozi wa kujitolea kutoka katika kila kata watakaokuwa na wajibu wa kufuatilia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yote ya kata zao.
Alisema wakati mradi huo unafanya kazi katika kata zote 16 za Manispaa ya Iringa, Iringa vijijini kata zilizoingizwa katika mradi huo ni Ifunda, Mseke, Kihorogota na Kisinga. Kwa mujibu wa Nduhise, mabalozi 20 watakaofanya kazi katika kata hizo watapewa mafunzo ya kuwawezesha kushiriki kukabiliana na vitendo vyote vya unyanyasaji.
Meneja Utawala na Fedha wa mradi huo, Beatus Magoti alisema katika mafunzo hayo mabalozi hao watafanya kazi ya usuluhishi na utetezi na kuziwasilisha taarifa za vitendo hivyo katika ngazi za uongozi na mradi kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya Dola kama kutakuwa na haja.
HabariLeo | Iringa yavuka wastani ukatili wa kingono