A
Anonymous
Guest
Napenda kuwasilisha malalamiko rasmi kuhusu hali ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kinachojulikana kama Shalom Center, kilichopo Kisongo, Arusha.
Kwa masikitiko makubwa, kuna taarifa zinazoonyesha kuwa watoto katika kituo hicho wanakumbana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa hali ya juu, ikiwemo:
Kutokana na uzito wa tuhuma hizi, naomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kufanya uchunguzi wa kina juu ya kituo hiki, kulinda usalama wa watoto waliopo hapo, na kuwawajibisha wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivi vya ukatili.
Afya, usalama, na haki za watoto lazima zilindwe kwa gharama yoyote.
Kwa masikitiko makubwa, kuna taarifa zinazoonyesha kuwa watoto katika kituo hicho wanakumbana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa hali ya juu, ikiwemo:
- Kukosa lishe bora na mlo kamili, hali inayosababisha baadhi ya watoto, hususan walio chini ya umri wa miaka 5, kuonyesha dalili za utapiamlo.
- Adhabu kali na za kikatili kutoka kwa walezi, ikiwa ni pamoja na kupigwa kwa kutumia fimbo, mwiko, mateke na vipigo vinavyosababisha majeraha na makovu ya kudumu.
- Watoto kutumikishwa kazi zisizowafaa, ikiwemo kufanya kazi za ndani (house girls) katika familia za baadhi ya wafanyakazi.
- Baadhi ya watoto kupelekwa kufanya kazi katika biashara za mkurugenzi (ikiwemo duka lililopo Iringa), pamoja na madai ya unyanyasaji wa kingono unaofanywa na baadhi ya ndugu wa mmiliki wa kituo.
- Wafanyakazi wa kituo kutishwa kufukuzwa kazi endapo watajaribu kuripoti au kupinga vitendo hivi.
- Misaada inayotolewa na wafadhili kutowafikia watoto kama ilivyokusudiwa.