Iran yawakamata majasusi 17 wa CIA

comrade wetu

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
964
605

Serikali ya Jamhuri ya watu wa Iran imesema imewakamata majasusi 17 wanaofanya kazi katika Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, na wengine wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Televisheni ya taifa ya Iran imemnukuu afisa wa wizara ya ujasusi akisema kuwa pia imelivunja genge la majasusi hao.

Afisa huyo amesema waliokamatwa wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Tangazo hilo limetolewa miezi mitatu tangu kuzuka kwa mvutano na mataifa ya Magharibi ulioanza wakati Marekani ilipoweka vikwazo vikali kwa Iran ambavyo vilianza rasmi mwezi Mei.

Wiki iliyopita, Iran iliikamata meli ya mafuta yenye bendera ya Uingereza katika Mlango Bahari wa Hormuz, baada ya Uingereza kuikamata meli ya mafuta ya Iran kwenye pwani ya Gibraltar, Julai 4.

Haijajulikana wazi kama kukamatwa majasusi hao kunahusiana na kesi ambayo Iran ilisema mwezi Juni kuwa imegundua mtandao mkubwa wa kijasusi iliyodai unaendeshwa na CIA na kwamba majasusi kadhaa wa Marekani walikamatwa katika nchi tofauti.
 
Mbona trump jana kakanusha kuwa si za kweli ni uongo

Na wangefanikisha malengo yao ungekuja hapa kuwasifu kuwa majasusi wa CIA wametimiza malengo yao na usingelalamika, ivi kwani nyinyi mnakosa kulalamika kwa Irani?
Umepata na habari za upande wa pili au kila kisemwacho humu jamvini kuhusu Iran huwa ni cha kweli kwako?
 
Ukamate zizi lote hilo hata mmoja wao kusema kaneno asiseme.
Hata majina yao
 
Tumia Google, dunia kiganjanu siku hizi, mashirika yote ya habari makubwa duniani yameweka hizo habari. Usingoje kila kitu kuletewa.
Kwa vile Iran wamesema,lazima google itakuwepo tu,Hlafu google hata wewe unaweza kuandika chochote tu...Nakumbuka kipindi walikamata boti ya US walituwekea hadi na picha na video za hao wanajeshi..Sasa kwa hili naona hata picha hamna...
 
Back
Top Bottom