Inasikitisha kuona kwamba mbinu za 'watawala dunia' siku zote hufanikiwa. Kwa kweli Iran itakaposalimu amri kutakuwa hakuna tena hope ya kuweza kupambana na mfumo wa dunia 'world order' ulioko hivi sasa, kwani ni Iran pekee iliyokuwa 'haiogopi' kuupa shinikizo mfumo huo, kwa maneno na vitendo.
Wakati vuta -nikuvute baina ya Iran na mataifa ya magharibi na vibaraka wao (Waarabu) inaendelea, siku zote nilifikiria kuwa safari hii dola linalopingana na hawa litashinda. Lakini matukio yanayoendelea hivi sasa Iran, yaliyosababishwa na vikwazo ambavyo havijawahi kuwekewa taifa lolote duniani, hata former Soviet Union, yananifanya nikate tamaa. Labda tuangalie kitu gani kimepelekea kwenye hali hii ambayo sioni kuwa Iran itaibuka mshindi.
Binafsi naona kosa kubwa limesababishwa na mgando 'rigidity' ya uongozi wa Iran baada ya kuja Ahmedinedjad. Pamoja na mambo mengi mazuri aliyoyafanya, Ahmedinedjad amekuwa 'dogmatic' sana badala ya kuwa 'practical' kama rais aliyetangulia. Suala la nguvu za nuklia, ambalo kwa kweli naamini Iran haina haja hivi sasa ya kutengeneza silaha, lilipaswa kuendeshwa kwa ujanja mkubwa na mitego ya kisiasa, badala ya kuvumburuka na kuweweseka kila siku, mara kwa kukanusha Holocaust mara nyingine kwa kuitishia Israel. Ukweli ni kuwa nchi za Magharibi na hasa Marekani ni makoloni ya Israel na hayana hiari isipokuwa kufanya kile Israel inachotaka. Mtu anayetaka kujua undani kwa nini Israel ina nguvu hizi na asome historia ya mapinduzi ya Bolshevik. Kuna video nyingi kwenye utube pia zinazoelezea vizuri.
Yaelekea Ahmedinedjad na Khamenai hawajui vizuri jinsi gani mtandao wa wanaojiita Wayahudi ni mkubwa kiasi gani na ulioanza zaidi ya miaka 150 iliyopita kusuka mambo tunayoyaona hii leo. Ili kuushinda ilibidi waufahamu vizuri na kwenda nao kijanja. Mapambano dhidi ya mtandao huo, Uzayuni, yatachukua kwa uchache miaka 50 (Uzayuni ni mkuba kuliko Israel. Israel ni sehemu tu ya mpango mzima wa Uzayuni).
Si rahisi kuwalaumu viongozi wa Iran pekee, kwani mambo haya ni 'too complicated' kiasi kwamba wengi hapa hamtafahamu ninazungumzia nini! Mapambano ya kujinasua kutoka utawala wa dunia wa hawa jamaa ni makubwa mno na yanahitajia nchi nyingi zishirikiane. Nchi moja pekee haiwezi.
Ila kitu cha kulaumu ni kuwa Ahmedinedjad na Khamenai wanaona mapambano haya yatakwisha katika miaka michache tu na katika kipindi cha utawala wao! Hilo ndio kosa kuu walilofanya.
Haya niyaandikayo hayana uhusiano wowote na dini. Kama utadhani hivyo basi yaelekea hufahamu nazungumzia nini. Mfumo wa sasa wa dunia kwa kweli unaongozwa na watu wanaopinga dini-dini yeyote- infact, wengi huwaita 'Satanists' kwamba wanaabudu mashetani. Isipokuwa mara kwa mara wanatumia dini kuu:Uislamu,Ukristo,Uyahudi, Hindu nk kuendeleza mipango yao.
Very good starting point, ni kwamba tunalo tatizo ulimwenguni? Na kama hakuna tatizo basi haina haja ya kuendelea kwa maana kama ulivyosema hapo juu, watu watakuwa hawafahamu nini kinazungumzwa.
Na nini ufumbuzi wake?
1. Je ufumbuzi huu upo hapa hapa ulimwenguni au inabidi tuulete kutoka sayari nyengine? Mimi naamini upo hapahapa ulimwenguni, na wala hatuhitaji kuutoa kutoka sayari nyengine ya dunia.
2. Je nani anaujua ulipo ufumbuzi huo? Mimi naona kuuona ufumbuzi huo inawezekana kuwa rahisi au kuwa ni vigumu saaana kutegemeana na state of mind ya mtu au watu(yaani ni free thinking mind au ni mind iliyokuwa tayari imeshakuwa-contaminated na hao Mazayuni kwa njia mbali mbali). Maana kumbuka kwamba nao hawapati usingizi katika kuhakikisha kwamba watu hawaigundui hiyo hazina ambayo kiukweli hata wao wanaijuwa fika ilipo ni wapi.
3. Ni nini quality za ufumbuzi huo? Bila ya shaka ni lazima iwe alternative system of life (every aspect of huma life: individual, social, economic, national, global, etc, most importantly in the engine room of human life-spiritual)maana hatuwezi kutegemea kuondosha "system moja dhalimu" na ku-replace with "nothing or no system", can we?. Ama kutambua quality za system hiyo ni lazima mtu au watu a/w/afanye uchambuzi wa kina katika critical appraisal (analysis) ya alternative systems ambazo either tulizonazo hapa tayari ulimwenguni au kuzitoa kutoka sayari nyengine, maana watu (hao Wazayuni na makoloni yao)wana vituko vingi, kama ilivyo kawaida yao wao wao kujifanya kuwa wanaleta ufumbuzi, wanaweza wao wao kuleta mifumo (systems)na kudai kwamba inatoka Mars au Venus, etc, na bado still kuna watu hata humu jamvini, wataamini na kuisifia, maana akili zao tayari zimeshavurugwa na hao Wazayuni na makoloni yao. Hivyo pointi namba 2 hapo juu ni muhimu saana, FREE THINKING, UNBIASED, RATIONAL, REASONABLE STATE OF MIND.
4. Je, in urefu gani safari hii?
All the best to everyone, na zichambuliwe systems (mifumo) mbali mbali na category mbali mbali za mifumo hiyo. Kwa kuwa lengo letu ni ufumbuzi, basi sio vizuri na ni kujitia upofu na ufinyu wa fikra kama zitawekwa restrictions za mifumo, iwe ya kidini, iwe ya kidunia, ni kuchambua na kuendelea kuchambua, na silaha yetu kubwa na tegemezi iwe poit namba 2 above, FREE THINKING, UNBIASED, RATIONAL, REASONABLE STATE OF MIND au INTELLECT
Nafikiri itakuwa busara kulinganisha systems (mifumo) kinamna hii: mmoja wa kidini na mwengine wa kidunia, halafu wakidini na wakidini, halafu wakidunia na kidunia au mtiririko wowote katika hiyo. Na tuchukulie kwamba mfumo uliyojificha wa Zionism ndio huu tulionao ambao ni tatizo. Hivyo nini alternative kati ya mifumo hii na category ambayo tunatafuta uokozi kutoka systems hizo kwao ni mfumo wa kiuchumi. kwa Mfano:
1. Wa kidini ni Christianity na wa kidunia ni Communism
2. Second iwe wa kidini ni Budhism na kidunia ni Perestroika.
3.Tatu iwe wa kidini ni Hinduism na wa kidunia Ujamaa na kujitegemea.
4. Nne iwe wa kidini ni Islam na kidunia ni Capitalism.
N tuanze, pengine Mungu akitujaaliwa tutagundua system yenye kutufaa humo, na tukikosa tena tutasubiri hiyo tutakayoletewa kutoka Mars au Jupiter.